Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,513
Picha kwa hisani ya: Mwananchi: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/matukio-kumi-ya-uasi-wa-mwalimu-nyerere-3805830
Tutake tusitake, sasa ni wazi kwamba, kupitia ajenda ya "No Reform No Election" Tundu Lissu anatekeleza kwa Vitendo Falsafa ya "Uasi" iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.
Uchambuzi wa Kitabu kipya cha "Development as Rebellion: A biography of Julius Nyerere" unabainisha matukio zaidi ya kumi ya ‘uasi' huo katika historia ya maisha ya Mwalimu Julius Nyerere, muasisi wa Taifa la Tanganyika.
Uchambuzi huo ulifanyika hivi karibuni jijini Dar es Dalaam wakati wa Kongamano la kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere katika mtazamo wa kiuchumi chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), kama picha hapo juu inavyoonyesha.
Tafsiri ya “uasi” katika kitabu hicho imejikita katika upinzani alioufanya Mwalimu Nyerere dhidi ya mifumo mbalimbali kutokana na imani yake katika usawa, haki na maendeleo.
Baadhi ya matukio ya uasi ulioandikwa katika kitabu hicho ni pamoja na:
- Uasi dhidi ya mfumo wa kikoloni kwa kujiuzulu mara tatu ikiwamo nafasi ya uwaziri mkuu,
- Uasi dhisi ya lugha ya kigeni na kuamini Lugha ya Kiswahili,
- Uasi dhidi ya mfumo wa kibepari kwa kuzindua wazo la Azimio la Arusha
- Uasi dhidi ya mfumo wa Elimu huku akiamini elimu ya kujitegemea,
- Uasi dhidi ya viongozi waliokuwa wanakandamiza wanafunzi,
- Uasi dhidi ya mifumo dume iliyokandamiza mwanamke,
- Uasi dhidi ya mavazi ya suti za kikoloni na kutumia kaunda suti,
- Uasi dhidi ya utumwa,
- Uasi dhidi ya ukoloni,
- Uasi dhidi ya ujinga, umaskini na maradhi kwa kuanzisha huduma za kijamii kwa wote.
Profesa Saida Othman, mwandishi wa juzuu mojawapo ya kitabu hicho anasema kuwa mbali na Mwalimu Nyerere, "hata leo pia tunao waasi wastaafu na waasi watarajiwa, Mwalimu alikuwa na misimamo tofauti katika familia yake, shuleni, kanisani na serikali ya kikoloni, akitaka usawa, haki na maendeleo ya watu.”
Kwa ujumla, katika mtazamo wa Nyerere, dhana ya "maendeleo kama aina ya uasi" ("development as rebellion") inasisitiza kwamba maendeleo ya kweli yanahitaji juhudi za makusudi za kupambana na mifumo ya kitumwa inayofanya kazi kama vizingiti vya uhuru (freedom constraints).
Mapambano hayo ni kwa ajili ya kuibomoa mifumo ya kitumwa na kujenga mifumo mipya inayostawisha uhuru mpana, usawa mkubwa zzaidi na haki thabiti, badala ya kubweteka na kuikumbatia mifumo iliyo kama minyororo miguuni mwetu.
Hivyo, kwa mtazamo wa Nyerere, "utumwa" au ni kinyume cha "uhuru" ni dhana yenye sehemu tatu:
Mosi, kuna "mtendaji" anayepaswa kunufaika na uhuru unaoongelewa; pili, kuna "malengo" aliyo nayo mtendaji huyo; na tatu, kuna "vizingiti" vinavyomzuia mtendaji kutimiza dhamira yake.
Vizingiti vinaweza kuwa ndani ya mtu kama vile ujinga au ugonjwa; au vinaweza kuwa nje ya mwili wa mtu, kama vile katiba mbaya, sheria mbovu, kanuni kandamizi, miiba, minyororo, milima, mabonde, makorongo, ukosefu wa vitendea kazi. Maendeleo ni mchakato wa kuondoa vizingiti hivi.
Ni kwa sababu hizi, Sheria ya Makosa ya Jinai, toleo la kwanza mpaka toleo la sasa, yanai Tanzania Penal Code, RE 2019, inatofautisha kati ya "uasi halali" na "uasi haramu" katika ibara ya 55.
Kwa mfano, katika Sheria hii, "uasi haramu," yaani "uchochezi haramu," unatajwa kwenye aya ya 51(1)(b), kama ifuatavyo:
"55(1) (b) Nia ya kufanya uchochezi (haramu) ni nia ya: ... kuwatia hamasa wakazi wowote wa Jamhuri ya Muungano ili kuleta mageuzi, kwa njia nyingine isiyo ya halali kuhusu jambo lolote katika Jamhuri ya Muungano lililowekwa na sheria; au
Katika aya ya 51(3) Sheria hii inafafanua "uchochezi haramu" kwa kusema kwamba,51(3) Katika kuamua endapo nia ya kitendo chochote kilichofanywa au inayohusishwa na kitendo ilikuwa ya, maneno yoyote yatakayozungumzwa au nyaraka yoyote itakayo andikwa itahesabiwa kuwa ni ya uchochezi (haramu), na mtu yeyote atahesabiwa kuwa alinuia matokeo ambayo kwa hali ya kawaida yanatokana na kitendo chake kwa wakati na katika hali ya kimazingira aliyoitenda mwenyewe."
Na kwa mfano tena, katika sheria hii "uasi halali," yaani "uchochezi halali," unatajwa kwenye aya ya 51(2)(b), kama ifuatavyo:51(2)(b) Kitendo, hotuba au tangazo halitahesabiwa kuwa ni la uchochezi haramu kwa sababu tu linalenga katika: ... kuonyesha makosa au mapungufu katika serikali au Katiba ya Jamhuri ya Muungano au kama ilivyowekwa na sheria, au katika usimamiaji utoaji wa haki kwa lengo kurekebisha makosa hayo au upungufu huo; au
Kwa ufupi, kifungu cha 51 kinasema kuwa kuhimiza watu kutumia mbinu halali kisheria kuzuia uchagui ili, kwa njia hiyo, usogezwe mbele na kutoa mwanya wa kufanyika kwa mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi, ni "uchochezi halali."
Mbinu halali kisheria ni pamoja na mikutano ya hadhara, maandamano, midahalo, kuandika na kusambaza petisheni, na kususia hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.