Tetesi: Tundu Lissu azawadiwa gari(Bus)

Tetesi: Tundu Lissu azawadiwa gari(Bus)

Status
Not open for further replies.
Nasikitika hujui unacho kisema. Wewe kama mtanzania una nini, kiasi kwamba ukafanya kitu bila Amerika? Ambayo wengi humu mnaisifu kuwa ni nchi yenye Demokrasia pure?

Any way, sikiliza mkuu inavyo onekana ni kuwa unapenda kutoa hoja ya vitu ambavyo umevisikia lakini huna uhakika navyo. Sasa subiri nikukalishe chini. Hizo habari za kuhusu uchawi wa kanda ya ziwa mwaka 77/78 huo utakuwa ni uongo, kwani katika miaka hiyo Kanda ya Ziwa haikuwepo badala yake Tanzania iligawanyika katika majimbo makubwa Manne. Jimbo la Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. Hapakuwa na Kanda ya Kaskazini wala Central corridor.

Mwaka 1977 East African Community ilikufa. Storry ilikuwa kubwa sana kuhusu kuvunjika kwa EAC. Watu wengi sana walipoteza kazi na wengine kutupwa mpakani na wakenya, ni kitu ambacho watanzania wa generation yangu hatuta kisahau. Ilikuwa ni muda wa giza kubwa sana kwa nchi ambayo ni changa na ambayo ilikuwa inaanza kuyaweka maisha ya wananchi wake katika hali nzuri ya maendeleo. Mwaka huo huo pia Chuo Kikuu cha DSM kilifungwa na Mwalim Nyerere kwa sababu ya maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu. Na mwaka 1978 tulienda vitani dhidi ya Id Amin Dada. Hizo habari za Kanda ya Ziwa ngoja ni Pass, sijawahi kusikia miaka hiyo. Nitazifanyia uchunguzi!

Umesema vizuri kuwa serikali haijatoa Statement yeyote kuhusiana na watu walio kuwa wanawaua polisi wetu. Sina haja ya kueleza mengi kwani najua serikali inatenda wajibu wake kama inavyo paswa. Mda utafika wa kusikia mengi kutoka kwa wahusika. Subira lazima iwepo.

Unajua watu wengine mnaudhi sana. Yaani mnajisahau kama polisi nao ni binadam na wanastahili kuishi vile vile. Ingekuwa rahisi kama unavyo dhani nafikiri mambo yangekuwa mengine. Kuuliza swali la kwanini hao wauaji waliamua kuwaua polisi? Hilo swali sidhani kama ni rahisi kujibiwa, maana mawazo ya kuua mtu mwingine bila sababu, hiyo itakuwa kwenye ubongo wa huyo mtu aliyesababisha hayo mauaji ya polisi. Vinginevyo mtu unatakiwa uwe na uwezo wa Yesu Kristo kuweza kutambua nini kinaendelea katika ubongo wa binadam mwingine. Na kama huyo mtu ameuawa katika mapambano hiyo nafikiri ndiyo kabisa is difficult. Binafsi naona ni swali la kijinga. Maswali kama haya yanaulizwa na watoto wadogo ambao wanaanza kujifunza jinsi ulimwengu unavyoenda.

Katika maswala yanayo husu siasa na vyama kuhusika, kupeleka malalamiko Bungeni hiyo isiwe ndiyo ufumbuzi wa matatizo ambayo wanachi wanakabiliana nayo. Ningependa utambue kuwa vyama vya siasa na hasa vyama vya upinzani ulimwenguni kwote vinapo peleka malalamiko yao Bungeni, utambue kuwa mara nyingi ni kutaka kiki na vile vile kutaka kukidhalilisha chama kinacho tawala ili kuwaonyesha wapiga kura waone chama tawala kinavyo fanya makosa. Vyama vya upinzani always haviko kwa ajili ya kuvisifu vyama tawala. Usitegemee hilo. Na ndiyo maana vinafanya kila wawezalo kuupotosha uma ili katika uchaguzi wapiga kura wawa pigie wao kura. Ni kawaida.

Kama kweli kuna uonevu umefanyika wa hali ya juu namna hiyo kama unavyo jaribu kutuaminisha au wapinzani wanavyo jaribu kuwaaminisha wananchi yaliyotokea, nashangaa na kustaajabu kwanini wasipeleke mashtaka ya malalamiko hayo mahakamani?

Kama kuna unyama kweli umefanyika wapinzani kwa kushirikiana na mawakili wangekusanya informations za matukio na watu walio kumbwa kweli na mkasa na wangepeleka mashaka kwa hakimu na kuishtaki serikali. Sielewi kwa nini mpaka sasa hatua kama hizo hazijachukuliwa.

