Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hana sifa za kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hana sifa za kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Uzee co kigezo cha kukosa uongozi ,kwa saiv naona majaliwa ndio anafaa awe rais kama nikitumia vigezo vyako,magufuli nooo ,kwa uliosema tundu lisu hafai ,
kuna umri ukifika huwezi kuwa na nafasi nzuri ya kuongoza unakumbuka Mugabe yaliyomkuta na huwezi kumfananisha Ahmed .Lowassa na Umri wa Magufuli hao wawili kwasasa wamefika umri ambao wanahitaji kupumzika si misukosuko ya huko na kule kwenye nchi zetu masikini hizi ambazo zinahitaji misuli kuongoza maana unakuta zaidi ya asilimia 50 ya wananchi elimu zao ni za kawaida sana.Na ndiyo maana Mwl Nyerere alitumia muda mrefu sana kutoa hotuba kwa wananchi za kuelimisha kama mwalimu Rais ili wananchi waelewa maana uraia wao,uhuru wao jinsi ya kujitegemea na faida zake kuanzisha madara ya kufuta ujinge ili watu wajue kusoma na kuandika ilikuwa ni kazi ngumu sana aliifanya na ndiyo maana mpaka leo kuna maneno ya mwalimu hayaiishi vinywani mwa watu na akilini mwao.
 
Uko sahihi, Lisu anafaa kuwa na MTU juu wa kumwambia cha kufanya, yupo sawa na Raia No. 1 utais hauhitaji watu wenye mihemuko

Sent using Jamii Forums mobile app
kaliba na hulka za kuzaliwa ni ngumu sana kuzibadili mpaka ushauri na mentorship ya muda mrefu sana ndo wanaoweza kubadilika.
 
Kwa presentation kama hii nani katika jumuiya ya academicians atakuheshimu! Watu wenye IQ hata ya wastani watakudharau! very shallow reasoning portrayed!
Asshole comment
 
kupitia kupigania haki za wananchi kwenye maeneo ya migodi ndipo nilipoanza kumfuatilia Tundu Lissu kuhusu jinsi alivyokuwa anajibizana na waandishi na wageni pale anapokuwa ktk vipindi kwenye TV na ndipo alipofika hata bungeni tabia yake ya majibizano na ubishi na kuonyesha dharau kwa wengine....kuhusu kupigania haki za wananchi kwenye migodi alikuwa yuko sawa kabisa wala hapo sijasema kuwa hakuwa sawa.naongea tabia zake na kiburi na kujiona kuwa yuko juu ya wengine na kuonyesha dharau ya wazi wazi kwa wengine.kisa tu anajua sheria tuna wanasheria wangapi tz na wana hekima na busara.Muone Wakili wa kujitegemea mtoto kutoka Ifakara Wakili Kibatara mbona ana busara sana hekima na Baba yake alikuwa Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa sasa ni marehemu lakini mtoto sheria anazijua sana tu na kesi nyingi huwa anashinda huko mahakani lakini ana heshima sana wenzake hata apale anapoona kuwa kuna kasoro kwa wenzake.

Sasa nadhani nimekuelewa vizuri zaidi.

"Tundu Lissu hafai kuwa Rais kwa sababu 'ana majivuno, dharau na kujiona yuko juu ya wengine, n.k.,

Na sio kwamba Tundu Lissu hafai kuwa Rais kwa sababu hana uwezo wa kuwa Rais.

Nadhani sifa hizo ulizompa zinajadilika na kamwe haziwezi kuwa ndio zinazomwondolea sifa ya kuwa Rais, maanake hata sasa tunaona Rais aliyepo anazo sifa hzo na mbaya zaidi ya hizo; lakini sijaona kwenye bandiko lako ukisema hafai kuwa Rais.

Sasa labda uwe unazo sababu nyingine za kumzuia Lissu kuwa Rais ambazo hujaziweka bayana hapa.
 
hata usipo quote bandika lakini boss wako hafai kuwa Rais ana mihemko kwa kila mahali

Ni wapi ilipoandikwa kwamba Kalamu1 ana boss aitwae Tundu Lissu?
Magufuli amefanya vizuri... yeye anajibu kwa kukebehi Mwamoyo Hamza wa VOA akawa anamshangaa tu kejeli zake alipomuuliza swali hilo.

Ulijuaje kuwa huo mtangazaji alikuwa 'akikebehi'? Huoni kuwa unaweka hisia zako ziwe zake?

Kwa michango kama huu uliouweka hapa kunijibu inakuonyesha usivyokuwa makini katika unayoyaandika.
 
Sasa nadhani nimekuelewa vizuri zaidi.

"Tundu Lissu hafai kuwa Rais kwa sababu 'ana majivuno, dharau na kujiona yuko juu ya wengine, n.k.,

Na sio kwamba Tundu Lissu hafai kuwa Rais kwa sababu hana uwezo wa kuwa Rais.

