Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajikoroga

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajikoroga

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
CHADEMA kupitia Mgombea Urais wao ametamka kujenga masoko yatakayofanya kazi nyakati za usiku.

Namnukuu Lissu “Tutajenga majengo makubwa kwa ajili ya Wamachinga ili wafanye biashara kwa uhuru na sio kuwapa vitambulisho halafu wafanyie biashara kwenye mitaro ambako mvua inakuwa yao na jua linakuwa lao” -Tundu Lissu akiwa Mbeya

“Kwenye stendi za Mabasi tutajenga majengo ambayo Mama Lishe watauza vyakula, tunataka kuwa na masoko ambayo yatakuwa yanafanya kazi usiku kucha ili Mtu yeyote ambaye atakuwa amechelewa kufika kwenye mji husika apate huduma”-Lissu

Hoja kuu hapa ni kujenga masoko, watu kufanya biashara nyakati za usiku na vitambulisho vya wajasiliamali.

Lissu huyu anayesema kila siku maendeleo ni Watu na sio vitu, leo hii huyo huyo Lissu anasema atajenga masoko. Iko wapi hoja yake aliyosema maendeleo ya Watu na sio vitu? Ama soko ni Watu na sio kitu tena?

Huyo huyo Lissu na wenzake wanaosema wakiingia ikulu watauza ndege zote za nchi zilizonunuliwa na Rais Magufuli ndio hao hao wanatumia usafiri wa ndege kuzunguka mikoani. Au wanazopanda sio ndege ni mitumbwi?

Lissu huyu huyu anayepinga ujenzi wa umeme wa Mto Rufiji utakaozalisha megawatts 2115 kuwa unalifilisi Taifa, leo hii anasema atahakikisha Wajasiliamali wanafanya biashara hadi usiku. Anapinga ujenzi wa umeme wa uhakika anataka hao Wajasiliamali wafanye biashara gizani?

Alivyokuwa mkurupukaji Lissu anazungumzia vitambulisho vya Wajasiliamali kuwa havina tija kwa Wamachinga na Wajasiliamali. Lahaula!

Inawezekana "dish" limeyumba hajui kuwa hajui vitambulisho hivyo ni mkombozi kwa Wamachinga na Wajasiliamali wote wadogo. Mmachinga, Mama Lishe hapo awali walikuwa kwenye misukosuko mikubwa na Mgambo kutokana na suala la ulipaji ushuru waliokuwa wakitozwa kila siku ambapo walikuwa wakilipia ushuru wa Tsh. 500/- ama Tsh. 1,000/- kwa siku.

Leo hii badala ya kulipa Tsh. 180,000/- ama Tsh. 365,000/- kwa mwaka leo hii wanalipa Tsh. Elfu ishirini tu (20,000/-). Wanaokoa Tsh. 160,000/- na wengine wanaokoa Tsh. 345,000/- pamoja na bidhaa zao. Lissu atasemaje vitambulisho havina tija?

Inawezekana Lissu anapajua zaidi Ubelgiji kuliko Tanzania, nimkumbushe Tanzania kuna masoko kwa ajili ya Wamachinga yapo mfano hai ni soko la Machinga Complex lililopo Karume wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.

Si hayo tu bali pia Rais Magufuli amejenga stendi mpya nyingi tu ikiwemo ya Mpanda Katavi, Morogoro, Dodoma nk na kote huko kuna majengo ya Wajasiliamali wote wakiwemo Mama Lishe.

Lissu aache kujikoroga, aelewe hizi sio zama za drama, siasa za uongo kwani Watanzania wa sasa ni waelewa sana wanajua mbivu na mbichi, hawalishwi matango pori!!

*Shilatu E.J*
 
Mkuu Lissu anatumiwa na chama chake kwa nia ya kuongeza majimbo ili ruzuku iwe nene miaka mitano ijayo.

Mwenye kumtumia siku akifanikiwa kukipata akitakacho kutazuka mtafaruku mkubwa. Ni siasa zile zile za malengo yaliyojificha.
 
yuko sahihi kabisa tukishuka stendi saa nane usiku toka shift tutakula na kuchukua mahitaji ya kwenda nayo nyumbani. machinga wataingiza hela mchana na usiku kwenye hizo malls watasaidia ndugu zao vijijini.

hayo ndio maendeleo ya watu, serikali itatoa tenda kwa kampuni binafsi za kitanzania na kuwalipa cash, pesa itazunguka mtaani.
 
Kuna mambo inahitaji akili kubwa kuliko hizo ulizonazo ili uweze kuyaelewa.
 
Alisema Mwaka 1967 wakati wa azimio la Arusha serikali ilitaifisha mali za watu binafsi na taasisi binafsi,

kwa hiyo wakati wote kabla ya Uhuru na miaka michache baada ya Uhuru, watu binafsi na taasisi binafsi walimiliki uchumi na vitega ucgumi, Kama banks majengo viwanda, mashule, hosipitali, nakadhalika

akasema ukiwaacha watu wawe huru, kiuchumi, wataweza kujenga hizo infrastructure, Kama watu binafsi au Kama taasisi

kujenga masomo ya usiku au maduka rejereja si lazima yajengwe na fedha za serikali za Kodi, ipo mifuko mbalimbali ina weza zikopesha halmashauri, yapo mabank yanaweza kopesha halmashauri kujenga hiyo miradi bila kutegemea ufadhiri wa serikali

pia Kuna sheria ya bunge inayoelekeza PPP,
ushiriki wa secta binafsi kwa ubia na na serikali katika uwekezaji
 
Kila miaka 5 wanasiasa huja kutafuta kura kwa wananchi,ili wapate mlo wao.

