Pre GE2025 Tundu Lissu amteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu. Ateua Manaibu Katibu Wakuu na Wajumbe wa Kamati Kuu
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Mwenyekiti Mpya wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama ambalo limekutana leo Jumatano, Januari 22, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ameanza kupanga safu yake ya uongozi kwa Kuteua Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu.

Mh. Tundu Lissu amefanya uteuzi kama ifuatavyo

Katibu Mkuu
1. John John Mnyika

Manaibu Katibu Mkuu
1. Aman Golugwa - Naibu Katibu Mkuu Tanganyika (Tanzania Bara)
2. Wakili Ally Ibrahim Juma - Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Wajumbe wa Kamati Kuu
1. Godbless Lema
2. Dkt. Rugemeleza Nshala - Mwanasheria Mkuu wa Chama
3. Rose Mayemba
4. Salma Musa Kasanzu
5. Hafidh Ally Salehe

Pia soma
- Freeman Mbowe akubali kushindwa, awapongeza Lissu na Heche kwa ushindi


View: https://www.youtube.com/live/n57Tc7XtINo
 
Safi sana naona kamati ya roho mbaya inazidi kukamilika.
Naomba Mheshimiwa mwenyekiti GODLESS LEMA awe MKURUGENZI WA ITIKADI NA UENEZI WA CHAMA.
HAPO KAMATI YA ROHO MBAYA KWA MAFISADI ITAKUWA IMEKAMILIKA KUWAPELEKEA MOTO WALE NZI WA KIJANI.
100%
 
Back
Top Bottom