Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amjibu Magufuli: Kama kweli anampenda aseme wakina nani walimpiga risasi, na kwanini alimnyima pesa ya matibabu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amjibu Magufuli: Kama kweli anampenda aseme wakina nani walimpiga risasi, na kwanini alimnyima pesa ya matibabu

Yeye amependwa sasa hivi aachane na yaliyokwishapita.
 
Tatizo la mgombea wa CCM hana sera wala hoja nzito za kuweza kuwavutia wananchi, siku zote yeye huongea mambo rahisi rahisi tu ambayo yanaonekana ni yenye tija kwa watu wenye akili duni na upofu wa kufikiria. Viongozi makini duniani huwa hazungumzii vitu vyepesi ktk nyakati za kampeni za uraisi, bali hushusha nondo zilizojaa madini tupu.

Haya ndiyo mapungufu ya kiongozi wa nchi kukwepa kuongea ama kushauriana na viongozi wengine mashuhuri hapa duniani kwa kificho cha kubana matumizi. Kwa kuwa anajikuta hawezi kuongelea mambo muhimu yenye kugusa maslahi mapana ya Watanzania wenye fikra pana.
Duhh kwaiyo Lissu anasera? Yaani hizo zakupigwa risasi nazo ni sera? Nyumbu!
 
“Kwakuwa amesema ananipenda kama alivyodai akiwa Ikungi, Singida aseme ni akina nani walionipiga risasi 16,

Kwakuwa ananipenda aseme ni kwanini alininyima pesa za matibabu baada ya kupigwa risasi.." Mhe. @TunduALissu.

"Kwakuwa amesema ananipenda aseme ni nani aliyemkusudia auawe katika hotuba yake aliyoitoa wakati akipokea ripoti ya madini na kusema kuwa anamsumbua sumbua katika agenda yake ya madini na kwamba bora msaliti auwawe"-; Mhe. @TunduALissu

t.co / Twitter

Kampeni zimefika patamu .
 
Hilo swali la Lissu ni gumu sana, haliwezi kujibiwa kamwe, ndio maana siku hizi jamaa yetu anaonekana mpole sana, anajua wakati huu wa kampeni mengi sana yatasemwa, hasa yale asiyopenda kuyasikia, namshauri awe mvumilivu sana.
Na akileta vurugu tuna mng'oa kwa nguvu
 
Kama angeacha wapinzani waongee na magazeti na TV ziwe huru, wapinzani wasingekuwa na ya kuongea sasa hivi. Kinyume chake sasa hivi Magu hana jipya, watu wamewamiss wapinzani
Who cares?
 
Mambo ya muhimu siku zote hutofautiana na upeo wa msikilizaji binafsi. Kwa mtu ambaye tangu azaliwe hajawahi kuwa na maji karibu na nyumba aliyozaliwa siku akipata uhakika wa maji safi kwake hilo ni jambo la muhimu sana.

Muuzaji samaki wa Ukerewe aliyezoea kupoteza ndugu zake ziwani kwa sababu ya mitumbwi siku akianza kupanda meli kwake hilo ni suala muhimu sana.

Vitu vyepesi kwa mtu mmoja lakini kwa mwingine ni vitu muhimu sana.
Mkuu hivi Mv Bukoba ilikuwa meli au mtumbwi? Sorry nimesahau
 
Na akileta vurugu tuna mng'oa kwa nguvu
Nafasi pekee ni October akipona October atoki milele,mwakani kikokotoo cha kumnyonya mtumishi kinaanza tumika,
Pia kuna hati hati ya wafanyakazi kukosa mishahara ashindwi kusema anaetaka kufanya kazi afanye asiyetaka afungashe serikali haina pesa tumetoka kwenye kampeni hadi hali itakapokuwa nzuri.
 
Back
Top Bottom