LGE2024 Tundu Lissu atimba Ikungi na kugawa Nakala za viapo kwa Mawakala wa CHADEMA. Suphian Juma wa CCM naye kuwaongoza Wana Ikungi!

LGE2024 Tundu Lissu atimba Ikungi na kugawa Nakala za viapo kwa Mawakala wa CHADEMA. Suphian Juma wa CCM naye kuwaongoza Wana Ikungi!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakati God bless Lema wa Arusha na Pambalu wa Mwanza wakiendelea kulialia, Makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu yuko Ikungi Singida na mambo yanakwenda vizuri

Kadhalika mkoani Mbeya mh Sugu anaendesha seminar ya Mawakala na wanakwenda vizuri

Suphian Juma naye yuko Ikungi bampa to bampa na Ni Yeye anayewaongoza Manunda wa Ufipa

Ahsanteni sana
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu akigawa nakala ya viapo kwa mawakala wa chama hicho wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Tarafa ya Ikungi katika Halmashauri ya Ikungi mkoani Singida, Novemba 26, 2024.

1732622531963.png

1732622573499.png
 
26 November 2024
Ikungi, Singida
Tanzania

BALAA LA TUNDU LISSU IKUNGI SINGIDA, ATINGA KWENYE UAPISHAJI MAWAKALA, AGAWA FOMU KWA MAWAKALA WA CHADEMA


View: https://m.youtube.com/watch?v=BA1GgidGg8k
Mawakala wa CHADEMA wafurika kupata fomu zao kwa ajili ya wagombea wa CHADEMA uchaguzi wa kesho TAMISEMI tarehe 27 November 2024...

Tundu Lissu amesimamia zoezi na akigawa fomu za Mawakala wa CHADEMA Tarafa ya Ikungi mkoani Singida walioapishwa leo Novemba 26, 2024 tayari kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024
 
26 November 2024
Kata Ya Pamba
Mwanza Tanzania

Ezekia Dibogo Wenje -" Waalimu wasimamizi wa uchaguzi kesho Wapewa Maelekezo Kijani Washinde ... Kwa Kutimua mawakala wa vyama pinzani, Kura Tayari zimeshapigwa"


View: https://m.youtube.com/watch?v=qbPbzhh8W6E

Pia mawakala kuhujumiwa kwa kutupwa nje ya vituo ili kura zilizo katika mafurushi ziweze kuingizwa bila kuonekana na mawakala wa vyama ...
 
26 November 2024

CHADEMA KANDA YA SERENGETI WAIBUA MAMBO AMBAYO SERIKALI ITAFANYA JESHO 27 NOVEMBER 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=ZCpR_fNJv6U

Lucas Ngoto mwentekiti wa CHADEMA kanda ya Serengeti atoboa mikakati ya CCM kupata ushindi usio wa haki ..... kanda ya Serengeti CHADEMA ina majimbo 24 na mikoa 3 ...


Wafuasi wa CCM katika magandwa ya Mgambo kusimamia vituo vya uchaguzi kesho ...

Maelekezo yametolewa na mkuu wa wilaya Rorya amewaambia wasimamizi wa uchaguzi wasitangaze matokeo katika vituo hadi mkuu wa wilaya afahamu matokeo...

Matokeo ya kulazimisha yatafanyika kwa kutanganza kisha wasimamizi wasaidizi kukimbia vituo vyao ...
 
Mbinu za chama cha Frelimo Mozambique zimetumika na zitatumika siku ya uchaguzi TAMISEMI 2024 kupitia chama dola kongwe CCM . Je ni mbinu gani ? kuhitimishwa tarehe 27 November 2024:

Kigogo wa Tume ya Uchaguzi Mozambique ktk mahojiano exclusive - Mchakato na Uchaguzi uligubikwa na uchafuzi


View: https://m.youtube.com/watch?v=2B_xQtuZLW8

Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Fernando Mazanga asema uchafuzi wa uchaguzi na uchafuzi wa chakato wa uchaguzi, Tume haiwezi kusema nani alishinda..

Kwanza kiukweli kulikuwa na Tume mbili zinazosimamia mchakato, moja ni Tume ya Uchaguzi halisi isiyo na meno, na nyingine ni Tume Kificho ya Watu Wachache wa Frelimo waliokuwa na meno, rasilimali fedha na maamuzi ya kupika matokeo asema Fernando Mazanga

Alipoulizwa kuhusu Tume Kificho ya Watu wachache wa Frelimo ikifanyaje kufanya uchachuzi wa mchakato wa mzima wa matayarisho ya uchaguzi, uandikishaji na upigaji kura siku ya uchaguzi tarehe 9 Oktoba 2024 kigogo Fernado Mazanga alifunguka ...

Tume ya Ukweli ya uchaguzi ilinyimwa fedha na wizara ya fedha ya Mozambique na hata pesa zikipotolewa kidogo zote zikitumika makao makuu ya tume huku mikoani, wilayani na mitaani wasimamizi na wasimamizi uchaguzi walikuwa hoi si kifedha bali hata kimafunzo ya kuwapa uwezo wa kuandikisha wapiga kura, uteuzi na rufaa za mapingamizi.

Wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi walikuwa hawaelewi kanuni, sheria na miongozo ya kufanikisha uchaguzi ulio wa kiwango cha kukubalika ni huru, usiopendelea upande wowote na wakuweza kutoa matokeo sahihi ya kura zilizopigwa na mgombea yupi kazoa kura halali.

