POTOSHI Tundu Lissu ametinga mahakamani akiwa amevaa T-shirt ya 'Oktoba tunatiki'

POTOSHI Tundu Lissu ametinga mahakamani akiwa amevaa T-shirt ya 'Oktoba tunatiki'

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
POTOSHILISSU19AG2025.jpg
 
Tunachokijua
Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu alisisitiza kusimamia agenda ya 'No reforms, No election' iliyotaka kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi, ili kuwezesha uhuru, haki na uwazi wakati wa Uchaguzi.

Mnamo tarehe 09 Aprili, 2025 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Tundu Lissu alikamatwa na jeshi la polisi mara baada ya mkutano wa hadhara alioufanya Jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma na kusafirishwa hadi Dar es Salaam na baadaye alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X ambapo kesi hiyo inaendelea leo Agosti 18, 2025


Madai

Kumekuwepo na Picha inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Tundu Lissu akiwa mahakamani akiwa amevalia T-shirt yenye maneno ya 'Oktoba tunatiki bilioni 86.31'

Ikumbukwe kuwa Oktoba tunatiki ni kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayotumika kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi mkuu 2025 kwa kwenda kupiga kura, na bilioni 86 kikiwa ni kiasi cha fedha za harambee ya CCM kuchangia Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na Urais ambapo ilifanikiwa kuchangisha Fedha zaidi ya Shilingi Billioni 86.


Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini picha halisi ilichapishwa Mwezi Mei 19, 2025 mpigaji wa picha hiyo akiwa ni Ericky Boniphace wa AFP wakati wa kesi katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hivyo picha hiyo, inayosambazwa mtandaoni imehaririwa kwa kuondolewa maneno ya 'No reforms, No election' na kuwekewa 'Oktoba Tunatiki' hatimaye kupotosha uhalisia.

AFP__20250519__479G4JY__v1__HighRes__TanzaniaPoliticsTrial-1747653119.jpg
Back
Top Bottom