Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Ruzuku huwa zinatumika kuendesha Chama unafikiri zinangojea Uchaguzi wa Mwenyekiti?Chama kimenunua Jengo la Makao Makuu ya Chama Mikocheni.Na ruzuku pia huwa zinakaguliwa na CAG.Unafikiri unapewa tu na unatumia unavyotaka.Asilete tu masharti na malalamiko achangie na nyie changieni kama ni rahisi ili Mkutano ufanyike tarehe 21.
Ni mentality ya kitoto kusema kifanyike hiki na kile bila kujua pesa kama zipo.

Mnanunuaje jengo la bil 1.6 then mnalalamika hamna hela ya uchaguzi?

Mnabidi kujitafakari Kwa hilo PIA.

Mtu makini lazima awe na priority in his or her decisions.


Wangenunua Nyumba ya mil 500 then hela nyingine wakafanyia uchaguzi

Huo ujinga tundulissu anabidi asiruhusu
 
Mnanunuaje jengo la bil 1.6 then mnalalamika hamna hela uchaguzi?

Mnabidi kujitafakari Kwa hilo PIA.
Chama kilishajiwekea malengo kwamba wajumbe wa Kamati Kuu watoe michango ya kufanikisha Mkutano Mkuu.Hao mnaowasifia ndio wanakwamisha kwa kutotoa michango yao.Wawili wameganda na mmoja kakimbilia Canada.
Ndio sababu kwa nia njema kabisa Mwenyekiti Mbowe ametoa milioni 250 ili Mkutano Mkuu ufanyike.Usipofanyika madhara yake kikatiba ni kwamba Chama kinaweza kufutiwa usajili.
Wenye kupiga domo na kupenda popularity kwao hiyo sio priority. Priority ni kulumbana badala ya kufanya kila linalowezekana Mkutano Mkuu ufanyike.Talk is cheap.
 
Nyerere wa kizazi hiki anaongea.
Mbona anatumia nguvu kubwa sana kana kwamba ni suala la kufa na kupona?

Hizi siyo dalili njema.

Maana yake akishindwa atadai ameibiwa kura na kuhama au kukigawa chama.

Yaani ni aidha awe mkiti ama chama kife.

Hiyo ni nia ovu.

I can smell Lissu hana nia njema.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Chama kilishajiwekea malengo kwamba wajumbe wa Kamati Kuu watoe michango ya kufanikisha Mkutano Mkuu.Hao mnaowasifia ndio wanakwamisha kwa kutotoa michango yao.Wawili wameganda na mmoja kakimbilia Canada.
Ndio sababu kwa nia njema kabisa Mwenyekiti Mbowe ametoa milioni 250 ili Mkutano Mkuu ufanyike.Usipofanyika madhara yake kikatiba ni kwamba Chama kinaweza kufutiwa usajili.
Wenye kupiga domo na kupenda popularity kwao hiyo sio priority. Priority ni kulumbana badala ya kufanya kila linalowezekana Mkutano Mkuu ufanyike.Talk is cheap.


Kati ya kununua Nyumba ya billion 1.6 na kufaya uchaguzi kipi ni muhimu .

Utamwambiaje mtu achangie mil 30 wakati chama kinapokea ruzuku zaidi ya mil 100+ kila mwezi .

Kumbuka hapo chadema watu wanaoliowa mshahara hawafiki watu 20.

Mgetoa mchangunuo mzuri wapi mnaipelekea hiyo ruzuku ambayo ni mil 100+ kila mwezi .
 
Kwani Chama hakipokei ruzuku?
Ruzuku ndio imenunua Makao Makuu ya Chama.Ilikuwa ni aibu kwa Chama kiwe na ofisi za kukodisha.Hilo pia hamlitaki.Badala ya kumwambia mgombea wenu atimize ahadi aliyotoa ya kuchangia milioni 30 mnabaki kuulizia ruzuku.Lisu hataki kutoa milioni 30 kwani anajua he is losing.
 
Ndio nimemaliza kuitazama hotuba yote. Hotuba fupi iliyojaa hoja za msingi.

Lissu ni mwanasiasa kamili, ana sifa zote za kukiongoza chama kikuu cha upinzani nchini. Chadema mtatukosea sana msipompitisha Lissu, hatutolaumiana kwenye sanduku la kura uchaguzi Mkuu.
Mtavuna mlichopanda endapo mtamchagua tena king'ang'anizi Mbowe.
 
