Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kama unajinasibu unanusa ufisadi, muulize Mbowe michango ya Wabunge iko wapi?

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kama unajinasibu unanusa ufisadi, muulize Mbowe michango ya Wabunge iko wapi?

Ndugu Tundu Lissu mgombea wa CHADEMA unapokuwa jukwaani unaongea kwa jazba na kuonyesha kuwa wewe hutaki ufisadi na matumizi mabaya. Tena unaongea kwa kukakamaa kama unataka kumkaba mtu aliyekwapua mali ya umma.

Tundu Lissu, Wabunge wa chama chako walichangishwa pesa na pesa hizi zilikuwa kwa ajili ya uchaguzi. Lakini ilikuja kubainika kuwa pesa hizo zimekwapuliwa na wajanja kihuni.

Kama unajinasibu kusema unanusa ufisadi kwenye miradi inayotekelezwa na serikali ya CCM basi jikakamue umuulize Mbowe ziko wapi hizo bil 8.8? Hizi pesa zingekusaidia wewe na chama chako kunadi sera zenu kwa ufanisi.

Maana unatuchosha kila kukicha mara ndege za ATCL ni ufisadi, mara uwanja wa ndege Chato ni ufisadi mara Dotto James anajichotea pesa hazina. Basi kama wewe ni mpinga ufisadi kweli kweki anza na hizi ambazo zipo wazi zilikwapuliwa na chama chako ili utuhakikishie kweli wewe unapambana na ufisadi.
Weee weeee weeeee.....Mbowe alikwishawaambia SUMU HAIONJWI KWA ULIMI. athubutu aone kama ataendelea kuwepo Chadema.
 
Baba mwizi mtoto atadiriki kusema ndiyo sidhani.huwa nashangaa kiongozi anapojisifu kufanya jambo fulan wakat ni wajibu wake kulifanya suluh kwa kuwa amepew kijiti.
ifikie mda tutake mabadiliko halisi tuache unafiki
 
Back
Top Bottom