Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati

Watu wanasema nafanya kampeni mapema. Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini, inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati. Na kama wakisema hii ni kampeni kabla ya wakati, basi wasisahau kuwa Rais Magufuli amekuwa anafanya kampeni kwa miaka mi5 sasa.
Na Hilo tulikusea tunawambia wakwa wanasema wao ndio watawala na kejeli nyingi tu .
 
Anachofanya lisu ni kubinya tu kende, ili akili iwakae sawa, unataka amtaje kibajaj, musiba,polepole na wapiga domo wengine wa nzi wa kijani? Hao sio size yake

Harafu kwa nn mnaogopa jina lake lisitajwe kama mnaona sio mvumilivu mtoeni kwenye kinyag'anyiro cha kuomba urais muweke atakayeweza ebo!
 
Huyu sijui anazungumza sheria za nchi gani kwani sheria za Tanzania ziko wazi sana kuhusu jambo hili. Kuna sheria ya Uchaguzi CAP 343 ya mwaka 2015, sheria ya matumizi ya Uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010, pamoja na taarifa ya kawaida namba 722 kwenye Gazeti la serikali toleo la 23 la tarehe 5 June 2020. maandiko yote hayo yanasisitiza kuwa kampeini zinafanyika zikiwa zimeratibiwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa vile tume imeshasema kuwa kampeini zitaanza tahere 26 August, mtu yeyote anayefanya kampeini kabla ya wakati huo anavunja sheria. Maandiko hayo pia yameeleza maana ya kampeini ni nini.

View attachment 1536520

View attachment 1536519

View attachment 1536517

Mkuu kwanza ungetuambia kampeni ni nini? Anachokifanya Lisu ni kutafuta wadhamini na hayo anayoyaongea ni maneno ya kawaida ya siasa. Huwezi kusema anafanya kampeni wakati kwa mujibu wa sheria kampeni zinaanza tarehe 26 August. Hapo kipengele C ya hiyo sheria inazungumzia taratibu wakati wa kampeni ndiyo maana hata hizi shughuli za sasa unazodhani ni kampeni zinaenda hadi usiku na polisi hawaingilii kwasababu si kampeni. Hakuna sheria tanzania inayokataza watu kufanya shughuli za siasa nchini wala maandamano ndiyo maana kila anayechukua fomu anapokelewa kwa maandamano, utaratibu hapo juu ni kwa wakati wa uchaguzi tu. Ukitaka kusema TL ameanza kampeni mapema atakuuliza sheria inayokataza haya anayoyafanya sasa hivi kama hamna basi si kmapeni ni shughuli za kawaida. Kampeni zitakapoanza hata mikutano itakuwa inaisha saa 12 jioni na zaidi ya hapo itakuwa ni kwenda kinyume cha sheria.

Mfano Rais Magufuli kasema anataka miaka mingine 5 kumaliza miradi yake akiwa mbele za watu ile si kampeni, Membe kasema akiapishwa tu wafungwa wa kizanzibari watarudishwa kwao siyo kampeni na yeyote atakayesema chochote kwasasa si kampeni maana kampeni zinaanza tarehe 26 August. Mfano kama kufunga ramadhani inaanza tarehe 26 august mtu akianza kufunga tarehe 1 august hawezi kasema anafunga ramadhani.
 
Asante mkuu Kichuguu, ila nitashukuru sana kama utaweza kupaste hapa kwa manufaa ya wengine pia kujielimisha.
[emoji120][emoji120]
Asante; nitaweka vifungu hivyo pole pole, usivikopi kabla sijaweza kuviweka vyote; nina kazi nyingine zitakazonichelewesha kuvitafuta vyote harakaharaka. Cha kwanza za ni hiki
1597389919698.png

Hiki kinasema Campaign inaaaza baada ya wagombea kuwa nominated na tume. Kipindi cha kutafuta wadhamini siyo cha kampeini kama mtu anatumia kipindi hicho kuongea na prospective wadhamini tu. Akishaanza kuongea na wapiga kura wote katika kutafuta udhamini kabla hajawa nominated, anakuwa anakiuka maana ya campaign period. Nitaleta vingine pole pole; sheria huwa hazisomwi kama novel bali ni muunganiko wa mambo mengi na nitajitahidi kuyaleta yote.
 
