Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti CHADEMA upande wa Bara Tundu Lissu, amewataka wanachama wa chama hicho kutokuwa waoga katika kukabiliana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchauzi huu wa Serikali za Mitaa na kuwataka kutokuwa waoga wa mabomu. Lissu ameyasema hayo wakati akisalimiana na wananchi wa Kata ya Lamadi wilayani Busega Mkoa wa Simiyu, Leo Novemba 21, 2024 akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Tarime mkoani Mara, ambapo jioni atakuwa na mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.