nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
Saturday, 09 April 2011
MJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Tundu Lisu, jana alitoka ndani ya ukumbi wa mkutano kuhusu mjadala wa maoni wa muswada wa sheria ya mapitio ya katiba, kwa madai kuwa kulikuwa na kundi la watu waliokodiwa kuvuruga mchakato huo.
Lisu alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutoka nje ya kumbi wa mikutano wa Karimjee, kufuatia kuwapo kwa kundi la watu waliokuwa wakuzomea wachangiaji wa mjadala.
Akiwa nje ya ukumbi huo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kundi hilo lilikodiwa na CCM kwa lengo la kuvuruga mchakato huo, ili usifanikiwe.
Tundi pia aliwatupia lawama polisi katika Kanda Maalamu ya Dar es Salaam, kuwa wamekuwa katika katika eneo hilo, kwa lengo la kulinda kikundi hicho kilichokuwa kinafanya kazi ya kuzomea wachangiaji, waliokuwa wakikosoa muswada.
"Jana (juzi)tulikubaliana kwenye kikao cha kamati kuwa ulinzi katika mkutano wa leo (jana) ungeimarishwa na mtu yeyote atakayebainika kuwa anazomea au kuzuia maoni ya watu wengine kutolewa, polisi wangemtoa nje ya ukumbi, lakini kinchofanyika leo ni tofauti kwa sababu polisi wanawalinda wanaofanya vurugu," alisema.
Lisu pia alipinga muswada huo kwa maelezo kuwa una mapungufu mengi na kwamba hakuna
sababu ya kuupeleka bungeni kujadiliwa, kwa utumia hati ya dhararu.
Kwa mujibu wa Lisu, muswada huo ulipaswa kufuata njia ya kawaida ya kutunga sheria na si kwa hati ya dharura.
Alisema haiwezekani kwa muswada ambao ni mali ya wananchi na roho ya taifa, kujadiliwa ndani ya siku tatu na kupitishwa.
Alisema sababu nyingine ya kupinga muswada huo, ni vipengele vilivyopo ndani yake ambavyo alisema kwa maoni yake, vinakandamamiza uhuru wa watu kushiriki katika kutunga katiba.
Alisema kwa hali ilivyo, mjadala huo ulioandaliwa kwa siku chache hautakuwa na manufaa kwa wananchi na kwamba badala yake, utatengeneza manung'uniko kwa wananchi.
Alipoulizwa kuhusu hatua ya Lisu kutoka nje ya ukumbi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Pindi Chana, alisema hawezi kulizungumzia hadi kwanza apate sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo.
"Mimi muda huu siwezi kuzungumza chochote mpaka niwe na ushahidi wa kile kilichomfanya atoke ndani ya ukumbi wa mikutano,"alisema Chana.
Katika mjadala huo wadau mbalimbali waliochangia walipinga baadhi ya vipengele vya muswada kwa maelezo kuwa vinavunja katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

[/