Tundu Lissu: Ili mfumuko wa bei upungue Rais apunguze kodi

Tundu Lissu: Ili mfumuko wa bei upungue Rais apunguze kodi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema mfumuko wa bei unaoendelea Nchini kwa bei ya vitu vingi kupanda ni wa Rais na kama akitaka upungue lazima apunguze kodi.

Amesema “Ukipunguza kodi bidhaa zitapungua bei, ila sijasema ifutwe bali ipunguzwe, kwani ni lazima Serikali inununue VX (magari) ya Ths. Bilioni 560 ambayo uamenunuliwa kwa mwaka moja!”

Kuhusu wajibu wa Bunge katika kuisaidia Serikali katika hali kama hiyo, Lissu amesema “Bunge letu ni Bunge la Ikulu tangu Mwaka 1926 lilipoanzishwa.”


Chanzo: Mahojiano ya Jambo TV
 
Ana point, ni bunge la chawa wa kutumikia ikulu na sio wananchi, ndio maana hata mwendazake aliwazimia live TV na ingekuwa wanajitambua asingethubutu , na kuna ulazima gani wa nchi maskini kama Tanzania kutumia bilioni 600 kununua magari ya serikali, Mwigule atoke hajuia anafanya nini, anaua uchumi kwa kuongeza matozo na mikodi inayoua biashara za watu na kufanya nchi maskini zaidi, tunahitaji katiba mpya na bunge lenye nguvu ya kumwajibisha Raisi na maofisa wa serikali wanaokwenda kinyume na sheria/katiba
 
Back
Top Bottom