Uchaguzi 2020 Tundu Lissu hana sifa za kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Nimsikia Mhe Tundu Lissu akiwa huko Uingereza kuwa akipata ridhaa ya watanzania na chama chake basi atagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Nimekuwa nikumuangalia Mhe Tundu Lissu alipokuwa mwanaharakati na mtetezi wa madhila waliyokuwa wanapata wananchi katika migodi mbalimbali huko kanda ya ziwa na baadaye kuwa mbunge wa Singida.

Akiwa mbunge katika Bunge la Jamhuri amekuwa ni mchangiaji wa mara nyingi sana na muuliza maswali sana na kuomba kuhusu utaratibu na muongozo wa spika mara kwa mara kiasi cha kusababisha hata kutolwa nje na spika pale anapokataa kutii kiti cha spika.

Nakumbuka hata wakati wa Bunge la Katiba hapo ndipo Mhe Lissu alikuwa mkali kama mbogo kwa baadhi ya taratibu alipoona kama vile zina malengo fulani ambayo hayakuwa na faida kwa baadhi ya makundi.

Kwa ujumla ukimuangalia Mhe Lissu na jinsi anavyochangia mada au hoja na maneno anayotumia kwenye public kiukweli sidhani kama anaweza kuwa sahihi kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.

Kwa mtazamo wangu mimi kiukweli nidhamu ya Tundu Lissu katika kuchangia mada au hoja kwa wenzake huwa kuna dharau kubwa sana anaonyesha kiasi cha kutoheshimu michango ya wenzake na kama ndivyo alivyo basi kiti cha uraisi sidhani kama ni size yake.
Na umuelezeaji anayewaita mawaziri wake wajinga na vilaza hadharani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama magufuli ameweza Lissu anashindwa nini? Kwa mtazamo wangu ukiachilia mbali ujinga wetu wa kuona kikundi cha watu kinachoitwa ccm ndo Tanzania,Lissu is far better than Magufuli in term of competence
Mkuu kama huwezi changia hoja ni afadhali ukakaa kimya. Which competence do you mean, he does have? Wa kutoa grimace kama sokwe na kutoka povu wakati akizungumzua uongo wake?

Lissu amefanya nini katika dunia hii ambacho wewe unaona kuwa ana competence kubwa kuliko Magufuli? Unaijua historia ya Magufuli wewe mpaka ukaja na hoja za kifukara kama hizo? Hivi nikuulize wewe unaishi wapi?

Hii ndiyo kauli ya mtu kwenye competence kuliko Magufuli ya kuutangazia ulimwengu kuwa wasishirikiane na serikali ya Magufuli ili sisi tuzomewe? "Du hast einen Vogel!"

Issue ya makinikia jamaa anacopy na kupaste yale yale aliyoyasema Lissu pale bungeni licha ya mwanzo kumuita msaliti.ni uroho tu wa madaraka otherwise alitakiwa amuombe radhi.incompetence yake ilimtuma kutumia nguvu kuliko akili.la pili ni mahusiano yetu na nchi zilizokuwa marafiki zetu unavurugwa kwa sababu ya uwezo wake mdogo wa kushindwa kujua kipi kitamkwe hadharani na kipi kifanyike kisiri siri tu.interchange ya ubungo na barabara ya kimara kibaha ni mifano sahihi ya his incompentency.orodha ni ndefu
 
Sifa za kuwa rais ni zipi?,,,,huitaji kuwa special ili kuwa rais........watu mnakuza sana kile cheo
 
Mkuu kama huwezi changia hoja ni afadhali ukakaa kimya. Which competence do you mean, he does have? Wa kutoa grimace kama sokwe na kutoka povu wakati akizungumzua uongo wake?

Lissu amefanya nini katika dunia hii ambacho wewe unaona kuwa ana competence kubwa kuliko Magufuli? Unaijua historia ya Magufuli wewe mpaka ukaja na hoja za kifukara kama hizo? Hivi nikuulize wewe unaishi wapi?

