Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, harakati ziendane na sera

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, harakati ziendane na sera

UTAKUJA UJE

Member
Joined
Aug 4, 2020
Posts
34
Reaction score
78
Mheshimiwa Lissu na wapenda demokrasia wote.Hongereni kwa kuzindua kampeni leo ktk viwanja vya zakheem Mbagala.Kuna mambo kadhaa nimejifunza,vema tushirikishane.

MOSI: Jazba na hasira.Bado wanachadema wengi wametawaliwa na hasira na jazba.Hili laweza wanyima imani kwa wapiga kura wengi hususani wa vijijini.Mfn,Lema,Mwenyekiti wa baraza la wazee,Mbowe hata Lissu mwenyewe,bado mmetawaliwa na jazba kali.Sidhani kama ni sahihi kuenenda hivo

PILI: MATUMIZI MABAYA YA MUDA:Tundu Lissu katumia muda mwingi kueleza yalompata na kutoa shukrani.Ni jambo jema,lkn itoshe kusema,yalompata Lissu wote tunayajua,tunayalaani na dunia nzima inayalaani.Katika kipindi hiki cha kukimbizana na muda,dk tatu za shurani za jumla zinatosha

TATU: HARAKATI: Kwangu sioni kama zitaleta positive impact kutokana na nature ya nchi yetu,uongozi uliopo na watu wetu.Wapiga kura wengi wa vijijini huwezi waambia ingia barabarani upinge uhuni unaofanywa na watawala,ni waoga,hawatoenda.Jema nililoona NI KUZISHIRIKISHA JUMUIYA ZA KIMATAIFA,NCHI MARAFIKI NA MASHIRIKA MBALIMBALI KUINYOOSHEA KIDOLE TANZANIA.Hili litasaidia sana

NNE: KUKOSEKANA SERA:Mh Tundu katueleza aliandaa hotuba ya kurasa 24,lkn kutokana na uhuni wa engua engua hatoisoma leo,vzr,lkn nadhani angejikita kwenye sera,nini kimo kwenye hotuba ile na akasisitiza juu ya msimamo wao wa kupinga engua engua ingeleta logic.TUTAFANYA HAYA NA HAYA,TUTAONDOA KERO HIZI NA HIZI,Lkn hayo yote tutayafanya baada ya wagombea wetu wote walioenguliwa kihuni kuwa wamerudishwa nk,Mbona CCM wepesi tu

TANO: KUKOSEKANA MSIMAMO MBADALA WA CHAMA.Hapa nimeshindwa kumuelewa Lissu na cdm kwa ujumla,IWAPO TUME HAITOWAREJESHA ILIOWAENGUA KIHUNI,NINI KITAFANYIKA?IWAPO WANANCHI HAWATOFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUDAI HAKI,NINI MSIMAMO WA CHADEMA?

Nihitimishe kwa kuwaomba washauri wa chama,kumshauri vzr Mh Tundu,jinsi gani atumie muda vzr wa kipindi hiki cha kampeni ili kuwashawishi wapiga kura kumuamini na mwisho kuindoa CCM madarakani,mbona simple tu?

Kuna issue nyingi za kuwamaliza,UHURU WAVYOMBO VYA HABARI,HUDUMA ZA AFYA NA VIFAA TIBA,TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA WETU, UMASKINI ULIOKITHIRI MIONGONI MWA WATANZANIA,KILIMO NA MAZONGEZONGE YAKE, WATUMISHI KUNYIMWA HAKI ZAO NK,MIUNDOMBINU MIBOVU NCHINI,UHURU WA MIHIMILI Na mengine mengi mengi mengi
GOD BLESS CHADEMA,GOD BLESS TUNDU LISSU,GOD BLESS TANZANIA
 
UTAKUJA UJE,
Tumehubiriwa na CCM sera nzuri kwa miaka 60 lakini hadi Sasa wastani wa kipato chetu kwa mwaka ni milioni mbili (2,000,000) nadhani tunahitaji kitu kingine zaidi ya sera kututoa hapa. Na hicho ndo Lissu anajifanya Otherwise ccm itaendelea kutunyonya damu
 
Tungu ni kilaza tu hata hajui azungumze nini ,hana sera za kuomba huruma na michango
 
Kwani walisema leo ni siku ya kutangaza sera?
Ulisikiliza vyema kweli?[emoji112][emoji112]
 
We Pendo ww!Uzinduzi wa kampeni manake nn?Nn utafanya iwapo utapata ridhaa ni jambo muhimu sana!
 
Huna hoja- mazingira ya siasa yalivyo ni mhimu kucheza ligi hii kwa akiri kubwa.

Kwa muda wa miaka 5 hukujawahi kuwa na space ya kianaharakati kupenyeza hoja za msingi . Huu ndo wakati wake. Let them go....
Wananchi tunaelewa kinachoendelea
 
Back
Top Bottom