Hamjambo wote!
1. Ndugu zangu Watanzania, mnakumbuka miezi ya nyuma kidogo niliandika nyuzi takribani tatu mfululizo nikiisihi serikali kumiachia Tundu Antipas Lisu.
2. Nafikiri wengi wenu mnakumbuka. Niliandika vile kutokana na sababu kuna Jambo na mambo mengi niliyaona katika spiritual gallery.
3. Mimi sio nabii wala mtume. Lakini kwa walioishi na kukua na mimi wanajua Nina karama nyingine ya siri ambayo siipendi Sana kwani inanifanya niishi maisha ya mawazo.
4. Baada ya kuiomba Serikali kwamba September 7 wamuachie Tundu Lisu. Kila aliyepata ujumbe ule aliuchukulia kwa namna yake.
5. Wapo walioona naitisha serikali. Wapo walioona napiga blablablah. Wapo walioona namtetea Lisu na kutumia mbinu za sungura kuishawishi serikali imuachie.
6. Baada ya September 7 kupita na nilipoona serikali imenipuuza. Kimsingi nilisikitika Sana. Kama mnakumbuka karibu mwezi mzima sikuingia humu JF.
Siku zile nilienda kutuliza roho Yangu kwa kufunga na kuomba. Sio mimi tuu bali mimi na Familia Yangu. Lakini familia Yangu sikuiambia agenda nyingine ya siri ya kwa nini tunafunga.
7. Katika Siku hizo thelasini Siku tatu nilikesha kwaajili ya kumlilia Mungu afute Yale yote niliyoyaona kwenye Spiritual gallery.
8. Lakini mambo Yale yaligoma kufutika. Nilipouliza kwa nini, nikaambiwa kwamba nikasome Aya moja isemayo ukinidharau nami nitakudharau. Huyo ni Mungu.
9. Nilirejea Mtandaoni na kukuta maoni ya Watu wengi wakinilaumu, kunikejeli na kunidhihaki kwamba nilidanganya.
10. Ndugu Watanzania na serikali hasa vyombo vya Dola. Ni muhimu kutambua wapo baadhi ya watu hatunaga interest za kisiasa na tunapojitokeza kuandika au kusemea Jambo Fulani ni muhimu kuyatazama mambo hayo kwa kina kuona ulazima wake.
11. Nilisema tangu Siku ya Kwanza sipo kumtisha yeyote ila nazungumzia uhalisia wa mambo. Kwani mara nyingi ndivyo nilivyo.
12. Kumuachia Tundu Lisu kwa sasa haina maana yoyote Ile tena. Kila Jambo Lina expired date yake.
13. Niliandika pia hakuna umuhimu wa kuwa na kiburi na haimaanishi kwamba pia NI lazima mimi kusikilizwa. Ila kwenye matokeo hakuna hiyari.
14. Nina sikitika njia tuliyoichagua. Sio tuu ni ngumu Bali pia ni Mbaya sana.
15. Niliwahi kuandika pia. Damu ya mtu haifukiwi na mchanga.
16. Hata hivyo ninatumaini dogo. Kama hatutaamua kuchelewa Sana tukaamua kutubu na kuungama Ile roho ya machafuko Mungu ataizuia na Ile spiritual gallery inaweza kuondolewa kwa rehema za Mungu wetu.
17. Kujishusha ni muhimu Sana. Lakini kama haiwezekani pia ni sawa. Kujishusha ni heshima kuliko kushushwa na Mungu mwenyewe au na watu.
18. Mwisho niseme, Kama mtibeli naomba Kila mwenye nafasi aiangalie nchi yetu. Nchi ni muhimu kuliko chama chochote. Nchi ni muhimu kuliko mimi. Nchi ni muhimu kuliko cheo cha MTU. Ni muhimu kujishusha.
19. Watu wasikilizwe.
TaikonMaster
Kibaha mailimoja