Inananiwia kidogo vigumu kuamini kama kweli hali ndiyo hivyo kama wapinzani wanavyo dai. Kuwa mwangalifu na wapinzani. Hawana lengo la kuisifu serikali. Lengo lao ni kukiangusha chama kinacho tawala kwa Ballot kama hujui.

Kama unafuatilia malumbano yanayo endelea Amerika kati ya Democratic Party na Republican na vile vile England na the Rest of Europe kuhusu maswala ya BREXIT, with a Deal or with no Deal na Treaty ya Back Door na kadhalika, utaona kuwa hiyo ni political circus tu! Ukweli wa mambo ni ushindani wa kisiasa na sio zaidi ya hayo.

Sidhani kama kuna mtu au serikali ambayo inafanya ukatili wa namna hiyo Tanzania. Inawezekana kuna baadhi ya watu ambao wana attitude ya aina hiyo, lakini huwezi ukadai kuwa serikali yetu ina tendence hiyo. Si kweli na atapenda kukubaliana na mawazo ya kinjinga ya namna hiyo.

Pamoja na hayo lazima tukubaliane kuwa hii hali ya magaidi kuamua kuyatoa maisha ya watu bila kutoa sababu zozote haiwezi likawa jambo la kulifumbia macho eti kwa sababu hatutaki serikali inayo wafanyia wananchi wake ukatili. Vitendo vya aina hii ni lazima vikomeshwe kwa nguvu zote. Na ndiyo maana navipongeza vyombo vya usalama kwa hatua iliyo chukua kukomesha vitendo vya ovyo namna hiyo.

Well done jeshi letu la usalama. Mmefanya kazi nzuri sana. Na sisi wananchi wazalendo kwa nchi yetu tuko sambamba na nyie. BIG UP![emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakushangaa sana. Unadai wewe ni mwananchi mzalendo, hivyo unavipongeza vyombo vya usalama kwa kupoteza raia!!! Maajabu. Nimekupa mfano mmjoja wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa miaka ya 1977/78 kwenye mauaji ya "wachawi"
Wakati Rais mwenye kuheshimu Misingi ya Utawala bora, Mwalimu J. K. Nyerere, aliunda Tume ya Uchunguzi juu ya suala hilo. Matokeo Ni kwamba ukweli ulithibitika kuwa vyombo vya ulinzi na usalama unavyovisifu leo vilipatikana na tuhuma zilisababisha Waziri wa mambo ya ndani Ali Hassan Mwinyi, Wakuu wa Mikoa mitatu ya Mwanza, Shinyanga, Tabora walijiuzulu na Inspector Generali Polisi walijiuzulu. Baadhi ya viongozi wa vyombo vya usalama wakiwemo wa Usalama wa Taifa walipelekwa mahakamani na kupatikana na hatia. Kwa hiyo si suala la upinzani wa kisiasa. Suala Ni kuwa hata wale wanaooneka kutaka kujua ukweli wa kilichokuwa kinatokea MKIRU kwa kukusanya data, wanatoweka!!!! Mfano Ni Azory Gwanda mwandishi wa gazeti la mwananchi.
Wabunge wa maeneo hayo wamepeleka data ya watu wanaokaribia 400 kutoweka. Hili si suala wabunge tu wa upinzani, maana wabunge wanaotoka maeneo ya MKIRU Ni mchanganyiko.
Muhimu hapa Ni Serikali inayojinasibu kuwa ya Wanyonge kuja hadharani na kutuambia Nini hasa kilikuwa kinatokea katika maeneo hayo, na watu wangapi wamepata maumivu yasiyo halali wakiwepo Polisi.
Mwisho, Aliyekuambia kuwa Amerika Ni mfano tukuka wa demokrasia duniani alikudanganya. Lakini waamerika wana tabia moja iliyotukuka kwamba: Hawako tayari kuuvumilia ujinga wa viongozi wao.
 
Safi sana. Na ili kukwepa figisu za bandarini, gari hiyo itaingia nchini kupitia bandari ya Mombasa na kisha kusafirishwa kuja nchini kwa njia ya barabara. Msidhani CHADEMA ni wajinga kama CCM. MaCCM endeleeni kujitekenya na kucheka mkidhani mtaizuia kuingia nchini. Mmeliwa!!!!!!!!
 
