Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

JK anadai yy kazi yake ni ku-balance gender kutoka kwenye list ya majina aloletewa...WHAT A CHEAP ANSWER...

Hii inanikumbusha maswali ya multiple choice...kwamba ni lazima ujaze herufi hata kama hakuna jibu sahihi from the list of proposed answers....

haha ha...
Hahahahahaha ila kweli aaisee
 
alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.
hapa nimekuelewa Lissu.
 
Lissu amkomalia JK

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Lissu alisema Bunge litaangalia kama rais ameteua majaji kwa mujibu wa katiba au ameikiuka, na kwamba yeye ana uhakika kuwa rais amekiuka katiba.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012

Dah JF ni kiboko. Kila kitu ukitaka unakipata see this was 2012.
 
Bilisikiliza hotuba ya Arusha, JK alikuwa anaongea kama mtu asiye na uhakika na akisemacho kuhusu suala hili. Pia alikuwa anaongea kisiasa kuliko uhalisia.


Aweke ushahidi hadharani mfano LISSU amewataja baadhi ya majina, Sasa kama si kweli basi waweke hadharani vielelezo vya majaji hawa. Au wenyewe wajitokeze kukanusha kutokana na vigezo.

ACHENI BLABLABLa​


MIZAMBWA
nabii mtarajiwa!!!
Mungu Mbariki mtumishi wako Tundu Lissu .
 
Si ajabu hao ni ndugu zake au waliwahi kuwa washikaji zamani Raisi wetu ni zaidi ya umjuavyo yeye kufuata katiba kuendesha nchi kwake ni tusi ,ashukuru watanzania wapole kama kondoo nchi zingine angekiona
We unajua anamzungumzia nani lkn au unkurupka na chuki zako kujibu
 
Lisu is a very intelligent person , ishu zake nyingi anazoziibua mwanzoni wapuudhi wanamuona mzushi ila mwishoni lisu anaibuka mshindi.
Mungu akubariki na akupatie Maisha marefu sana wewe ni tunu kwenye nchi yetu.
Unafaa kuwa rais wa nchi hii kwa kweli
 
Labda anabalance gender na dini, au ushemeji, au kulipa fadhila.
 
Kikwete ni janga la taifa, yeye na Chenge ni mapacha. Huyu mtu akamatwe na kunyongwa tu, hana faida na taifa letu.
 
Lissu ni hazina,

Lissu apewe nchi jamani huyu bwana mdogo ni mzalendo hakuna mfanowe!
 
Lissu siku zote watu wanaompinga huwa hawakatai hoja zake, huwa wanaleta tu maneno ya hovyo hovyo. They never go to the core of the arguments
 
Lissu katoa vigezo vyake anavyotaka yeye; Raisi anateua majaji kwa mujibu wa katiba inavyomruhusu; sasa yeye Lissu kama haradhiki na uteuzi wa majaji huo ni mpango wake; mpaka sasa hakuna aliyelalamika na maamuzi ya majaji husika na kwa utaratibu wa maamuzi ya mahakama kuu na rufaa ni jopo la majaji ndilo linalotoa maamuzi; Lissu na atueleze ni wapi Raisi amekiuka madaraka yake kuteua hao majaji.
Hoja hapa sio kwamba watu wanalalamika au hawalalamiki, hoja ni kwamba sheria imekiukwa bila kujali utendaji.
Sasa hivi nchini kuna sakati la kuwatimua makazini wenye vyeti feki, kwanza wote walilalamikiwa? Wengine ni watenda kazi wazr lkn bado sheria imekiukwa.
Sio lazima ukosoe.
 
Tuwe na TUME safi za KITAALUMA. Watu waombe kazi hizi. Ifanyike vetting ya hali ya juu. Interview ziwe wazi kabisa. Wenzetu hapa Kenya sasa hata JAjiMkuu anaomba kazi kwa uwazi kabisa hadi TV zinaonyesha "live" mahojiano. Kenya wanatuacha sana.


Tundu Lissu njoo huku utupe mwongozo wa uteuzi wa majaji unasemaje?
 
Back
Top Bottom