Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

Kwa maana hiyo Chadema hamwajibisha yeyote aliyekosea huko nyuma kwa kuwa kosa si lake ni la mfumo wa CCM? Na kama mkichukuwa madaraka na mtu akafisadi, mtawezaje kutofautisha kuwa hilo ni kosa lake au la mfumo wenu? Kura yangu mmeikosaje
 
AHSANTEH PROF. LIPUMBA kwa kauli yako hii "Lowasa amaeondoka serikalini 2008 UFISADI umeongezeka".

My take: Kama Lowassa alikuwa tatizo kwenye ufisadi, basi UNGEPUNGUA ama kuisha kabisa.
 
Tupo pamoja, Mbele kwa mbele. Lowassa ni mtaji mkubwa na bora katika siasa za upinzani. Vilevile ni shortcut kuing'oa CCM Madarakani.

Ninazipenda sana siasa za nchi ya Kenya , hakuna kuombana msamaha, hakuna kudai fidia ya kuzalilishwa. Wanasiasa wa Kenya wasema kama wewe ako na evidence enda kwa court kushitaki.

Kwa kweli Lowassa walimuonea kama sio wangempeleka mahakamani mbona Mramba na Yona wamekula miaka tena kwa kosa la kutumia madaraka yao vibaya tu. Sembuse Lowassa wanayemtuhumu kuiba mabilioni.

Karibu Lowassa, karibu Mzee, karibu uongoze nchi yetu tupo tayari.
 
Hapa kuna harufu ya rushwa siyo rahisi kupokea kinyesi hiki mbele ya chakula!!
 
ukawa ndo habari ya mjini, kila kona ukawa
 
Kalitaka hata kumuua mwakyembe wetu. Nenda baba....
 
Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA


Wewe ndie unakurupuka na kuropoka sio TL!! Man you have put your brain; if you have any into gear B4 you start rambling with your keypad! hivi unakwepaje kufahamu au unajitoa akili tu kwamba Dr Slaa mwenyewe ni sehemu ya vikao vilivyofanya uamuzi huo! this far we have not heard a single dissenting word from him; kama hakuridhika na kuridhia maamuzi makubwa kama hayo wakati yeye ndiye chief executive wa CDM na mdau mkubwa kabisa wa UKAWA; kwa nini hajajitoa CDM kama alivyowahi kujitoa CCM way back in 1995!!?? A man of Dr Slaa's calibre sio mtu wa kuburuzwa buruzwa hovyo!

Man think out of the box!!
 
Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:EdwardLowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawishana kulinda ufisadi.??Sisi Chadema na UKAWA tumeamuakuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchimtuelewe na kutuunga mkono.
 
Ninawaunga mkono, ninawaamini maana nyie ndo viongozi wetu mlioko site mmepima na mkaona hiyo ndiyo njia sahihi. Tuko tayari kusikiliza maagizo ya viongozi wa Ukawa/CDM na kuyafuata kikamilifu katika kipindi hiki muhimu kwa taifa letu.

Hakika ukombozi uko mlangoni.

Mungu Ibarika Tanzania, Mungu Ibariki Ukawa/ CDM.

Tutafika tu, tusipozimia roho
 
Ccm mwaka huu watataga na watajutia maamuzi yao yakumteua john alcohol padlock pale dodoma
 
Sijawahi kuona unafiki wa kisiasa kama hivi sasa. Ndg EL alikuwa anapondwa,anakashifiwa, anadhalilishwa na kufedheheshwa sana na viongozi wakuu wote wa upinzani hasa CDM. Na wakatamka kuwa hawatopokea masaza toka ccm, hivi leo wanafanya nini?

Hisia zangu ni kuwa ukawa dhamira yako kubwa hasa ni kuwa na viti vingi katika bunge lijalo na kwa kumtumia EL ni mahesabu mazuri tu na uwezekano wa kushinda urais kimahesabu utakuwa ' too close to call' lakini mwisho wa siku washindwa wa politiking watakuwa ccm wametengeneza matatiza ambayo hayakupaswa kuwepo na kwa masikitiko makubwa ninaweza kusema kuwa imetokana na udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho.

Ninaweza kwenda mbali zaidi kwa kufikiri kuwa ingawa chama hicho kina think tank wengi lakini inaelekea aidha kuna makundi au pengine wanabaguana. Hivi kweli inawezekana Nape Nnauye akapewa nafasi aliyonayo kutokana na uwezo kweli? mimi siyo mwana siasa lakini ninauhakika ningekuwa kwenye nafasi yake kuna mambo na kauli nyingi nisingezitoa.

EL kama kutolewa basi angetolewa kwa taratibu za chama hicho nazo ni pamoja na kuhoji waombaji wote, kujibu tuhuma kama zipo halafu wao kama wagombea SP ipi ambayo inaweza kukipeleka chama juu n.k.

Uhakika wa kura kwa upande wa kanda ya ziwa ni zaidi ya asilimia 80 [nao wanataka rais atoke kwao. Kanda ya kaskazini ni kazi kweli kweli na maeneo mengine ni hivyo hivyo.

KAMA CCM IKISHINDWA KWENYE UCHAGUZI WA MWAKA HUU JK HATOKWEPA KUWA YEYE NDIYO CHANZO CHA KUSHINDWA HUKO[ ndugu zangu haya ni mawazo yangu tu]
 
Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA
Duh! Siasa Bwana yaani leo wewe ni mtetezi wa Dr. Slaa??? CCM is safe with Lowassa outside, it is extremely risky with him in; so cool down.
 
Uzuri wa siasa ndio huu.. huwa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu... hivyo ccm watakua wanajidanganya sana kama watakaa na kubweteka kuwa EL kuhamia ukawa sio tishio kwao...
 
Politics are sometimes like soccer, no opponents in soccer for life
 
Ni neno ccm or? unamansha nn by ccm. cdm hamna jipya nlikuwa nawaunga mkono ss nawashusha to negativu. tamaa hzo mbaya mnakuwa km demu malaya bwana!
 
Lissu katika uborawake wa kukurupuka na kuropoka....
Mmemdhalilisha sana Dr Slaa amepambana na mafisadi hata kuweka maishayake hatarini..leo manasema mtu aliyemtaja kama fisadi anafaa zaidiyake...
Lowassa ataishia kuwa rais wa UKAWA

Ngoma ya UKAWA ww wa lumumba inakuhusu nn mkuu subili october ndio utajua hii ndio kete ya kuwauwa wote pale Lumumba na vibaraka wenu
 

Attachments

  • 1438083144007.jpg
    1438083144007.jpg
    13.3 KB · Views: 195
Back
Top Bottom