Hiyo uliyotoa siyo hoja! Tangu lini "udhaifu" au "madhaifu" yakawa ndiyo "siri" za chama? Siri za chama ni mbinu au mikakati chama kilichonayo kwa ajili ya ushindani wa kisiasa, na ambayo inasubiri muda muafaka ndipo iwe hadharani. Sasa hii ndiyo ikianikwa kabla, kinyume na utaratibu wa chama, huko ndiko kuvunisha ziri za chama. Hakuna chama madhubuti kinachojivunia maovu au tuhuma za rushwa au ubadhilifu wa fedha kama siri zake. Hata katika familia maovu kama kuchepuka (kuvunja uaminifu wa ndoa), kumnyanyasa mke/mume/mtoto hakuwezi kuwa siri ya familia. Siri ya familia ni mipango mizuri ambayo familia inayo kwa ajili ya kujiletea maendeleo, ambayo kama itatolewa kwa watu wengine kabla ya muda wake, familia inaweza kuhujumiwa katika mipango yake. Hii ndiyo inaweza kuwa siri ya familia.