Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Ndugu zangu,
Nimepata fursa ya kumsikiliza Tundu Lissu akitangaza ilani ya Chadema nikiri kwa kusema kuwa ili kutekeleza "wish list" yake inahitaji kufadhiliwa na fedha za nje kwa asilimia zaidi ya 90 na uenda akashindwa kulipa hata mishahara ya watumishi wa umma.
Tundu Lissu anasema ataondoa kodi na nyingine atazipunguza ili kuchochea biashara na uwekezaji. Ukitaka kujua kuna utapeli hasemi ataondoa kodi zipi?na atapumguza zipi na kwa asilimia ngapi?
Tundu Lissu ameendelea kuhadaa umma kuwa atalipa fidia watu waliobomolewa kupisha ujenzi.Hapa atatumia sheria ipi kulipa fidia mtu zaidi ya mmoja zaidi ya mara moja kwa eneo lile lile?Je atakuwa tayari kufanya double standard hiyo nchi nzima?ukiacha waliobomolewa kupisha barabara,kuna waliobomolewa kwa kujenga eneo la reli,eneo la miundombinu ya maji na kadhalika atakuwa tayari kufanya hivi nchi nzima?Watu waliolipwa fidia miaka ya 70 na 80 kupisha ujenzi wa miondo mbinu wakawauzia wengine je hapo serikali italipa fidia kwa sheria ipi?Huu ni utapeli.
Mfuko wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HELSB) kama tujuavyo hii ni "relvolving fund" ili wengine wanufaike lazima walionufaika kabla walipe la sivyo mfuko utakufa.Tundu Lissu anaongopea watu kuwa inawezekana watu kulipa kiduchu kiduchu,hii haiwezekani,bodi itashindwa kujiendesha na matokeo yake sababu ya makudanyo hafifu ya marejesho wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu watakuwa wachache.Hili halikubaliki.
Kwa kifupi,ilani hii ya Chadema na Tundu haina uhalisia labda kama nchi itageuzwa "NGO" ya akina Robert Amsterdam"
Nimalize kwa kusema hakuna nchi inayoweza kuwa huru kama serikali yake haikusanyi kodi na wananchi wasipowajibika.
Tujadili kwa makini