Mbona pressure ipo juu Mkuu?Kila Press Conference analalamika tu.Leo kaja na masharti mengi ya namna anavyotaka Uchaguzi uwe.
Anataka viongozi wa dini wasimamie Uchaguzi kama observers eti ili haki itendeke.
Unawapa picha gani wajumbe wanaopiga kura kwamba huwaamini.Wanaopiga kura ndio waamuzi wa nani atakuwa Mwenyekiti kuwaamini na kufanya kampeni ili wakuchague ndio priority.Yeye ameanza kampeni mapema ili akienguliwa aseme kaonewa.Nafikiri ameona wazi hana nafasi ya kushinda. Hiyo scenario ya kuanza kampeni mapema Slaa ameitumia juzi kama kisingizio.
Wee ni mpumbafuu kumbe
 
Uongozi ni falsafa.

Falsafa za lisu zinajulikana hata kwa wasio fatilia siasa
1.Kupinga rushwa
2.Kupinga ufisadi
3.Kupinga uongozi usiofata katiba na sharia

Sasa wajumbe kazi kwenu
Ndiyo maana tunamuhitaji Lissu kutokana na mazingira ya sasa. Lissu ni chaguo sahihi kwa wakati sahihi. Mbowe anafaa ila si sahihi kwa wakati huu.
 
Mhe Lissu kama alivyoahidi kuhutubia Taifa Leo siku ya tarehe 01.01.2025 majira haya ya mchana,

Mhe Lissu ni mkweli na tayari amenafanya hivyo msikilize.

Usiondoke Jf kwa habari na madili mbalimbali



View: https://www.youtube.com/watch?v=ozQqkisoXJ4

==============================================

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Tundu Lissu amesema:

"Kiuhalisia kama sio kisheria, nchi yetu sasa iko kwenye utawala wa kiimla usiokubali ushindani wa kiuchaguzi wa wazi wazi. Kama baada ya chaguzi hizo mbili (2019 na 2020) kuhusu aina ya utawala wa kiimla tulionao mashaka hayo yameondolewa na Uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka huu"

"Kuanzia sasa hakuwezi kuwa na ubishi miongoni mwetu kuwa bila kupigania na kubadilisha mfumo mzima uliopo wa kikatiba, kisheria na kitaasisi wa mfumo mzima wa Uchaguzi, hakutakuwa tena na uwezekano wa kuwa na Uchaguzi ulio wa wazi na haki"



  • Lissu ameishauri kamati kuu kuwepo na mabalozi wa nchi rafiki kama watazamaji na waangalizi wa uchaguzi wao wa ndani ya chama:

"Sambamba na viongozi wa kidini, kamati kuu vile vile iwaalike wawakilishi wa kibalozi wa nchi rafiki ili nao washiriki kama watazamaji wa uchaguzi wetu. Hiyo pia itaongeza uzito wa uchaguzi wetu ikiwemo kuongeza macho dhidi ya wale wote wanaopanga uchaguzi huo"


  • Kuhusu ukomo wa madaraka kwa wabunge na madiwani wa viti maalum ndani ya CHADEMA, Lissu amesema:

"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"

"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"



  • Lissu pia ameonesha kushangazwa na watu ndani ya CHADEMA wanaopinga hoja ya ukomo wa madaraka:
“Mimi nimependekeza kurudisha ukomo wa madaraka katika mfumo wa uongozi wa chama chetu, na katika uwakilishi wa wanawake bungeni na katika halmashauri za serikali za mitaa.

Hili ni jambo la pili linalohitaji kufanyiwa kazi ili tuweze kujiweka sawa kitaasisi. Katika hili ni lazima nikiri kwamba nimeshangazwa sana na mapokeo ya baadhi ya viongozi wa juu wa chama chetu.

Sikuwahi kufikiri kwamba, kwenye suala la ukomo wa madaraka ya kisiasa, kuna baadhi yetu ndani ya chama ambao, kwa kujielewa au la, bado wanatamani kuirudisha nchi yetu nyuma kikatiba kwa zaidi ya miaka arobaini.”

Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama.

Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”


  • Kuhusu kuachiliwa kwa George Sanga, Tundu Lissu amesema:
"Huu ulikuwa ni mwaka wa George Sanga mfungwa mwingine wa kisiasa ambaye amemaliza miaka 4 na amemaliza mwaka wa 5 ndani ya gereza la Njombe akiwa ni mhanga wa siasa za kiuchaguzi za John Pombe Magufuli na kazi inayoendelea na Samia Suluhu Hassan."