Asante; nitaweka vifungu hivyo pole pole, usivikopi kabla sijaweza kucviweka yote; nina kazi nyingine zitakazonichelewesha kuvitafuta vyorte harakaharaka. Cha kwanza za ni hiki

View attachment 1536760
Hiki kinasema Campaign inaaaza baada ya wagombea kuwa nominated na tume. Kipindi cha kutafuta wadhamini siyo cha kampeini kama mtu anatumia kipindi hicho kuongea na prospective wadhamini tu. Akishaanza kuongea na wapiga kura wote katika kutafuta udhamini kabla hajawa nominated, anakuwa anakiuika maana ya campaini period. Nitaleta vingine pole pole; sheria huwa hazisomwi kama novel bali ni muunganiko wa mambo mengi na nitajitahidi kuyaleta yote.
Tunajaribu kuwafahamisha hawa jamaa wabishi sana, ila mwisho wao umefika kama wanategemea ubeligiji itaongea na sisi tutaongea kama taifa huru na wala hatuingiliwi uhuru wetu kama taifa, wavunja sheria lazima waadabishwe
 
Unfortunately unatafsiri sheria ile kimakosa.
Nani sasa anatasfiri? MATAGA si ndio wanasema kwamba lissu ashaanza kufanya kampeni? Lissu ndio kawajibu kwamba kama kufanya kampeni kabla ya muda basi Magufuli ndio anafanya tena zaidi ya miaka mi5 na hapa juzi juzi ameanza kutoa rushwa kila anapopita.
 
Hasira hasara.

Nimejibu swali hili huko nyuma kuwa Magufuli ni Rais wa Tanzania mpaka atakapoapishwa rais mwingine, kwa hiyo yeye kuwa mgombea haimzuii kuwa rais. Ataendelea kufanya kazi za uraisi ingawa zinawea kutafsiriwa kuwa ni kampeini. Ukirudi nyuma utakuta nilipoongelea hilo. Kuna mambo machache sana anayozuiwa wakati wale challengers wake wanazuiwa mambo mengi sana; inaitwa power of incumbancy.
 
Watu wanasema nafanya kampeni mapema. Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini, inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati. Na kama wakisema hii ni kampeni kabla ya wakati, basi wasisahau kuwa Rais Magufuli amekuwa anafanya kampeni kwa miaka mi5 sasa.
Sehemu ambayo Tundu Lisu anawaumiza kichwa maccm ni hapo kufanya mambo ambayo hayakatazwi na sheria za nchi yetu isipokuwa taratibu za maccm.
 
Sasa atapambanaje na mtu bila kumtaja kwenye Siasa mnataka kumpangia cha kusema ati bora kule sijui nini kama humuelewi si utamnyima tu kura unamia nini wengine wanapenda hivo anavofanya na watamchagua.
Aliyesema wapinzani wakipewa nchi watauza vyuma vya madaraja ni nani yule ?
 
Huyu sijui anazungumza sheria za nchi gani kwani sheria za Tanzania ziko wazi sana kuhusu jambo hili. Kuna sheria ya Uchaguzi CAP 343 ya mwaka 2015, sheria ya matumizi ya Uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010, pamoja na taarifa ya kawaida namba 722 kwenye Gazeti la serikali toleo la 23 la tarehe 5 June 2020. maandiko yote hayo yanasisitiza kuwa kampeini zinafanyika zikiwa zimeratibiwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa vile tume imeshasema kuwa kampeini zitaanza tahere 26 August, mtu yeyote anayefanya kampeini kabla ya wakati huo anavunja sheria. Maandiko hayo pia yameeleza maana ya kampeini ni nini.

