GE2025 Tundu Lissu apeta tena, pingamizi lingine lakubaliwa, Mahakama yaikataa ripoti ya video ya uhaini

GE2025 Tundu Lissu apeta tena, pingamizi lingine lakubaliwa, Mahakama yaikataa ripoti ya video ya uhaini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kutoka kwenye chumba namba moja (1) cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu inaendelea tena leo, Alhamisi Oktoba 23.2025, chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru

Mapema kabisa, Mahakama imeanza kutoa 'uamuzi mdogo' kufuatia pingamizi lililokuwa limewekwa na mshtakiwa Tundu Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, ambapo pingamizi hilo limelenga kupinga kuwasilishwa Mahakamani kama kielelezo taarifa ya uchunguzi ya picha jongefu (video), kutoka kwa shahidi wa tatu (3) wa Jamhuri Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Samwel Elibariki Kaaya

Katika kujenga hoja ya pingamizi hilo, sambamba na kufanya marejeo ya hoja mbalimbali za kisheria na kesi mbalimbali, Lissu aliieleza Mahakama kuwa shahidi huyo ana uwezo wa kutoa 'certificate' na sio 'report', na kwamba shahidi alipaswa kuandaa picha mnato (still picture) alizopelekewa kufanyiwa uchunguzi na kuzikuza, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) na au Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa mujibu wa tangazo la serikali

Wakili wa Serikali Mkuu Job Mrema alipinga vikali hoja hiyo, akieleza Mahakama kuwa Mahakama hiyo haibanwi na maamuzi yake iliyotoa mapema jana, Oktoba 22.2025 ya kukataa kupokelewa Mahakamani hapo kwa 'Memory Card' na 'Flash Disk' kama kielelezo kutoka kwa shahidi huyo

Mrema alienda mbali zaidi na kuieleza Mahakama kuwa, mshtakiwa ameingilia 'content' ya hizo 'report' kwa kuzisoma jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Mahakama Kuu, yanayoelekeza kwamba nyaraka yoyote haitakiwi kusomwa kabla haijawasilishwa na kupokelewa Mahakamani, hivyo kuiomba Mahakama kutupilia mbali pingamizi hilo

Akijibu hoja za kutetea pingamizi lake alilokuwa ameliweka hapo jana, Lissu alisisitiza kuwa Mahakama hiyo imekataa kupokea 'Memoy Card' na 'Flash Disk' kama kielelezo, hivyo kwenye mazingira ya kisheria taarifa hiyo ya uchunguzi haiwezi kusimama yenyewe

Akitoa uamuzi huo, Jaji Ndunguru amesema Mahakama imekubaliana na hoja za mshtakiwa hivyo kielelezo hicho kimekataliwa...
1761206384604.png
 
Usiwaamini sana hawa watu .... Wanauma na Kupulizia. Wote wanacheza the same script. Wanavuta tu siku mpaka Maza aapishwe na aitishe MUAFAKA wake kama anavyodai.
analeta utani baada ya Mama kuapishwa Lissu anatoka wanatengeza mazingira mapema sana Lissu muafaka wa kitaifa atakubali hapo ndo kuna kimbembe
 
Hii kesi ya Lissu inaendelea kudhihirisha ya kwamba kuna watu wengi serikalini wamepewa vyeo vikubwa huku wakiwa hawana uwezo.

How come mawakili wa serikali wanaoliow mishahara kutokana na kodi zetu, hawajui taratibu za kuwasilisha mahakamani vielelezo vilivyo chukuliwa kwa njia ya video! Hivi ndiyo maana kesi nyingi wanazofunguliwa nje ya nchi huwa wanashindwa.
 
Hivi kuna mtu yeyote alikua anaamini kua Tundu lisu atanyongwa? Watesi wake Wapo ndani ya lengo maana lengo lao lilikua wamshikilie wamuachie yeye na makamo wake baada ya uchaguzi na ndio hicho kinaenda kutimia

Ili ionekane mahakama imetenda haki imemuachia huru... Hii nchi nzito sana
 
Wanavuta tu siku mpaka Maza aapishwe na aitishe MUAFAKA wake kama anavyodai.
Sasa huo utakuwa ni "Mwafaka" kweli, au ujinga ujinga tu.
Mtu afanye madhambi waziwazi ili abakie madarakani kwa nguvu; na wakati huo huo akiahidi kufanya mwafaka juu ya mambo ambayo aliyatumia kumbakisha madarakani?
Unamfanyia mtu ubaya na kumuumiza; wakati huo huo ukimwahidi kumpa pole kwa mabaya yote aliyo kutendea huko mbele ya safari?
Ulaghai wa huyu mwanamke hauna mipaka.
 
Hii kesi ya Lissu inaendelea kudhihirisha ya kwamba kuna watu wengi serikalini wamepewa vyeo vikubwa huku wakiwa hawana uwezo.

How come mawakili wa serikali wanaoliow mishahara kutokana na kodi zetu, hawajui taratibu za kuwasilisha mahakamani vielelezo vilivyo chukuliwa kwa njia ya video! Hivi ndiyo maana kesi nyingi wanazofunguliwa nje ya nchi huwa wanashindwa.
It's more complicated than that!
Kuna mambo mengi hapo yanaingiliana
Wewe watazame watu kama akina Nassoro Katuga na huyo AG Hamza Johari na wengi wengine; wao wanakuja na malengo yao zaidi ya hayo unayozungumzia hapa.

Nenda jeshi la polisi, utawakuta akina Jumanne Mulilro na wenzake wanaopigana kufa na kupona kwa sababu zao tofauti na hao akina Camillius Marwa na wenzake.

Tupo hivyo sasa hivi; kutoyaona hayo ni kujisahaulisha tu kwa maksudi.
 
mind kuwa kuna maandamano yananukia na Lissu ahusiki nao, sasa huo muafaka utahusisha pia waandamanaji?
Ni wapi ulipowahi kuona mwafaka unafanyika kati ya Jambazi na aliyefanyiwa ujambazi? Ulaghai wa Samia Suluhu Hassan umeanza leo?
Huyu ni mtu ambaye maisha yake yote katumia njia za kilaghai, hadi hapo alipofikia.
 
Back
Top Bottom