Pre GE2025 Tundu Lissu: Anayechukizwa mimi kuwa Mwenyekiti aelimishwe

Pre GE2025 Tundu Lissu: Anayechukizwa mimi kuwa Mwenyekiti aelimishwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni maneno sahihi Sana, mwanachama yeyote atakayempinga lissu kutumia haki yake ya kuomba kuchaguliwa aelimishwe maana ya demokrasia na misingi yake
 
You're really under estimating the capacity of Tundu Lissu to turn tables. Utaiona nguvu yake kampeni zikianza Mbowe mwenyewe atatangaza kujitoa. Maana hata akishinda kihalali majority wataamini kamuibia Lissu ma hivyo kupasua chama na hakitoweza recover mapema.
Sasa hapo nani atakuwa kashindwa Mbowe au CDM kama chama.
 
Tundu Lissu nadhani ndio aelimishwe huu ukweli mchungu sana, na kila siku tunasema Chadema ni SACCOS YA MBOWE, iko hivi CHADEMA ni Mali binafsi ya Familia ya Mzee Mtei na Mbowe kaoa kwa Mzee Mtei, yaani Mbowe ni mkwe wa Mzee Mtei,, hivyo CHADEMA ni Mali binafsi ya Mbowe family, so kuachia urithi kwa njia ya Demokrasia hilo halipo, kwani Chadema hakuna demokrasia, ni uhuni tu kama kucheza kamari.

Mbowe kila mwana Chadema akitaka kugombea Uenyekiti anamwita msaliti, tena anatumia hadi maneno ya kuwa sumu haionywi, kuanzia Zitto, Mzee Sumaye, etc wote waliondoka CDM sbb hakuna Chama ni Mali binafsi au Saccos ya Mbowe & Family, niwaambie tu, kwa asilimia 100% Tundu Lissu anaondoka CHADEMA na soon atatangaza, kama wewe ni mwana siasa makini huwezi kuwa mwana CHADEMA, ni genge la wahuni tu, Chadema sio Chama cha siasa, ni Saccos ya Mbowe, hivi hamuelewi hadi lini nyie watu?

CCM ndio CHAMA PEKEE cha Siasa nchini Tanzania.
 
"Wanachama wa Chadema, wanapaswa kufanya Tathmini ya uongozi wa Tundu Lissu kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwabla ya kumpa Tena nafasi ya uwenyekiti wa chamdema Taifa.Na tathimini hiyo inapaswa kuzingatia vipengele vifuatavyo:

1. Mchango katika Sera na Mikakati
- Je, Lissu ameweza kuandaa au kuboresha sera zinazowezesha chama?
- Ni mikakati gani aliyoanzisha ili kuimarisha ushawishi wa chama ndani na nje ya bunge?

2. Uhamasishaji na Ujumuishaji
- Ameweza vipi kuhamasisha wanachama na jamii kwa ujumla kuhusu malengo ya chama?
- Je, alifanya kazi gani katika kuunganisha makundi mbalimbali ndani ya chama na jamii?

3. Uongozi wa Kijamii
- Lissu ameshiriki vipi katika masuala ya kijamii na haki za binadamu?
- Je, alifanya kampeni yoyote ya kuhamasisha haki za binadamu na demokrasia?

4. Ushirikiano na Vyama Vingine
- Ameweza kuanzisha ushirikiano gani na vyama vingine vya siasa au mashirika yasiyo ya kiserikali?
- Je, alifanya jitihada za kuimarisha umoja wa wapinzani?

5. Uwezo wa Kukabiliana na Changamoto
- Alikabili vipi changamoto za kisiasa, ikiwa ni pamoja na vitisho na dhuluma kutoka kwa serikali?
- Je, alionesha ujasiri na uthabiti katika nyakati ngumu?

6. Mawasiliano na Uwazi
- Je, Lissu alifanya mawasiliano gani na wanachama wa chama na umma?
- Ni kiasi gani alijenga uwazi katika uongozi wake?

7. Matokeo ya Kazi Zake
- Je, kuna mafanikio yoyote makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wake?
- Matokeo ya kazi zake yanaweza kuonyeshwa vipi katika uchaguzi au katika kuimarisha chama?

8. Maadili na Msimamo
- Je, Lissu ameweza kuonyesha maadili ya juu katika uongozi wake?
- Alisimama vipi katika masuala ya msingi yanayohusiana na maadili ya chama?

9. Uwezo wa Kuongoza Timu
- Alijenga vipi timu yenye nguvu na ushirikiano ndani ya chama?
- Ni vipi alihamasisha viongozi wengine wa chama kufanya kazi kwa pamoja?

10. Ufanisi katika Mawasiliano ya Kisiasa
- Je, Lissu alitumia vizuri vyombo vya habari na majukwaa mengine kufikisha ujumbe wa chama?
- Alifanya vipi kampeni za kisiasa na kuhamasisha wananchi?

Kwa kuzingatia vipengele hivi, tathmini ya uongozi wa Tundu Lissu kama Makamu Mwenyekiti inaweza kuwa na uwazi zaidi na kusaidia kuelewa uwezo wake wa kuongoza katika nafasi ya Uwenyekiti wa Chadema Taifa
 
Tundu Lissu nadhani ndio aelimishwe huu ukweli mchungu sana, na kila siku tunasema Chadema ni SACCOS YA MBOWE, iko hivi CHADEMA ni Mali binafsi ya Familia ya Mzee Mtei na Mbowe kaoa kwa Mzee Mtei, yaani Mbowe ni mkwe wa Mzee Mtei,, hivyo CHADEMA ni Mali binafsi ya Mbowe family, so kuachia urithi kwa njia ya Demokrasia hilo halipo, kwani Chadema hakuna demokrasia, ni uhuni tu kama kucheza kamari.