Nadhani sifa hizo ulizompa zinajadilika na kamwe haziwezi kuwa ndio zinazomwondolea sifa ya kuwa Rais, maanake hata sasa tunaona Rais aliyepo anazo sifa hzo na mbaya zaidi ya hizo; lakini sijaona kwenye bandiko lako ukisema hafai kuwa Rais.

Sasa labda uwe unazo sababu nyingine za kumzuia Lissu kuwa Rais ambazo hujaziweka bayana hapa.
Rais Magufuli hana hizo sifa kama unavyosema ila Rais Magufuli yeye hana mzaha pale linapokuja suala uwajibika na hana urafiki katika kuwajibika na hataki kabisa visingizio vya kutomaliza majukumu ya mtumishi bila sababu za msingi na hasa anachukia sana wanaofanya starehe na pesa au mali ya umma hilo alikuwa anachukia toka akiwa waziri na ni mkali sana kwenye uzembe wa mtu yoyote eneo lake la kazi na kamwe hapendi uwongo na hana mzaha kabisa hizo ni baadhi ya sifa zake lakini sio dharau na lugha za kebehi na majivuno na kujiona anajua kila kitu na kuwaona wenzake hawajui kama Tundu Lissu.Mimi ndiyo mtazamo wangu kwa huyu ndugu yangu hata kama ni msomi lakini ajue kuwa wapo wanaojua zaidi yake na wanaheshima na busara na kutokebehi wenzake.Mbona Zitto hana hayo pamoja na kuwa mpinzania anayesumbua serikali kweli kweli lakini kiburi wala dharau wala majivuno kabisa.
 
sio dharau na lugha za kebehi na majivuno na kujiona anajua kila kitu na kuwaona wenzake hawajui kama Tundu Lissu.

Nimekukumbusha mengi lakini hutaki kuyaelewa. Ngoja nikupe mfano mwingine wa mama wa watu, sijui DED au nani yule wa Kagera aliyeshindwa kukariri kiasi cha pesa za mradi na hapohapo akapoteza kazi!
Nikikwambia kwamba wewe huna uwezo wa kukariri namba kama alionao Rais Magufuli bila shaka utasema huna, lakini hapo hapo unataka kila mtu awe hivyo kwa mjibu wa bandiko lako hapo juu. Wewe hii kazi huiwezi.
Naendelea kukupima kiasi chako, hadi sasa ni F.
 
Nimsikia Mhe Tundu Lissu akiwa huko Uingereza kuwa akipata ridhaa ya watanzania na chama chake basi atagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Nimekuwa nikumuangalia Mhe Tundu Lissu alipokuwa mwanaharakati na mtetezi wa madhila waliyokuwa wanapata wananchi katika migodi mbalimbali huko kanda ya ziwa na baadaye kuwa mbunge wa Singida.

Akiwa mbunge katika Bunge la Jamhuri amekuwa ni mchangiaji wa mara nyingi sana na muuliza maswali sana na kuomba kuhusu utaratibu na muongozo wa spika mara kwa mara kiasi cha kusababisha hata kutolwa nje na spika pale anapokataa kutii kiti cha spika.

Nakumbuka hata wakati wa Bunge la Katiba hapo ndipo Mhe Lissu alikuwa mkali kama mbogo kwa baadhi ya taratibu alipoona kama vile zina malengo fulani ambayo hayakuwa na faida kwa baadhi ya makundi.

Kwa ujumla ukimuangalia Mhe Lissu na jinsi anavyochangia mada au hoja na maneno anayotumia kwenye public kiukweli sidhani kama anaweza kuwa sahihi kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.

Kwa mtazamo wangu mimi kiukweli nidhamu ya Tundu Lissu katika kuchangia mada au hoja kwa wenzake huwa kuna dharau kubwa sana anaonyesha kiasi cha kutoheshimu michango ya wenzake na kama ndivyo alivyo basi kiti cha uraisi sidhani kama ni size yake.
Hata Mandela aliitwa Gaidi,akafungwa miaka 27,
Lakini alikuja akawa Raisi,na anaheshimiwa duniani kote,Ndani kijani sasa HV,hakuna hata mmoja anayestahili hata kushika viatu vya Mandela au Nyerere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
please please
Huyu rafiki yako nimemwambia time and again kama hawezi kujibu post zangu bila matusi apite, apotezee, lakini kila nikiandika ananitukana , soma post yake hapo juu. I will not spare him! Wacha nifungiwe, I will opt for another ID, to tell the truth!
 
please jamani sisi ni watu wazima tuyaache hayo maneno ya mitaani.
Tatum huyu UCD anakera, kila nikiandika lazima anitukane, anajibu kwa lugha ya kuudhi na matusi. nitamtukana bila kujali the outcome!
 
Back
Top Bottom