Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tundu Lissu amewataja baadhi ya viongozi na Wanachama wa CHADEMA ambao hawajatubu kwa Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe na anawashughulikia ipasavyo ndani ya Chama.
"Tukikutana hivi kwenye vikao hatupigani ngumi, hatuko kama tulivyokuwa mwanzoni. Mwenyekiti aliyekwenda gerezani, sio Mwenyekiti aliyetoka gerezani na huyo sio mimi peke yangu ninayesema hivyo, mimi sasa ni mhaini wa sasa, kulikuwa na mhaini anaitwa Peter Msigwa, kulikuwa na mhaini anaitwa John Heche, kulikuwa na mhaini anaitwa Godbless Lema, kulikuwa na mhaini anaitwa Gaston Garubindi, kulikuwa na mhaini anaitwa Ezekia Wenje kabla hajaenda kufanya Sala ya kitubio na kutubu dhambi zake kwa Baba yetu.....akisema nimekosa mimi, nimekosa sana ndio dhambi zake zikafutwa hao wengine niliowataja hawajatubu na wamekuwa wakishughulikiwa kweli kweli"
Soma, Pia: Mbowe amvaa Dkt. Slaa kisa Tundu Lissu, adai "mpiga debe wa CCM hapaswi kutufundisha CHADEMA"