Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati

Mkuu kwanza nikiri me sio mwanasheria (kitaaluma) ila kwa vifungu ulivyo ambatanisha nnacho jaribu kuelewa ni kuwa kampeni (kwa mujibu wa tume) inaanza tar 26/08 na kumalizika 27/10.

Hivyo basi haya yote yanayofanyika sasa (kutafuta wadhamini) hayana sifa ya kuitwa kampeni kwa kuwa yapo nje ya hiyo schedule ya tume. Ndio maana Lissu anayafananisha na siasa alizokuwa akizifanya Magufuli tangu 2015 na ndio maana anasema kwenye sheria za uchaguzi hakuna kitu kinaitwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
 
nadhani hujasoma maana ya kampeini kama wao walivyoindaika kwenye sheria ya uchaguzi sura 343; ile sheria ina kurasa 106
 
Lissu bora wangeaacha tu aendelee na harakati za kisheria lakini kumuweka kwenye hiyo nafasi apambane na Magufuli ni kupoteza muda.
Kinyume chake ndiyo kweli. Jiwe kwa miaka yote amekuwa akisema yy siyo mwanasiasa. Na ndiyo maana anahaha. Wapambe wake kama wewe jasho linawatoka mpk sehemu nyeti
 
Namhurumia sana Lissu kwa vile amepitia trauma kubwa sana ya kimwili kwa kushambuliwa ila sasa anaweza kujikuta anaingia kwenye trauma nyingine ya kisaikolojia kwa kushindwa uchaguzi katika mazingira ya kukejeliwa. Nadhani hakupata mshauri mzuri wa kisiasa, angeweza yeye kuwa kujiweka katika position ya kingmaker akiwa pembeni na huenda akiwa anatengeza mazingira mazuri ya kisiasa mbeleni. Ila sasa yeye ni mtu wa aina yake; ngoja tusubiri 28-10
 
nadhani hujasoma maana ya kampeini kama wao walivyoindaika kwenye sheria ya uchaguzi sura 343; ile sheria ina kurasa 106
Ni kweli sijaisoma na kama nilivyokiri pale awali me si mtaalamu wa sheria ila nilikuwa najibu kutokana na vifungu ulivyo ambatanisha kupinga hoja ya Lissu.

By the way, kwenye hiyo sheria kuna kitu inaitwa 'kuanza kampeni kabla ya wakati?'

Kwa uelewa wangu mdogo wa mambo ya sheria nafahamu kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo sheria imekaa kimya (haijayazungumzia), mambo hayo huwa hayawi regarded kama ni makosa.

Nadhani huwa wanaangalia merit kwenye maamuzi na mara nyingi hujitokeza kama case within a case ila huwezi kuyafungulia mashtaka ya msingi sababu hayana locus stand. Dah field za watu hizi ila humu kuna wajuvi zaidi watatusaidia.
 
Mkuu unanikosea heshima! Nilishasema kwa Tanzania mtu mwenye IQ kubwa wa kwanza ni mimi, kisha ndo anafuata Lissu, wa mwisho kabisa kwa TZ ni dikteta Magu, hata tafiti zinaonesha hivyo
[emoji23][emoji23][emoji23] naona unamtafuta Meko!!
 
Huyo ni mkuu wa nchi Lissu huwezi kujifananisha naye, ndiyo maana ataendelea kuwa rais hadi rais mteule mwingine atakapoapishwa. Hivi huyu Lissu sheria amesema wapi??? Magufuli anatembea nakofia mbili yeye lissu hana kofia ya pili, asubiri tu KUKATWA kwani kafanya kampeni akiwa na akili timamu
 
Asante sana; sheria ile ina mambo mengi, lakini yale yanayowabana wagombea kuhusu kampeini yapo mawili tu. Moja ni kile kifungu kinachosema maana ya kampeini, halafu kingine kinatawala uratibu wa kampeini. Nikipata nafasi nitakuwekea hapa uvisome mwenyewe ila hata wewe unaweza kuvitafuta kutoka tovuti ya tume ya uchaguzi. Vifungu hivyo ndivyo vinavyofanya wanasiasa wawe makini katika kujiandaa na kampeini hizo.
 
Magufuli ataendelea kuwa rais na diyo maana anaendelea kutoa maelekezo ya kiserikali si ya kichama, 2015 JK aliwahi kuteua DC siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu. Chadema majanga makubwa, ndiyo maana mlinajisi wimbo wa Taifa kwa kigezo tuone watatufanya nini
 
Asante mkuu Kichuguu, ila nitashukuru sana kama utaweza kupaste hapa kwa manufaa ya wengine pia kujielimisha.
[emoji120][emoji120]
 
Kampeni kabla ya uteuzi iko kisheria .Sasa unafanyaje kampeni ya Uraisi wakati hata uteuzi wa NEC haujafanyika!!! Lisu haelewi nini
 
Eh na matusi tena?
 
Tumepata Mtu Ni yeye!! Haogopi kusema ukweli ,hapepesi macho ,blue ni blue ,black ni black! Jiwe anafanya kampeni na kugawa rushwa waziwazi.
 
Kampeni kabla ya uteuzi iko kisheria .Sasa unafanyaje kampeni ya Uraisi wakati hata uteuzi wa NEC haujafanyika!!! Lisu haelewi nini
Jiwe ndio anafanya kampeni sana au haujasikiaalivyosema kwenye mikutano yake aongeweze miaka mi5 amalizie viporo alivyoacha?
 
Kampeni kabla ya uteuzi iko kisheria .Sasa unafanyaje kampeni ya Uraisi wakati hata uteuzi wa NEC haujafanyika!!! Lisu haelewi nini
Umetumia lugha nyepesi kabisa nadhani kila mmoja humu ataelewa, acha na mimi nikope ufahamu wako kwa kusema, ni sawa na mtahiniwa wa form six kuanza kujaza form za kuingia chuo kikuu kabla ya matokea ya mtihani kutolewa na NECTA.
Mh. Kikwete aliwahi kusema "kuwa ufahamu wa Lissu wa sheria unamchanganya yeye mwenyewe na pia huwachanganya hatu wafuasi wake'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…