Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ametufumbua macho na kutujaza kujiamini kuwa Tanzania hii ni mali ya watanzania wote

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ametufumbua macho na kutujaza kujiamini kuwa Tanzania hii ni mali ya watanzania wote

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Tangu ametoka kwenye tanuru la mateso makali na kubezwa na kukashifiwa na kuitwa majina mabaya ya kila aina hapa duniani.

Amekuwa ni mtu wa kufurahia sana kila anapokuwa anazungumzia hayo madhila yake aliyopitia, anafurahi muda wote.

Amezidi kuimarika zaidi kwa kujiamini kwa kila jambo analolifanya na hivyo kulisimamia, kitu uoga kwake imekuwa ni kitendawili.

Ameweza kuwa kiongozi wa mfano mzuri kwa watanzania kwa kutokuwa na moyo wa malipizi, sifa ambayo wanayo viongozi wateule tu.

Ametuonyesha kuwa hakuna kisichowezekana, ametufumbua macho na kutujaza kujiamini kuwa Tanzania hii ni mali ya watanzania wote.

Hakika mh Lissu ni mtume wa kulikomboa taifa letu, atatuvusha bahari ya matatizo na machungu ya maisha na kutuingiza kwenye nchi ya asali na maziwa.

TWENDE NA LISSU, TUMCHAGUE LISSU.

ANATUFAA WATANZANIA.

photo%20266%2012-18-0.jpg
 
Tundu Lisu na viongozi wa Chadema wanajua kabisa uchaguzi huu wanakwenda kushindwa kwa aibu kubwa na ndiomaana viongozi wengi wa juu wa Chadema Dalili zote zinaonyesha wamesha kata tamaa.
 
Ni mwanga kwa walio gizani, ni macho kwa wasiyo ona, ni sauti kwa wasiyo na sauti, ni tumaini kwa walio katishwa tamaa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]...wazee wa [emoji304]
 
Historia itamkumbuka sana. Huyu mwamba kwa ujasiri alioonyesha naamin kabisa anaweza kupambana na mabeberu kwa vitendo sio Jiwe hata vikao vya international community anakimbia kisa tu hajiamini na hawezi kujieleza, wote tumemshuhudia miaka hii mitano akikimbia vikao vya kimataifa, matokeo yake nchi yetu imepoteza nguvu na ushawishi iliyokua nayo

Tundu Lissu ni mtu sahihi wa kuirudisha Tanzania kama nchi kiongozi.
 
Back
Top Bottom