Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu watanzania,
Tundu Lissu anayo mengi sana ya kujifunza kutoka Katika picha hii inayomuonesha Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Hii picha ilichukuliwa na kupigwa hapo jana walipokutana viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa katika mashauriano ya Masuala mbalimbali chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania. Picha hii na namna viongozi wetu hawa wa vyama vyetu wanavyotabasamu na kufurahi inaonyesha siasa siyo uadui.
Lakini pia inaonyesha namna viongozi hawa walivyoelewa vyema na kuzifanyia kazi 4R Za Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ambaye aliziasisi na kuzileta katika lengo la kulileta pamoja Taifa na kujenga umoja wa kitaifa, ndio sababu ya kuona leo watu wakiwa huru kuzungumza yaliyo katika vifua vyao kwa uhuru bila hofu.
Pia soma:
Sasa angekuwa ndio Lissu yupo kwenye nafasi ya Mbowe yaani ya uwenyekiti ungeona namna anavyotoa matamko makali makali na ya hovyo hovyo yenye kujenga chuki,uhasama,uadui na kuchochea ubaguzi kwa misingi tofauti tofauti kwa maslahi yake binafsi.maana yeye ni mtu ambaye anapenda mavurugu vurugu na uhasama wa kisiasa.
Ndio maana hutoa lugha zisizo nzuri akiwa mwenye majukwaa ya siasa.ndio sababu hupenda kuita haya ni Ma CCM na yale ni Ma PoliCCM. Yeye huona ambao hawapo kwenye chama chake au hawakubaliani naye kuwa wote hawana akili na hawajitambui na ni mambumbu tu.
anasahau kuwa katika siasa hakunaga adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu na siasa siyo vita wala uadui.anasahau pia kuwa ili upate ushindi katika ngazi ya aina yoyote ile basi ni lazima ufanye kazi ya kuyashawishi makundi mbalimbali kukuunga mkono na kuwa upande wako badala ya kuyachukia na kuyatukana kwa matusi na lugha za udhalilishaji.
Ndio sababu Lissu anachukiwa na watu wengi sana na watumishi na wafanyakazi wengi sana katika vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na maneno yake ya kuwadhalilisha na kuwashushia heshima. ndio maana hakuna anayeweza kumuunga mkono hata kwa kificho tu, maana kila mtu anaona ni mtu mropokaji, mkurupukaji, Mwenye kujaa mihemuko, jazba, hasira na hivyo kushindwa kutumia Busara na hekima katika kuzungumza na kushawishi watu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

- Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akamatwa uwanja wa Ndege Songwe
- Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa