Sasa nadhani nimekuelewa vizuri zaidi.
"Tundu Lissu hafai kuwa Rais kwa sababu 'ana majivuno, dharau na kujiona yuko juu ya wengine, n.k.,
Na sio kwamba Tundu Lissu hafai kuwa Rais kwa sababu hana uwezo wa kuwa Rais.
Nadhani sifa hizo ulizompa zinajadilika na kamwe haziwezi kuwa ndio zinazomwondolea sifa ya kuwa Rais, maanake hata sasa tunaona Rais aliyepo anazo sifa hzo na mbaya zaidi ya hizo; lakini sijaona kwenye bandiko lako ukisema hafai kuwa Rais.
Sasa labda uwe unazo sababu nyingine za kumzuia Lissu kuwa Rais ambazo hujaziweka bayana hapa.