CHADEMA kupitia Mgombea Urais wao ametamka kujenga masoko yatakayofanya kazi nyakati za usiku.
Namnukuu Lissu “Tutajenga majengo makubwa kwa ajili ya Wamachinga ili wafanye biashara kwa uhuru na sio kuwapa vitambulisho halafu wafanyie biashara kwenye mitaro ambako mvua inakuwa yao na jua linakuwa lao” -Tundu Lissu akiwa Mbeya
“Kwenye stendi za Mabasi tutajenga majengo ambayo Mama Lishe watauza vyakula, tunataka kuwa na masoko ambayo yatakuwa yanafanya kazi usiku kucha ili Mtu yeyote ambaye atakuwa amechelewa kufika kwenye mji husika apate huduma”-Lissu
Hoja kuu hapa ni kujenga masoko, watu kufanya biashara nyakati za usiku na vitambulisho vya wajasiliamali.
Lissu huyu anayesema kila siku maendeleo ni Watu na sio vitu, leo hii huyo huyo Lissu anasema atajenga masoko. Iko wapi hoja yake aliyosema maendeleo ya Watu na sio vitu? Ama soko ni Watu na sio kitu tena?
Huyo huyo Lissu na wenzake wanaosema wakiingia ikulu watauza ndege zote za nchi zilizonunuliwa na Rais Magufuli ndio hao hao wanatumia usafiri wa ndege kuzunguka mikoani. Au wanazopanda sio ndege ni mitumbwi?
Lissu huyu huyu anayepinga ujenzi wa umeme wa Mto Rufiji utakaozalisha megawatts 2115 kuwa unalifilisi Taifa, leo hii anasema atahakikisha Wajasiliamali wanafanya biashara hadi usiku. Anapinga ujenzi wa umeme wa uhakika anataka hao Wajasiliamali wafanye biashara gizani?
Alivyokuwa mkurupukaji Lissu anazungumzia vitambulisho vya Wajasiliamali kuwa havina tija kwa Wamachinga na Wajasiliamali. Lahaula!
Inawezekana "dish" limeyumba hajui kuwa hajui vitambulisho hivyo ni mkombozi kwa Wamachinga na Wajasiliamali wote wadogo. Mmachinga, Mama Lishe hapo awali walikuwa kwenye misukosuko mikubwa na Mgambo kutokana na suala la ulipaji ushuru waliokuwa wakitozwa kila siku ambapo walikuwa wakilipia ushuru wa Tsh. 500/- ama Tsh. 1,000/- kwa siku.
Leo hii badala ya kulipa Tsh. 180,000/- ama Tsh. 365,000/- kwa mwaka leo hii wanalipa Tsh. Elfu ishirini tu (20,000/-). Wanaokoa Tsh. 160,000/- na wengine wanaokoa Tsh. 345,000/- pamoja na bidhaa zao. Lissu atasemaje vitambulisho havina tija?
Inawezekana Lissu anapajua zaidi Ubelgiji kuliko Tanzania, nimkumbushe Tanzania kuna masoko kwa ajili ya Wamachinga yapo mfano hai ni soko la Machinga Complex lililopo Karume wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.
Si hayo tu bali pia Rais Magufuli amejenga stendi mpya nyingi tu ikiwemo ya Mpanda Katavi, Morogoro, Dodoma nk na kote huko kuna majengo ya Wajasiliamali wote wakiwemo Mama Lishe.
Lissu aache kujikoroga, aelewe hizi sio zama za drama, siasa za uongo kwani Watanzania wa sasa ni waelewa sana wanajua mbivu na mbichi, hawalishwi matango pori!!
*Shilatu E.J*