Tundu Lissu: Haikuwa rahisi kwangu kuamua kugombea Uenyekiti

Tundu Lissu: Haikuwa rahisi kwangu kuamua kugombea Uenyekiti

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu, akizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi Desemba 12, 2024, Mlimani City, Dar es Salaam, ameeleza azma yake ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

"Haikuwa rahisi kwangu kufikia uamuzi wa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama chetu. Tangu mwaka 2015 vishawishi vya kunitaka kugombea nafasi hiyo vilipoanza hadi miezi michache iliyopita, nimesema mara kwa mara, hadharani na faraghani, kwamba siko tayari kugombea nafasi hiyo.

Ili kuondoa mashaka yoyote juu ya msimamo wangu huo, tarehe 6 Agosti ya mwaka huu niliwasilisha rasmi kusudio langu la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo nimeitumikia tangu Uchaguzi Mkuu wa chama uliopita wa mwaka 2019.

Kwa vyovyote vile, kubadili msimamo wangu unaojulikana wazi na kwa muda mrefu kunadai majibu ya swali la kwa nini? Swali hili ni halali na halina budi kujibiwa kwa ukweli na kwa ufasaha. Nitajaribu kufanya hivyo kwa kadri ya uwezo wangu," alisema Lissu.

Snapinsta.app_469723505_2159849274408700_3846363846632503584_n_1080.jpg
Pia, Soma: Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA
 
"KUGOMBEA" neno muhimu ieleweke hivyo.

Ni muhimu sana hizi nafasi zipate ushindani, hakuna mmiriki wala hatupaswi kuogopa au kutishwa kugombea nafasi yoyote nchini, hilo ni takwa la demokrasia na haki.

Ni utamaduni mzuri sana, tujaribu kuutetea na kuuendeleza, siyo chadema tu hata ccm.
 
..mambo mengi yanayobishaniwa kwenye mitandao kuhusu uchaguzi wa mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu ameyajibu ktk hotuba yake, au kupitia majibu kwa maswali aliyoulizwa na wanahabari.
 
Back
Top Bottom