PreGE2025 Tundu Lissu asafirishwa kupelekwa Dar baada ya kukamatwa Mbinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu anayeshikiliwa na polisi mkoani Ruvuma yupo njiani kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

Screenshot 2025-04-10 113755.png
Lissu anayedaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma jana Jumatano Aprili 9, 2025 muda mchache baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbinga mkoani Ruvuma.

Wakati Lissu akidaiwa kuendelea kushikiliwa na polisi, huku wenzake watatu wakiwemo walinzi wake na kada mmoja wa chama hicho, Shija Shebeshi wameachiwa huru.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Aprili 10, 2025 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia amesema safari ya Lissu kusafirishwa kupelekwa jijini Dar es Salaam ilianza jana jioni baada ya kukamatwa na kupelekwa kituoni.

Hata hivyo, hadi sasa bado haijafahamika chanzo cha Lissu kushikiliwa na Polisi, ingawa jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya aliliambia Mwananchi yupo katika ufuatiliaji kuthibitisha kuwepo kwa taarifa hizo.

Jitihada za Mwananchi kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya au Msemaji wa Polisi zinaendelea.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii kazi ya kunyanyasa/kuwatesa/ kuwapiga/kuwaua wapinzani policcm huwa wanaipenda zaidi kuliko hata ile kazi yao ya msingi ya kulinda raia na mali zao.
Wao yawezekana wanapewa amri,tambua IGP,yaani mkuu wa askari polisi NCHI NZUMA ya TANZANIA,anateuliwa na RAIS ambaye ni MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI,na hao wapinzani wanaonyesha mwelekeo wa kuharibu UCHAGUZI ambao huwa SIYO HURU,ambapo MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI anateuliwa na MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI,ambaye pia ni RAIS wa nchi,unategemea nini?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu anayeshikiliwa na polisi mkoani Ruvuma yupo njiani kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

Lissu anayedaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma jana Jumatano Aprili 9, 2025 muda mchache baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbinga mkoani Ruvuma.

Wakati Lissu akidaiwa kuendelea kushikiliwa na polisi, huku wenzake watatu wakiwemo walinzi wake na kada mmoja wa chama hicho, Shija Shebeshi wameachiwa huru.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Aprili 10, 2025 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia amesema safari ya Lissu kusafirishwa kupelekwa jijini Dar es Salaam ilianza jana jioni baada ya kukamatwa na kupelekwa kituoni.

Hata hivyo, hadi sasa bado haijafahamika chanzo cha Lissu kushikiliwa na Polisi, ingawa jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya aliliambia Mwananchi yupo katika ufuatiliaji kuthibitisha kuwepo kwa taarifa hizo.

Jitihada za Mwananchi kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya au Msemaji wa Polisi zinaendelea.

Chanzo: Mwananchi
Kumbe jana Walimwacha apumzike.

Allahuakbar
 
Hata hivyo, hadi sasa bado haijafahamika chanzo cha Lissu kushikiliwa na Polisi, ingawa jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya aliliambia Mwananchi yupo katika ufuatiliaji kuthibitisha kuwepo kwa taarifa hizo.
😅😅😅Kuna kipindi Yesu alikamatwa hata Pilato akawa hajui kwanini Yesu amekamatwa.

Akanawa mikono
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu anayeshikiliwa na polisi mkoani Ruvuma yupo njiani kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.

Lissu anayedaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma jana Jumatano Aprili 9, 2025 muda mchache baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbinga mkoani Ruvuma.

Wakati Lissu akidaiwa kuendelea kushikiliwa na polisi, huku wenzake watatu wakiwemo walinzi wake na kada mmoja wa chama hicho, Shija Shebeshi wameachiwa huru.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Aprili 10, 2025 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia amesema safari ya Lissu kusafirishwa kupelekwa jijini Dar es Salaam ilianza jana jioni baada ya kukamatwa na kupelekwa kituoni.

Hata hivyo, hadi sasa bado haijafahamika chanzo cha Lissu kushikiliwa na Polisi, ingawa jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya aliliambia Mwananchi yupo katika ufuatiliaji kuthibitisha kuwepo kwa taarifa hizo.

Jitihada za Mwananchi kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya au Msemaji wa Polisi zinaendelea.

Chanzo: Mwananchi
No reforms No ection ipo pale pale
 
Wao yawezekana wanapewa amri,tambua IGP,yaani mkuu wa askari polisi NCHI NZUMA ya TANZANIA,anateuliwa na RAIS ambaye ni MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI,na hao wapinzani wanaonyesha mwelekeo wa kuharibu UCHAGUZI ambao huwa SIYO HURU,ambapo MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI anateuliwa na MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI,ambaye pia ni RAIS wa nchi,unategemea nini?

Nchimbi anaanza kuchemka , mwaka huu kazi ipo kwa kiumbe huyu. Uchafuzi utapamba moto chini ya Nchimbi
 
Back
Top Bottom