Watawala waovu walikuwa wameshawaaminisha watanzania kuwa tanzania ni mali ya watawala, na kwamba watawaliwa hawaruhusiwi kuhoji, wala kusema chochote zaidi ya kufuata kile kitakachoamuliwa na watawala, kuhoji ikawa kosa la jinai na kila mtu akaogopa kumuongea bwana yule akihofia usalama wake!
Ilikuwa ukitamka jina la bwana yule katika public basi ni katika kusifu na kumuabudu.
Ikafika mbali hata baadhi ya wajinga na wapumbavu wakamuita "mungu" na "yesu" mbaya zaidi eti wakadai ipo siku "MUNGU" atashuka kuja kumuomba msaada mtu yule, hii kufuru kabisa kuwahi kutokea, shame upon the dictator and his failed system!
Viva Mtanzania lissu, umewaondolea madikteta ule utukufu waliodhani wanao, walijifanya miungumtu, aibu yao sasa vile tunawadharau, sio kitu wao!