Ma ccm walio wengi wanadhani bandari ni moja tu ya dar
Safi sana. Na ili kukwepa figisu za bandarini, gari hiyo itaingia nchini kupitia bandari ya Mombasa na kisha kusafirishwa kuja nchini kwa njia ya barabara. Msidhani CHADEMA ni wajinga kama CCM. MaCCM endeleeni kujitekenya na kucheka mkidhani mtaizuia kuingia nchini. Mmeliwa!!!!!!!!

In God we trust
 
Kwa wapenzi wa demokrasia popote walipo ulimwenguni lazima tumpongeze mh Lissu kwa kukubalika kwake duniani kote.
Mh amekabidhiwa basi jipya kabisa ili litumike kukiimarisha chama chetu pendwa cdm na watanzania wanao ishi ubelgiji hongereni sana ndugu zetu.View attachment 1043864

In God we trust
Hii inafaa sana kuiweka kwenye mwendo kasi ipunguze foleni 🤓🤓🤓

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio expert sana katika graphics ila hapo picha ya wazi kabisa wamefanya editing
hakuna kitu kama hicho hapooo

Ukubwa wa maneno na nembo kiutaalamu umezidi ratio ya ukubwa wa gari
pia ziko juu haziko katika gari
pia designing ya gari kwa ubora wao wasingeweza kufanya design mbovu hiyo
so hapo ni uongo hakuna cha basi wala nini
Mkuu usipate tabu Sana.. hiyo picha ni ya PHOTOSHOP ., Lissu hajapewa basi lolote yupo anaomba msaada baada ya mshahara kuondolewa.Nakuwekea picha na link ya walipotoa picha ya hilo basi waliloedit na kuweka maneno yao...

Screenshot_20190312-230438.png
 
Kwa wapenzi wa demokrasia popote walipo ulimwenguni lazima tumpongeze mh Lissu kwa kukubalika kwake duniani kote.
Mh amekabidhiwa basi jipya kabisa ili litumike kukiimarisha chama chetu pendwa cdm na watanzania wanao ishi ubelgiji hongereni sana ndugu zetu.View attachment 1043864

In God we trust
Bora imefika picha tu huku likija hilo mtatulipa kodi zetu tu kwa gari hilo tukajenge SGR, hizo sera bakini nazo huko ubeligiji
 
Mkuu usipate tabu Sana.. hiyo picha ni ya PHOTOSHOP ., Lissu hajapewa basi lolote yupo anaomba msaada baada ya mshahara kuondolewa.Nakuwekea picha na link ya walipotoa picha ya hilo basi waliloedit na kuweka maneno yao...

View attachment 1046890
Chama cha wahuni wa mitandaoni. Utafikiri basi ndio uhai wa chama.
 
Safi sana. Na ili kukwepa figisu za bandarini, gari hiyo itaingia nchini kupitia bandari ya Mombasa na kisha kusafirishwa kuja nchini kwa njia ya barabara. Msidhani CHADEMA ni wajinga kama CCM. MaCCM endeleeni kujitekenya na kucheka mkidhani mtaizuia kuingia nchini. Mmeliwa!!!!!!!!
Hakuna basi hapo ni PHOTOSHOP....
Mnakaribia kuokota makopo..
Screenshot_20190312-230438.png
 
Mbona mnatwambia SGR tayari mapesa yapo tayari?
Bora imefika picha tu huku likija hilo mtatulipa kodi zetu tu kwa gari hilo tukajenge SGR, hizo sera bakini nazo huko ubeligiji

In God we trust
 
Naona umerthi tabia za kuchukia wapinzani kama mwenyekiti wako
Chama cha wahuni wa mitandaoni. Utafikiri basi ndio uhai wa chama.

In God we trust
 
Naona umerthi tabia za kuchukia wapinzani kama mwenyekiti wako
Chama cha wahuni wa mitandaoni. Utafikiri basi ndio uhai wa chama.

In God we trust
 
Naona umerthi tabia za kuchukia wapinzani kama mwenyekiti wako
Chama cha wahuni wa mitandaoni. Utafikiri basi ndio uhai wa chama.

In God we trust
 
Naona umerthi tabia za kuchukia wapinzani kama mwenyekiti wako

In God we trust
Sichukii upinzani mkuu hata 2015 nilipigia kura upinzani. Lakini kinachokera ni sera za kiuanaharakati na usanii ndani ya upinzani. Yaani ukabidhi nchi kwa mafisi.
 
Yapo ya kumalizia ya Dodoma lakini ujue SGR haijafika Mwanza na kwa jirani yetu Kagame.
Kagame ni jirani yenu au ndugu wenu wa damu?

In God we trust
 
Fisi na chui hawana tofauti hao

Back
Top Bottom