Tundu Lissu: CCM niliachana nayo nilipojiunga chuo kikuu

Tundu Lissu: CCM niliachana nayo nilipojiunga chuo kikuu

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
14 February 2023

TUNDU LISSU AIBUA MAPYA - ''VYUMA VIMEKAZA, CCM NILIACHANA NAYO NILIPOJIUNGA CHUO KIKUU




GLOBAL TV imefanya mahojiano maalum na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu ambaye amezungumza mengi juu ya muelekeo wa hali ya kisiasa nchini akigusia vyama vya siasa, katiba mpya na mambo mengine mengi.

Source: Global TV online
 
b201489e5c0e22213702c476ddaf234a.jpg
 
Mahojiano megine mazuri kabisa baina ya Tundu Lissu na chombo cha habari cha Tanzania, kufungua bongo za vijana kuwa hata Tanzania inawezekana kama kwa nchi zingine na vijana kujiunga na CHADEMA ili mabadiliko ya kweli yapatikane.

KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO

VIJANA WA TANZANIA KUANZISHA JUKWAA LAO HURU, NDIYO JIBU LA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKISHWA KTK NGAZI YA MAAMUZI KITAIFA

Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza / kispaniola vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Vijana wengi pamoja na umasikini wa familia zao wanashawishiwa kwenda vyuo vikuu kwa kuchukua mikopo wakiwa na matumaini ambayo ni hadaa kuwa kwa kumaliza elimu ya juu watakuwa sawa na wale watoto wa tabaka la watawala anasema kiogozi wa vuguvugu la wanafunzi wa chuo kikuu wa Chile kamanda Gabriel Boric mwaka 2017.

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhishs wananchi kama matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo ziluxokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Chile nchi iliyo na kiongozi kijana Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement

Likes
59,554
Views
2017
14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.


Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.


Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Back
Top Bottom