Hii ndiyo kauli ya mtu kwenye competence kuliko Magufuli ya kuutangazia ulimwengu kuwa wasishirikiane na serikali ya Magufuli ili sisi tuzomewe? "Du hast einen Vogel!"

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni ujinga wako tu.kwani serikali ya magufuli ndo itakuwa ya kwanza kususiwa na dunia?kama hiyo serikali haifuati sheria au inanyanyasa watu wake sio tu inatakiwa isuziwe hata ikipidi kuondolewa madarakani kwa nguvu ni sahihi.Tanzania na watanzania ni wakubwa na muhimu kuliko magufuli na serikali yake wewe mfia tumbo
 
Huwezi kumlinganisha JPM na Lissu JPM ni jembe la uhakika katika kuhakikisha watu wanfauata sheria na kuwajibika.
Mkuu mimi nadhani inategemea unataka kuwalingamisha kwenye mambo gani,kwa mfano kama unataka kuwalinganisha kwenye matumizi ya nguvu nyingi kuliko akili,au ukataka kuwalingamisha kwenye kutenda kwa kutumia mihemuko kuliko sheria na utaratibu Magufuli is far better than Lissu,but kama unataka matumizi ya akili,sheria,free discussion kwenye mombo yanayotuhusu kama taifa,kama unahitaji muono wa mbali then Lissu is far better than magufuli.let me end here for now
 
Na umuelezeaji anayewaita mawaziri wake wajinga na vilaza hadharani?

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna mawazi wamekuwa vilaza na wajinga katika matendo yao ya kikazi kwa mujibu wa uwajibikaji wao.........wewe kuna mgomo wa biashara ya korosho Mtwara na unajua zao la korosho linavyosaidia kuingiza pato la taifa ...wewe waziri uko mkoani Kilimanjaro unafanya kazi za kawaida tu.....kwanini huo usiwe ujinga unaoufanya wakati wewe ni mwenye dhamana.tatizo tunataka kuheshimiwa kwa kila jambo kisa tu unacheo fulani.Tatizo la Lissu ni dharau na majivuno na kuonyesha kuwa anajua kila kitu hilo ndilo nalolizungumzia hapa kuliko wenzake na yeye ndiye aanayeonewa kwa kila jambo.....anaongolea kesi zake 8 za kisutu utafikiri hajafanya makosa kwa mujibu wa sheria.....kama akifanya kosa kwa mujibu wa sheria atakamatwa tu na kufikishwa mahakamani hata kama yeye ni mbunge au mwanasheria lakini anaitangazia dunia kuwa yeye anaonewa tu...watz wangapi wana kesi ktk mahakama zetu hapa nchini kwa makosa mbalimbali?....anatumia nafasi yake vibaya na hana lugha nzuri anapokuwa ktk mijadala na wenzake na dharau za waziwazi......anahitaji msaada wa kisaikolojia kwa tukio lililompata la kupigwa risasi.
 
Nimsikia Mhe Tundu Lissu akiwa huko Uingereza kuwa akipata ridhaa ya watanzania na chama chake basi atagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.

Nimekuwa nikumuangalia Mhe Tundu Lissu alipokuwa mwanaharakati na mtetezi wa madhila waliyokuwa wanapata wananchi katika migodi mbalimbali huko kanda ya ziwa na baadaye kuwa mbunge wa Singida.

Akiwa mbunge katika Bunge la Jamhuri amekuwa ni mchangiaji wa mara nyingi sana na muuliza maswali sana na kuomba kuhusu utaratibu na muongozo wa spika mara kwa mara kiasi cha kusababisha hata kutolwa nje na spika pale anapokataa kutii kiti cha spika.

Nakumbuka hata wakati wa Bunge la Katiba hapo ndipo Mhe Lissu alikuwa mkali kama mbogo kwa baadhi ya taratibu alipoona kama vile zina malengo fulani ambayo hayakuwa na faida kwa baadhi ya makundi.

Kwa ujumla ukimuangalia Mhe Lissu na jinsi anavyochangia mada au hoja na maneno anayotumia kwenye public kiukweli sidhani kama anaweza kuwa sahihi kuwa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.

Kwa mtazamo wangu mimi kiukweli nidhamu ya Tundu Lissu katika kuchangia mada au hoja kwa wenzake huwa kuna dharau kubwa sana anaonyesha kiasi cha kutoheshimu michango ya wenzake na kama ndivyo alivyo basi kiti cha uraisi sidhani kama ni size yake.
Kusema kwel umeongea kwa busara sana Leo na kwa hoja,,,ila Lisu nazan kazi yake ya uwakili pia inamfanya awe na kama zarau,,ila MTU mtulivu,msikivu,mwenye huruma na asiye na makuu na mweny kusimamia kwa nguv zake zote anayo yaamin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mawazi wamekuwa vilaza na wajinga katika matendo yao ya kikazi kwa mujibu wa uwajibikaji wao.........wewe kuna mgomo wa biashara ya korosho Mtwara na unajua zao la korosho linavyosaidia kuingiza pato la taifa ...wewe waziri uko mkoani Kilimanjaro unafanya kazi za kawaida tu.....kwanini huo usiwe ujinga unaoufanya wakati wewe ni mwenye dhamana.tatizo tunataka kuheshimiwa kwa kila jambo kisa tu unacheo fulani.Tatizo la Lissu ni dharau na majivuno na kuonyesha kuwa anajua kila kitu hilo ndilo nalolizungumzia hapa kuliko wenzake na yeye ndiye aanayeonewa kwa kila jambo.....anaongolea kesi zake 8 za kisutu utafikiri hajafanya makosa kwa mujibu wa sheria.....kama akifanya kosa kwa mujibu wa sheria atakamatwa tu na kufikishwa mahakamani hata kama yeye ni mbunge au mwanasheria lakini anaitangazia dunia kuwa yeye anaonewa tu...watz wangapi wana kesi ktk mahakama zetu hapa nchini kwa makosa mbalimbali?....anatumia nafasi yake vibaya na hana lugha nzuri anapokuwa ktk mijadala na wenzake na dharau za waziwazi......anahitaji msaada wa kisaikolojia kwa tukio lililompata la kupigwa risasi.
Kuna watu zaidi ya arobaini kule kibiti na sehemu nyingine za mkoa wa Pwani ambao walipigwa risasi na wale jamaa wa misimamo mikali. Hatujawasikia ndugu zao wakilalamika, zaidi ya kuishi kwa majonzi ya kupoteza wapendwa wao.

Tulitaka kuingiziwa siasa za al shabab ambazo watu wanachukua maeneo ya maporini na kugeuza kuwa ni sehemu zao halali, serikali imepambana na mpaka wale wapumbavu wakaangamizwa, halafu na mbunge nae awe sehemu ya tatizo kwa serikali hiyo hiyo!!.

JPM ni mtu wa vitendo hataki kabisa mambo ya kipuuzi.
 
Ni ujinga wako tu.kwani serikali ya magufuli ndo itakuwa ya kwanza kususiwa na dunia?kama hiyo serikali haifuati sheria au inanyanyasa watu wake sio tu inatakiwa isuziwe hata ikipidi kuondolewa madarakani kwa nguvu ni sahihi.Tanzania na watanzania ni wakubwa na muhimu kuliko magufuli na serikali yake wewe mfia tumbo

