Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA

Elections 2015 Tundu Lissu: Edward Lowassa ndiye mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA



lissu.jpgKwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa hapo chni

"Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.
Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono"


hayo ndiyo majibu ya Lissu, lete maoni yako




 
I concur with his clarification, 100%

Lowassa karibu katika jeshi la ukombozi tumekusamehe tupambane pamoja



5
 
Very much understood
I have nothing to add....I am just on my way to register for the voting process.
I have to vote this year ....hakuna jinsi nyingine.
 
Wana jamii hii nimeikuta kwa makada kadhaa wa CCM walikuwa wakijadiri kuwa iwapo UKAWA watampendekeza LOWASA agombee urais kupitia UKAWA, basi itakuwa ndiyo mwisho wa mgombea huyo.

CCM ina mkakati wa kuwatumia watu nje ya CCM kumwekea pingamizi mahakamani kwaani ushahidi wa ufisadi wake wote upo mezani ikulu na usalama wa taifa.

TAHADHARI:
Iwapo atazuiwa na mahakama je wafuasi wake watakubari?
 
Hapo mkuu Tundu Lissu Tumekusoma ,Tumekuelewa , Adui yetu ni System ya CCM ,is not and Individual Thanks for Clarification.
 
Nenda kasome katiba, mtu ambae haruhusiwi kugombea uongozi... mtahangaika sana mwaka huuu... Lowassa ndio kashatinga ikulu
 
Acha kukimbia kimbia na maneno ya mtaani...nchi inaongozwa kwa katiba na sheria.
 
Kwa mizengwe ya CCM inawezekana kabisa siwezi kushangaa maana wakifikiria hii nyomi ya Ukawa wanatetemekajee.
 
100% nakubaliana na Lissu!! adui no 1 ni CCM na mfumo tawala!!
 
Hapo mkuu Tundu Lissu Tumekusoma ,Tumekuelewa , Adui yetu ni System ya CCM ,is not and Individual Thanks for Clarification.
Wapuuzi watupu !hatuna imani nanyi tena shida yenu ni uchu wa madaraka Hanna lolote , nkishindwa mtatuambia mini nyote mafisadi.
Karibu Magufuli tegemeo letu
 
Huu ufafanuzi wa Lisu nimeusoma kwenye ukurasa wake wa facebook ukanikonga nyoyo.Nakushukuru sana mleta uzi kwa kuuleta huu ufafanuzi kipande hii ya JF.Bila shaka ufafanuzi una viwango vya kutosha kabisaaa
 
Kamanda UKAWA kuna ufisadi huko nawaachia nyie makamanda.

Hahaha Ritz bwana,mbona huko wamebaki wengi mpaka Mwenyekiti wa Chama Chetu Cha Majangili pia wamo?

Tuamue kuanzisha chama chetu tu ambacho kwa uhakika kitapiga vita RUSHWA na UFISADI bila kuangalia sura ya mtu.
 
You are very right Lissu. This is an excellent philosophical answer on how to solve a dilemma which says "the best way to solve a dilemma is to choose the least evil". Kwenye dini wanasema hakuna dhambi ndogo lakini kidunia kuchinja mtu ni zaidi kuliko kuiba sindano ya mtu. Ukilinganisha ubaya wa mfumo wa ccm na ubaya wa Lowassa kwa wananchi ni tofauti by far.
 
I concur with his clarification, 100%

Lowassa karibu katika jeshi la ukombozi tumekusamehe tupambane pamoja



5

Nafikiri kisiasa CDM inatakiwa kumtaka radhi EL kwa kuwa ukweli umewekwa wazi. Wanaujua ukweli na hivyo kuendelea kuongelea jambo la ufisadi wake si sawa kwa kuwa si fisadi na mafisadi wanajulikana sasa. Fisadi hawezi kukana ufisadi wake ikiwa mfano kubadilisha itikadi. Hii itakuwa kukata mti umekalia tawi hilo hilo. Kuhama tu ni ishara kuwa mchafua CV ndio fisadi et al. Acha yamfike. Magereza hawakurekebisha hasa lile la maweni nafikiri ndio liwe la mafisadi soon 2016 na bila maboresho; kazi ngumu pamoja na kufilisiwa.
 
Back
Top Bottom