  • Kuhusu Maridhiano kati ya CHADEMA na Samia, Lissu alisema:
"Kuna wale ambao kwa sababu ya maslahi na vijimanufaa fulani fulani wamejisahau na kuanza kumsifia na kumsafisha utawala wa kiimla wa Samia Suluhu Hassan"

"Kama maridhiano na Samia yalikuwa na manufaa makubwa kama tunavyoambiwa sasa, tuwaambie nini wajane na watoto wa Marehemu Medi George Juma Mohamed, Steven Chalamila na Modestus au tuwaambie nini wazazi na ndugu zao Deus Soka, Emanuel Mbise, Jacob Mlay, Shadrack Chaula na John Kipanya"

"Au maaan ya maridhiano ilikuwa ni kupeana michongo ya pesa tu?"

Hotuba imepangiliwa.
Hotuba imetoa uelekeo.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Mnaongea sana kabla ya uchaguzi ili kujijengea mazingira. Mbowe sio mjinga kukaa kimya. Yule ni Mwamba wa Siasa za Chadema. Utaona mwenyewe.
Sasa aongee ana hoja gani mkuu za kumbeba??
Hana namna ni lazima akae kimya...amehudumu miaka 21 leo hii kwa wenye akili atawaambia ana nn kipya kwa maendeleo ya chama?!.
 
Lissu akiwa mwenyekiti Kuna mawili:-

1. Nchi kuingia kwenye machafuko, maana anafahamika jinsi anavopenda Shari

2. Chadema Kua na mwenyekiti hewa, Endapo akitimkia ubelgiji Kama kawaida yake (Kuhofia maisha yake).

..machafuko hayawezi kutokea kwasababu ya Tundu Lissu.

..machafuko yatatokea kwasababu ya udhalimu wa Ccm.

..wasiopenda HAKI ndio watakaosababisha machafuko na sio Lissu.
 
Yaani wewe unaweza ignore veteran politician, kwa kuweka njuka bungeni.

Akili zake zinamtosha mwenyewe.

Mwanasiasa ajajingea ufuasi kwenye jamii umuweke bungeni, utoe mwenye influence kwenye jamii. Kisa katiba ya chama.

Akili zake zinamstosha mwenyewe, Lissu ni mwanaharakati sio mwanasiasa.

..bungeni utaingia vipi bila kuwa kwanza umejijengea ufuasi kwa watu wa eneo lako?

..wakina Bob Makani wangeng'ang'ania madarakani huenda tusingepata nafasi ya kujua uwezo, na kufurahia utumishi wa, Freeman Mbowe.

..ukomo wa madaraka ni muhimu. Tanzania ina watu MILLIONI 60++ hakuna uhaba wa vipaji vya kuongoza.
 
..bungeni utaingia vipi bila kuwa kwanza umejijengea ufuasi kwa watu wa eneo lako?

..wakina Bob Makani wangeng'ang'ania madarakani huenda tusingepata nafasi ya kujua uwezo, na kufurahia utumishi wa, Freeman Mbowe.

..ukomo wa madaraka ni muhimu. Tanzania ina watu MILLIONI 60++ hakuna uhaba wa vipaji vya kuongoza.
Unaandika kama ni Mbowe aliyetoa ukomo wa Uongozi Chadema.Kwa katiba iliyopo Mbowe ana haki ya kugombea mpaka itapowekewa ukomo.Kumnyima haki hiyo ni kuisigina katiba iliyopo.
Kuna uoga wa nini?Kwani Mbowe akigombea ndio Lisu hawezi kuwa Mwenyekiti?
Uamuzi wa kuondoa ukomo ulifanywa na Mbowe peke yake?
Mnatetea demokrasia huku mnasigina uwepo wake uamuzi uliofikiwa ndio utakuwa valid mpaka ubadilishwe kwenye vikao.
Kuachiwa mnayemtaka ndio demokrasia mnayoiamini na sio Uchaguzi.
You cannot eat your cake and have it too.
 
Huyu rafiki wa Msigwa anashangaza sana. Ni kama vile Mbowe alijifungia chumbani na mke wake wakaondoa nkomo kwenye katiba ya chama, kuwa yeye hakuwa sehemu ya mchakato huo.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Sasa aongee ana hoja gani mkuu za kumbeba??
Hana namna ni lazima akae kimya...amehudumu miaka 21 leo hii kwa wenye akili atawaambia ana nn kipya kwa maendeleo ya chama?!.
Mbowe anajua aongee na nani, wakati gani, sehemu na nini Cha kuongea!
 
Back
Top Bottom