View attachment 1536520

View attachment 1536519

View attachment 1536517
Huyu lissu ni tatizo sababa anajifanya anajua sheria kuliko mtu yeyote Tanzania.
Tofauti yake na Magufuli mwenzake ni rais, ana utetezi kuwa anafanya haya mambo kama rais lakini yeye hata tume haijampitisha anataka kujilinganisha naye.
Pia pamoja na kwamba ni mwanasheria lakini kwa makusudi amekuwa akidharau mahakama, mara ya kwanza pamoja na kutotokea mahakamani alikuwa akizunguka ulaya akidai bado anaumwa.
Mara ya pili pamoja na kurudi hakutokea mahakamani kwa kisingizio amejiweka karantini lakini kesho yake alionekana kwenye mikutano ya chama chake akiomba kura ya kuwania urais wa Tanzania.
Jana hakuonekana mahakamani kwa kisingizio cha kutafuta wadhamini.
Ni wazi anatafuta sababu mahakama imwadhibu ili apate kura za huruma au kuna kitu ametumwa akilete nchi hii.
Kama ameanza kudharau mahakama tena akiwa mwanasheria ni wazi yeye ni mbaya zaidi ya Magufuli.
 
Asante; nitaweka vifungu hivyo pole pole, usivikopi kabla sijaweza kucviweka yote; nina kazi nyingine zitakazonichelewesha kuvitafuta vyorte harakaharaka. Cha kwanza za ni hiki

View attachment 1536760
Hiki kinasema Campaign inaaaza baada ya wagombea kuwa nominated na tume. Kipindi cha kutafuta wadhamini siyo cha kampeini kama mtu anatumia kipindi hicho kuongea na prospective wadhamini tu. Akishaanza kuongea na wapiga kura wote katika kutafuta udhamini kabla hajawa nominated, anakuwa anakiuika maana ya campaini period. Nitaleta vingine pole pole; sheria huwa hazisomwi kama novel bali ni muunganiko wa mambo mengi na nitajitahidi kuyaleta yote.

Asante mkuu, ila hapo tuzungumzie kwenye 'nomination'.

Maana ya kuwa nominated ni kuwa umeteuliwa na tume kuwa mgombea wa nafasi husika baada ya kutimiza matakwa mengine ikiwemo wadhamini.

Na ukisoma pia vile vipengele vingine vinasema uteuzi wa tume utafanyika tar 25/08 na kampeni zitaanza tar 26/08 (siku 1 baada ya uteuzi wa tume). Kwa muktadha huo (kwa tafsiri yangu) mtu anaweza kuhesabika kuwa amefanya kampeni kabla ya muda ikiwa tu,

1. Ameteuliwa na tume kuwa mgombea wa nafasi aliyoomba kuteuliwa yaani tar 25 kwa mujibu wa tume na pia

2. Akaanza kampeni kabla ya muda uliowekwa na tume yaani kabla tar 26/08.

Kwa maana hiyo ili mtu atende kosa hilo atatakiwa kufanya kampeni tar 25/08 baada ya kuteuliwa.

Kwenye tafsiri ya sheria vifungu huwa vinasomwa kwa pamoja ili kuleta maana na sio kimoja kimoja.

Kwa muktadha huo technically ni vigumu sana mtu kitenda kosa hilo.
 
Hasira hasara.

Nimejibu swali hili huko nyuma kuwa Magufuli ni Rais wa Tanzania mpaka atakapoapishwa rais mwingine, kwa hiyo yeye kuwa mgombea haimzuii kuwa rais. Ataendelea kufanya kazi za uraisi ingawa zinawea kutafsiriwa kuwa ni kampeini. Ukirudi nyuma utakuta nilipoongelea hilo. Kuna mambo machache sana anayozuiwa wakati wale challengers wake wanazuiwa mambo mengi sana; inaitwa power of incumbancy.
Kwasasa JPM ni Mgombea urais anapoenda Dodoma kuchukua form au kutafuta wadhamini anaenda kama mgombea na sio rais,jaribu kutofautisha kazi za Rais na mwenyekiti wa CCM ,Alivyoenda Lupaso alienda kama Rais.

Ndio maana tunataka katiba mpya kuondoa hayo makando kando(Loop holes) kufanya kampeni kwa kujifanya eti ni rais na sio mgombea.
 
Asante mkuu, ila hapo tuzungumzie kwenye 'nomination'.

Maana ya kuwa nominated ni kuwa umeteuliwa na tume kuwa mgombea wa nafasi husika baada ya kutimiza matakwa mengine ikiwemo wadhamini.

