Tundu Lissu: Kama haujayaweza kwa miaka 20, ukiongezewa miaka Mitano utayaweza?

Tundu Lissu: Kama haujayaweza kwa miaka 20, ukiongezewa miaka Mitano utayaweza?

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara ambaye ni Mgombea wa Uenyekiti wa chama cha CHADEMA, amesema akioata madaraka, kitu cha kwanza atakachofanya ni reforms.

Amesema chama kinatakiwa kiwe na katiba inayoeleza ukomo wa madaraka.

Kutokuwepo na ukomo wa madaraka unafanya watu wajione ni Chama cha Familia.

Ameyasema hayo wakati akiju Maswali Clubhouse.
20241226_124738.jpg

Tundu Lissu

Kwa Mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alitangaza rasmi kuwa kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa Kitaifa na Mabaraza ya Chama hicho utakaofanyika January mwaka 2025 ambapo fomu za kugombea Uongozi ngazi ya Taifa zinapatikana Ofisi za Makao Makuu ya Chama na Mabaraza na Ofisi za Kanda, Mikoa na Wilaya kuanzia December 17,2024 na mwisho wa kurejesha fomu ni January 05,2024 saa 10 jioni.

Tayari Tundu Lissu na Freeman Mbowe wameshachukua fomu za kugombea Iwenyekiti Taifa.

Soma: Tundu Lissu arudisha fomu makao makuu ya CHADEMA akiwa amevaa bulletproof. Hii ina maana gani?
 
Hii ni point, hata ningekuwa Mimi nimekaa kwenye uongozi muda mrefu mathalani miaka 15-20 nisingetamani kutoka. FAL alishajitengenezea mirija ya pesa na fursa CDM japokuwa ni vigumu yeye kuzisema hadharani. Hivyo kuondoka kwake ghafla ni mtihani mkubwa kwake kwani kuna vitu vingi anahisi atavipoteza sana.
 
Nilimkubali lissu alipotangaza kaulibiu ya "NO REFORM NO ELECTION"

LISU ni mtu sahihi kuongoza chama

Natabiri siku ya kwanza lisu akishinda uchaguzi chadema itapata wanachama mil 1. nchi nzima believe me
Kabisa tutajiunga chadema akipata uenyekiti lissu ila akibaki mbowe tutajitenga daima
 
Back
Top Bottom