Mbowe kila mwana Chadema akitaka kugombea Uenyekiti anamwita msaliti, tena anatumia hadi maneno ya kuwa sumu haionywi, kuanzia Zitto, Mzee Sumaye, etc wote waliondoka CDM sbb hakuna Chama ni Mali binafsi au Saccos ya Mbowe & Family, niwaambie tu, kwa asilimia 100% Tundu Lissu anaondoka CHADEMA na soon atatangaza, kama wewe ni mwana siasa makini huwezi kuwa mwana CHADEMA, ni genge la wahuni tu, Chadema sio Chama cha siasa, ni Saccos ya Mbowe, hivi hamuelewi hadi lini nyie watu?

CCM ndio CHAMA PEKEE cha Siasa nchini Tanzania.
Mcherengwa naye kaoa kwa Saa100.
Marwa naye kaoa kwa JK
 
Lissu ni sawa ‘Santino (Sonny) Carleone’, mtoto wa kwanza wa Don Carleone; kwenye ‘The Godfather’ movie.

Sonny alikuwa anaandaliwa kuwa head of the family, shida yake ilikuwa mihemko apigi hesabu za revenge zake familia inapopata changamoto.

Hiyo character yake ya mihemko ndio maadui wakaitumia kumuwekewa mtego rahisi wakielewa atakurupuka na atanasa tu na kumuua.

Same Lissu has become too ambitious, lakini hana leadership qualities bado, ni hasira zake tu za Magufuli, kuwachukia wote waliochukua offer ya viti maalum na desperation yake ya kutaka kuona social disobedience kwenye kuitoa CCM.

Huo uchaguzi wa ndani hawezi shinda na 2025 hatopewa nafasi ya kugombea uraisi. Hana busara ya kuwa kiongozi wa chama wala taifa. Ni mtu wa kusukumwa na hisia kuliko calculated moves.

Mbowe anampeleka Lissu kuwa diaspora wa kudumu au baada ya hapo atakuwa mwanaharakati tu.
Nimewahi kusema kitu kama hiki alipopewa jukumu la kugombea uraisi. Lisu ni mtu mzuri lakini hafiti kuwa kiongozi wa juu kabisa
 
Mbowe naye kukaa kwenye nafasi hiyo inatosha,kura iamue nani anafaa kuwa mwenyekiti demokrasia ifanye kazi,Mbowe miaka yote hii hamna kipya labda Lissu atakuja na political ideology mpya
 
Mbowe naye kukaa kwenye nafasi hiyo inatosha,kura iamue nani anafaa kuwa mwenyekiti demokrasia ifanye kazi,Mbowe miaka yote hii hamna kipya labda Lissu atakuja na political ideology mpya
Ni sawa,ila awe na uwezo wa kuishi Segerea!
Na sio kukimbilia Ubelijiji,na kuacha wanachama mitaani.
 
Kila la heri Tundu Lisu, mpambanaji wa siku zote.

CHADEMA ni chama cha wote, ni chama.cha kidemokrasia. Na wengine wenye nia za kugombea nafasi za ngazi za juu wapo huru.

CHADEMA wafundisheni CCM maana ya demokrasia.
 
Mcherengwa naye kaoa kwa Saa100.
Marwa naye kaoa kwa JK

Uwe na akili, stop being short sighted, Issue sio kuwa umeoa wapi, issue owner wa CHAMA ni nani? JK au Mama Samia sio owners wa CCM, Chama cha Mapinduzi ni Chama cha Watanzania wote..!! CCM sio Mali binafsi ya mtu yeyote yule, na CCM haijawa kuwa mali ya mtu binafsi tokea kianzishwe.

CHADEMA ni MALI YA MTEI, sasa Mbowe kapewa kama mkwe kuendesha CHAMA ambacho ni Mali binafsi, ukweli uko hivyo, sijui unaelewa wewe? Usikute naongea na mtu kumbe huna hata D in your subjects, acha ujinga.
 
Machawa ya Mbowe yamechukizwa sana Lisu kuwa mwenyekiti
 
Nimewahi kusema kitu kama hiki alipopewa jukumu la kugombea uraisi. Lisu ni mtu mzuri lakini hafiti kuwa kiongozi wa juu kabisa
Sifa ya uongozi ni kujenga sio kubomoa.

Kuwa diplomatic hiyo ni skill muhimu zaidi kwenye siasa kuliko popote.

Siasa ni tasnia ya maslahi ‘hakuna permanent enemy, kuna permanent interest’.

Lussu ana demand permanent loyalty, yeyote ambae yupo kinyume nae ni adui wake wa siasa. Ni dictator wa fikra.

Leadership inataka compromise
and negotiations in decision making. Kiongozi unatakiwa kuelewa unachotaka wewe sio kila anachotaka kila mtu (you have to settle) for what’s best for everyone.

Lissu ni mchanga akili zake ni ‘me, me, me’.

Ndio Mbowe anahitaji successor kwa mtazamo wangu. Chama amekifanya mali yake kwa urefu fulani Iła sio Lissu.

Lissu uelewa wake wa siasa ni mdogo ni mtu wa kukurupuka; anaendeshwa na hisia kuliko uelewa wa siasa.
 
Back
Top Bottom