Hapo ndipo uongozi wa CHADEMA, nanyi wafuasi, msipojitambua kwa kumshamgmbulia Magufuli binafsi. Laiti mngejua yeye hafanyi yatokayo kichwani mwake bali anatekeleza Ilani ya CCM, 2015, vivyo hivyo, Lissu, mgombea wa CHADEMA, angerejea kueleza Ilani ya chama (kama ipo) imetekelezwa kwa kiwango gani.
Lissu, hapo alipo hana kipimo chochote cha uongozi, kama mtu binafsi wala kichama. Kibinafsi anatetea kupigwa kwake risasi, kichama hathubutu kueleza ruzuku imetumikaje ili wananchi wakiamini chama kupitia viongozu wake.
Shutuma na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za chama dhidi ya Mbowe, M/kiti bado ni mbichi kabisa, anapaswa kumsafisha kwanza, ili awe na uhalali wa kumshambulia Magufuli. Nafasi anayogombea inamtaka afanye hivyo, ili jamii iamini akipewa madaraka ya kuongoza nchi hii siyo tu atakemea ubadhirifu wa mali ya umma bali pia atachukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Hakuna haki isiyo na wajibu au uhuru usio na mipaka, kama ilivyo kwenye Katiba ya JMT (1977), Ibara ya 30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.