Lakini hawaji pekee yao wanakuja na wapambe.Unakuta wapambe na washabiki wa kambi tofauti wanajaribu hata kusahihisha au kubadirisha maneno ya wagombea wao ili iwe je?Mshaambiwa uraisi hauna ubia.

Sisi tungetakiwa tuwaulize wagombea uraisi maswali ya papo kwa papo.Ajabu tunaanza kuwashangilia bila hata kutambua wao ndio wanaomba kazi nasi ni waajiri wao.

Tuache kujitoa ufahamu kuna maisha baada ya uchaguzi.
 
Tunamwitaji Lissu saa hii CCM imeshindwa na magu hafai.
 
Ni asilimia ngapi ya watanzania wanaaccess na masoko kulinganisha na asilimia ya watanzania wenye access na usafiri wa ndege
Unategemea hawa kina "WANATAFUNWA" wakujibu swali kama hili?
 
Unajikoroga tu mwenyewe kwa kukosa focus ya critical analysis yako. Kwani faida ya vitabulisho vile ni nini ikiwa wafanyabiashara tunawaona wakifanya biashara kwenye mitaro ya maji machafu? Kwa nini wasipewe TIN namba na kisha kuwekwa mahali penye hadhi kidogo kwa biashara zao?
 
Lisu hawezi kuwa Rais tz.

Huku ni kupoteza muda kujadili hoja za mtu ambaye hata serikali za mitaa hana.
 
Unahitaji kuwa na akili za kutosha ili kumuelewa Tundu Lissu. Lakini ukiwa na akili za kuvukia barabara utabaki mtupu kama mtoa mada.
hata kichaa hawez kumuelewa tundu lisu yan mkuu unakaa kabisa kusema unaitaj mda kumuelewa lissu africa tunataka kujitegemea yeye anakuja na sera za kushirikiana na ulaya a man who need to win the election unakuja na sera hiyo ya kipumbavu hivo sisi sio wapumbavu kiasi cha kutueleza ujinga huu
 
Chadema kupitia Mgombea Urais wao ametamka kujenga masoko yatakayofanya kazi nyakati za usiku.

Namnukuu Lissu “Tutajenga majengo makubwa kwa ajili ya Wamachinga ili wafanye biashara kwa uhuru na sio kuwapa vitambulisho halafu wafanyie biashara kwenye mitaro ambako mvua inakuwa yao na jua linakuwa lao” -Tundu Lissu akiwa Mbeya

“Kwenye stendi za Mabasi tutajenga majengo ambayo Mama Lishe watauza vyakula, tunataka kuwa na masoko ambayo yatakuwa yanafanya kazi usiku kucha ili Mtu yeyote ambaye atakuwa amechelewa kufika kwenye mji husika apate huduma”-Lissu

Hoja kuu hapa ni kujenga masoko, Watu kufanya biashara nyakati za usiku na vitambulisho vya Wajasiliamali.

Lissu huyu anayesema kila siku maendeleo ni Watu na sio vitu, leo hii huyo huyo Lissu anasema atajenga masoko. Iko wapi hoja yake aliyosema maendeleo ya Watu na sio vitu? Ama soko ni Watu na sio kitu tena?

Huyo huyo Lissu na wenzake wanaosema wakiingia ikulu watauza ndege zote za nchi zilizonunuliwa na Rais Magufuli ndio hao hao wanatumia usafiri wa ndege kuzunguka mikoani. Au wanazopanda sio ndege ni mitumbwi?

Lissu huyu huyu anayepinga ujenzi wa umeme wa Mto Rufiji utakaozalisha megawatts 2115 kuwa unalifilisi Taifa, leo hii anasema atahakikisha Wajasiliamali wanafanya biashara hadi usiku. Anapinga ujenzi wa umeme wa uhakika anataka hao Wajasiliamali wafanye biashara gizani?

Alivyokuwa mkurupukaji Lissu anazungumzia vitambulisho vya Wajasiliamali kuwa havina tija kwa Wamachinga na Wajasiliamali. Lahaula!

Inawezekana "dish" limeyumba hajui kuwa hajui vitambulisho hivyo ni mkombozi kwa Wamachinga na Wajasiliamali wote wadogo. Mmachinga, Mama Lishe hapo awali walikuwa kwenye misukosuko mikubwa na Mgambo kutokana na suala la ulipaji ushuru waliokuwa wakitozwa kila siku ambapo walikuwa wakilipia ushuru wa Tsh. 500/- ama Tsh. 1,000/- kwa siku.

Leo hii badala ya kulipa Tsh. 180,000/- ama Tsh. 365,000/- kwa mwaka leo hii wanalipa Tsh. Elfu ishirini tu (20,000/-). Wanaokoa Tsh. 160,000/- na wengine wanaokoa Tsh. 345,000/- pamoja na bidhaa zao. Lissu atasemaje vitambulisho havina tija?

Inawezekana Lissu anapajua zaidi Ubelgiji kuliko Tanzania, nimkumbushe Tanzania kuna masoko kwa ajili ya Wamachinga yapo mfano hai ni soko la Machinga Complex lililopo Karume wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.

Si hayo tu bali pia Rais Magufuli amejenga stendi mpya nyingi tu ikiwemo ya Mpanda Katavi, Morogoro, Dodoma nk na kote huko kuna majengo ya Wajasiliamali wote wakiwemo Mama Lishe.

Lissu aache kujikoroga, aelewe hizi sio zama za drama, siasa za uongo kwani Watanzania wa sasa ni waelewa sana wanajua mbivu na mbichi, hawalishwi matango pori!!

*Shilatu E.J*
.
IMG_20200906_180535_748.jpg
 
Back
Top Bottom