Inabidi kuwa makini na hizo haki. Magufuli akiagize viongozi kukamilisha ujenzi wa mradi wowote, anaweza kuonekana anapiga kampeini, lakini siyo kweli atakeleza majukumu yake ya uraisi. Akiahidi kuwa serikali itafanya jambo fulani, bado ni mojawapo ya majukumu yake kama kiongozi wa serikali. Anaposema kuwa Mbunge fulani hakuleta matatizo ya jimbo lake serikalini kushghulikiwa ndiyo maana jimbo hilo halikuudumiwa kwa vile matatizo yake yalikuwa hayajulikani serikalini, bado ni sehemu ya kazi zake za uraisi. Kwa hiyo ukichambua sana utaona kuwa kuna mambo machache sana ambayo hawezi kuyasema kama raisi. Kubwa asiloruhusiwa ni kutumia majina ya chellengers wake kwenye mikutano yake ya kikazi kwa kuwaponda.