Fernando Mazanga anaongeza kuwa kutokana na Tume halisi kunyimwa uwezo wa kila aina, Tume kificho ya FRELIMO iliingia kazi kutangaza idadi ya watu waliojiandikisha ambayo haiwiani na takwimu za sensa ya taifa ya Mozambique ikiyofanyika 2023.

Wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi katika majimbo na wilaya walikosa kuwa na idadi za kulinganisha idadi ya watu katika maeneo yao ya majimbo, wilaya, kata na mitaa hivyo kura za ziada ya kuongezwa na FRELIMO ziliweza kutangazwa.

Huku wananchi hawafahamu idadi ya watu rasmo ktk maeneo yao kama sensa ya taifa ilivyokuwa ikionesha eneo kwa eneo, kijiji kwa kijiji, mtaa na kata.

Ingawa vyama makini vya upinzani zilipiga kelele kuwa idadi ya kuandikishwa watu katika sensa hailingani idadi ya wapiga kura watarajiwa na kura za matokeo yaliyotangazwa zimezidi kwa mbali idadi ya watu katika ripoti za sensa za taifa .

Wananchi baada ya kustuliwa kuhusu wafanye rejea za idadi ya watu na idadi ya wapiga kura wakabaini uchafuzi uliofanyika na kupelekea maandamano nchini Msumbiji kupinga matokeo yaliyotangazwa.

Mahakama ya Kikatiba iliyopewa mamlaka kusikiliza mapingamizi ya matokeo, imeomba tume ya uchaguzi ya taifa iwasilishe nyaraka ili ukaguzi ufanyike. Tume ilipewa siku 8 iwe imewasilisha nyaraka zote za uchaguzi uliofanyika 9 Oktoba 2024 zipitiwe na kufanyiwa ukaguzi wa kina.

Bw. Fernando Mazanga Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Mozambique anasema siku 8 zimepita na zinaonesha kuwasilishwa nyaraka zote zilizohifadhiwa katika Ofisi za Majimbo na Wilaya.

Lakini pamoja na nyaraka hizo kukusanywa sehemu, Mahakama ya Kikatiba hawajapewa makaratasi hayo ya kura na rejister za wapiga kura leo.

Inasemekana serikali inalaumu kutofika makaratasi hayo kutokana na vurugu za maandamano, lakini kigogo huyo Fernando Maganza anatillia shaka sababu hiyo kuwa vurugu zimezuia katatasi hizo kufika mji mkuu wa Mozambique Maputo.

Pengine Tume fiche ya Uchaguzi ya FRELIMO imeshikilia makaratasi hayo katika kituo salama (safe house) ikiyapitia matokeo hayo ya uchafuzi wa uchaguzi na kujiuliza wayawasilishe au la. Pia wanatafuta njia nyingine ya kuingilia mchakato wa Mahakama ya Kikatiba n.k n.k kujiokoa kutoka skandali hilo zito.

Fernando Mazanga alipoulizwa kama matokeo yanaweza kufutwa kutokana na uchafuzi wa wazi wa mchakato na uchaguzi sawia, kigogo huyo mzalendo wa Tume Halisi ya Uchaguzi anasema hawezi kutoa mawazo yake sasa kwa kuwa yeye ni mtu wa ndani kabisa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mozambique.

Hivyo anaiachie Mahakama ya Kikatiba ibebe majukumu yake kuhakiki na kutoa hukumu sahihi baada ya kujiridhisha na ushahidi wote anahitimisha naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchi Mozambique Bw. Fernado Mazanga.

Muito Abrigado kwa kutusikiliza
Source : DW Português para África : DW Kireno Africa

More info :
Maputo, Mozambique
Mahakama ya Katiba Mozambique yataka wasimamizi wa uchafuzi wa uchaguzi kujitetea madudu ya wazi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 9 Oktoba 2024 nchini Mozambique
1732644185292.jpeg

Picha : Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Kikatiba Mozambique
 

MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MANISPAA YA SHINYANGA YAELEZWA KUKAMILIKA, CHADEMA YALALAMIKA VITUO KUONGEZWA​

Misalaba November 26, 2024


Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze, ameeleza kukamilika kwa asilimia 100 kwa maandalizi yote uchaguzi wa Serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika hapo kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 26, 2024, Kagunze ameeleza kuwa, hatua zote za maandalizi zimefanyika kwa ushirikiano wa karibu na wadau wote wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa Serikali na vyama vya siasa na kwamba, jumla ya vituo 285 vitatumika katika zoezi la upigaji wa kura katika Manispaa ya Shinyanga.

Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kutumia haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka, huku akiwasisitiza kudumisha amani wakati wote wa zoezi la uchaguzi.

Kagunze amesema Jumla ya vyama 9 vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo, huku akivitaja vyama vya CCM na CHADEMA kuwa ndiyo vyenye wagombea wengi zaidi ambapo vingine vilivyobaki vimesimamisha wagombea katika maeneo machache.

Taarifa hiyo ya Msimamizi wa uchaguzi inakuja huku chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi, kikilamikia kuongezwa kwa vituo vipya 122 bila chama hicho kushirikishwa mapema ili kuandaa mawakala, kinyume na orodha ya vituo 163 walivyopewa hapo awali.

Uchaguzi huo wa Serikali za mitaa ambao utawapa fursa wananchi wa Tanzania bara kuwachagua Wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji pamoja na wajumbe wao, utafanyika kesho Jumatano Novemba 27, 2024, ambapo vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Source : misalaba media
 
Back
Top Bottom