Sielewi unazungumzia nini mpaka ukanitukana "ni ujinga wangu tu"? Kama wewe unaona serikali inakunyanyasa basi nakupa pole sana. Lakini mimi ambaye niko nchini sioni manyanyaso hayo. Isitioshe mkuu wa Mkoa RC Makonga alikuwa na vijana juzi kwenye tamasha la kuzuru STGR yetu. Ebu kurudia hapo na wasanii wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi nadhani inategemea unataka kuwalingamisha kwenye mambo gani,kwa mfano kama unataka kuwalinganisha kwenye matumizi ya nguvu nyingi kuliko akili,au ukataka kuwalingamisha kwenye kutenda kwa kutumia mihemuko kuliko sheria na utaratibu Magufuli is far better than Lissu,but kama unataka matumizi ya akili,sheria,free discussion kwenye mombo yanayotuhusu kama taifa,kama unahitaji muono wa mbali then Lissu is far better than magufuli.let me end here for now
huo ni mtazamo wako kama mimi nilivyo na matazamo wangu kuhusu Lissu......kazi ya uongozi Lissu haifai kabisa kwasababu ya kujiona anajua kuliko anaowaongoza na may be uwakili wake wa huko mahakamani unaweza kuwa umemuharibu kwasababu ya kila wakati kuona tu mwenzako ana makosa hata kama anayemtetea ndiye mwenye makosa na ku apply attitude hiyo kwenye mambo ya siasa na uongozi......kazi moja wapo ya wakili ni kumtetea mteja wake hata kama amefanya makosa kweli lakini anatafuta kila namna ya upenyo wa kisheria kuhakikisha mteja wake anaonekana hana hatia mbele ya sheria.
 
Sielewi unazungumzia nini mpaka ukanitukana "ni ujinga wangu tu"? Kama wewe unaona serikali inakunyanyasa basi nakupa pole sana. Lakini mimi ambaye niko nchini sioni manyanyaso hayo. Isitioshe mkuu wa Mkoa RC Makonga alikuwa na vijana juzi kwenye tamasha la kuzuru STGR yetu. Ebu kurudia hapo na wasanii wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huoni watu wanaonyanyaswa na serikali hii either kwa ubinafsi wako au kwa uwezo wako mdogo,niambie Lissu alilisaliti nini hili taifa hadi akasitahili kufa? Je Pole pole ni mbunge wa jimbo gani hapa Tanzania? Na anapozunguka nchi nzima anafanya nini? Je lissu ni mtanzania kama watanzania wengine? Serikalimefanya nini baada ya kushambuliwa kwake?ukiwa mbinafsi au mchumia tumbo ad long as tumbo lako limeshiba huwezi ona.Hiyo ya str hata mkoloni angejenga still tulimuondoa
 
huo ni mtazamo wako kama mimi nilivyo na matazamo wangu kuhusu Lissu......kazi ya uongozi Lissu haifai kabisa kwasababu ya kujiona anajua kuliko anaowaongoza na may be uwakili wake wa huko mahakamani unaweza kuwa umemuharibu kwasababu ya kila wakati kuona tu mwenzako ana makosa hata kama anayemtetea ndiye mwenye makosa na ku apply attitude hiyo kwenye mambo ya siasa na uongozi......kazi moja wapo ya wakili ni kumtetea mteja wake hata kama amefanya makosa kweli lakini anatafuta kila namna ya upenyo wa kisheria kuhakikisha mteja wake anaonekana hana hatia mbele ya sheria.
Sawa ila kama Lissu hafai hata kwa 20% then Maguguli yupo kwenye 0%he is real incomplete na anaficha incompetence yake kwenye ukali na the so called kuabana matumizi ndo maana hasafiri .anashindwa kujua kuwa kuna mambo baba unatakiwa ukafanye mwenyewe na si kutuma mke au mtoto
 
Hata mie mwanzo niliamini kama wewe.. Lakini toka anusurike kuuawa na maharamia wa kisiasa, na kusimama upya na kuendelea kupambana, nimebadilisha mtazamo wangu, Tundu Lissu ndo mtu pekee ambae anaweza kuwa raisi na kuutendea haki uraisi wake.. Sababu moja kubwa Lissu ni muumini wa sheria, hajawahi ku-practise tofauti na anacho kihubiri.. Tunahitaji raisi atakaesimama na sheria, sio raisi anaedhani kila anachosema ni sheria..
 
Back
Top Bottom