Na ukisoma pia vile vipengele vingine vinasema uteuzi wa tume utafanyika tar 25/08 na kampeni zitaanza tar 26/08 (siku 1 baada ya uteuzi wa tume). Kwa muktadha huo (kwa tafsiri yangu) mtu anaweza kuhesabika kuwa amefanya kampeni kabla ya muda ikiwa tu,

1. Ameteuliwa na tume kuwa mgombea wa nafasi aliyoomba kuteuliwa yaani tar 25 kwa mujibu wa tume na pia

2. Akaanza kampeni kabla ya muda uliowekwa na tume yaani kabla tar 26/08.

Kwa maana hiyo ili mtu atende kosa hilo atatakiwa kufanya kampeni tar 25/08 baada ya kuteuliwa.

Kwenye tafsiri ya sheria vifungu huwa vinasomwa kwa pamoja ili kuleta maana na sio kimoja kimoja.

Kwa muktadha huo technically ni vigumu sana mtu kitenda kosa hilo.
Shukrani sana mkuu kwa kutoa elimu ndio maana lissu amesema hakuna kosa lolote kisheria amekosea kama basi amekosea basi JPM amekosea kwa muda wa miaka karibu mi5.
 
Watu wanasema nafanya kampeni mapema. Hakuna tafsiri yoyote ya kisheria nchini, inayosema kuna kitu kinaitwa kampeni kabla ya wakati. Na kama wakisema hii ni kampeni kabla ya wakati, basi wasisahau kuwa Rais Magufuli amekuwa anafanya kampeni kwa miaka mi5 sasa.
Idiot! Tatizo huwa Hakumbuki Jana Kasema nini
 
Kwasasa JPM ni Mgombea urais anapoenda Dodoma kuchukua form au kutafuta wadhamini anaenda kama mgombea na sio rais,jaribu kutofautisha kazi za Rais na mwenyekiti wa CCM ,Alivyoenda Lupaso alienda kama Rais.

Ndio maana tunataka katiba mpya kuondoa hayo makando kando(Loop holes) kufanya kampeni kwa kujifanya eti ni rais na sio mgombea.

Unajadili kwa hasira sana ila ii kuwa wakati Magufuli anaongea na wana CCM ndipo alikuwa anatafuta wadhamini kama mgombea ndani ya chama chake, hakukusanya mkutano wa hadhara kutafuta wadhamini. Kosa hili limeshafanyika sana Tanzania lakini ni kinyume cha sheria,

Alipokuwa anaongea na wanachi njiani kutoka Lupaso, alikuwa anaongea nao kama rais wa Tanzania, na ni sehemu ya amjukumu yake katika position hiyo. Hapo ndipo power of incumbency inambeba, na huwezi kuitengua kwa sababu yeye ni Magufuli jiwe. bali ataendeleakuwa Rais hadi October 30.
 
Hawa jamaa huwa wanapenda kumbeza Lissu kwa kila kitu kwa sababu za kisiasa, ila bro trust me...ni vigumu sana kumpata Lissu na hatia tena kwa makosa ya jinai, sababu sheria ameifanya kuwa sehemu ya maisha yake na ana slogan yake anasemaga, 'namna nzuri ya kutii sheria mbovu ni kuzivunja'.

Ndio maana wamembambika kesi nyingi sana na hawajafanikiwa kumpata na hatia so far. Kitu kingine, watanzania wengi hatuna uelewa wa sheria na mienenendo ya kesi mahakamani hadi kumpata mtu na hatia si mchezo.

Hata wengi wamefungwa sababu hawana wasaidizi wa sheria, nadhani pia ulimskia Lissu kule Nyamongo alitoa vifungoni watu zaidi ya 400 waliokuwa wamefungwa kinyume na sheria, imagine watu 400 ni kijiji kizima kipo jela kinyume na sheria ama sababu ya uonevu au maelekezo toka juu.
Shukrani sana mkuu kwa kutoa elimu ndio maana lissu amesema hakuna kosa lolote kisheria amekosea kama basi amekosea basi JPM amekosea kwa muda wa miaka karibu mi5.
 
Back
Top Bottom