Tundu Lissu katika sura ya Mangosuthu Buthelezi na kivuli cha Charles Njonjo

Tundu Lissu katika sura ya Mangosuthu Buthelezi na kivuli cha Charles Njonjo

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
207
Reaction score
678
TUNDU LISSU KATIKA SURA YA MANGOSUTHU BUTHELEZI NA KIVULI CHA CHARLES NJONJO.

Leo 10:45am 16/08/2020

Mangosuthu Buthelezi katika miaka ya 1975 alipata kuwa kiongozi wa chama cha Wazulu cha "Inkatha Freedom Party" alishirikiana na Makaburu kumpinga Nelson Mandela wa chama cha ANC wakati wa harakati za kuikomboa Afrika ya kusini,Chief Mangosuthu Buthelezi kiumbe wa kiafrika ambaye wazi wazi aliihujumu ANC iliyoongozwa na Wazalendo kupigania Uhuru wa Afrika ya kusini,

Charles Mugane Njonjo katika miaka ya 1975 alikuwa mwanasheria nguli wa Kenya,ndiye aliyemshauri Mzee Jomo Kenyatta kuivunja Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuteka vitu vyote vya kiuchumi vilivyokuwa roho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama shirika la ndege la Jumuiya ya Afrika Mashariki,shirika ambalo lilikuwa kubwa barani Afrika likishindana na mashirika ya Marekani na Uingereza,mtakumbuka ndege zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilishikiliwa pale Nairobi,Kenya kasoro ndege moja iliyotoroshwa na Mtanzania Mapunda kuirudisha Dar es Salaam, Tanzania.

Charles Mugane Njonjo aliwahi kukataa kupanda ndege iliyokuwa na rubani mweusi kwa kuwa alikuwa haamini kupanda ndege iliyoendeshwa na mtu mweusi,kwa hulka na tabia Charles Mugane Njonjo alijiona mzungu na alipenda kuitwa mzungu licha ya ngozi yake iliyokuwa nyeusi tii,hii ni kasumba ambayo imewaingia watu kama Zitto na Lissu hapa Tanzania,Charles Mugane Njonjo daima alimtukuza mzungu na kumdharau Mwafrika mwenzake,akisahau bilionea wa kwanza duniani alikuwa ni Mwafrika Mansa Kankan Musa kutoka Mali.

Mkenya Charles Mugane Njonjo alimtukuza mzungu na kuwatukana Waafrika,Charles Njonjo alikataa kuoa binti wa kiafrika toka kijijini kwake kabete nchini Kenya alipozaliwa akidai Waafrika ni wachafu na itamuhitaji kutumia spirit kumsafisha Mwanamke wa kiafrika baada ya kuoga ili aweze kulala nae,kwa jinsi hiyo ikamlazimu kuoa Mwanamke wa kizungu Bi Margaret Bryson,huyu alikuwa kibaraka wa wazungu mbaya zaidi kuwahi kutokea katika Afrika,

-Tunayo Sababu ya kujivunia Uafrika wetu,

Waafrika tunavyo vingi vya kujivunia wanawake wazuri na warembo,Akili kubwa ya kujenga mapiramid kule Misri hata mzungu akaiga na kujenga ghorofa,Waafrika tunajivunia utajiri mkubwa wa maliasili tulio nao katika Afrika,Mansa Musa aliutumia vizuri utajiri wa maliasili tulionao Afrika na kuwa bilionea wa kwanza duniani katika miaka ya 1300,Bara la Afrika limebarikiwa sana na Mali asili,mfano nchi ya Tanzania tuna kila aina ya kiumbe kwa maana Baada ya mafuriko yaliyoua dunia nzima wakati wa Nuhu,Safina ya Nuhu iliyokuwa na wanyama wote na viumbe vyote baada ya Maji kukauka ilisimama katika Milima ya Uluguru,Mkoani Morogoro,Tanzania.

-Uhalisia wa Uafrika wetu.

Mansa Musa ambae pia alijulikana kama Sandiata Keita,huyu alizaliwa mwaka 1280,na kufa mwaka 1337 nchini Mali,huyu ndie mtu tajiri zaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia kwa lugha ya kaburu tunasema"He was the most richest person ever in the world history" Neno " Mansa" lina maana ya sultan, hivyo Mansa Musa kwa lugha nyingine alijulikana kama Sultani Musa ndiye Mfalme wa Magharibi mwa Africa katika Ngome ya Mali iliyojulikana kama Mali Empire.

Utajiri wa Mansa Musa ulijumuisha vitu vingi sana alikuwa anamiliki vitu vingi sana kama,ardhi,ardhi yote ya mali alikuwa anaimiliki,alimiliki miji 24,ambayo ilikuwa na migodi mikubwa ya dhahabu (gold) mfano wa mgodi wa Wangara,ambao ndio uliokuwa unazalisha dhahabu kwa wingi hapa duniani hivyo kuifanya Mali kuwa ndio Nchi ilioyokuwa ikizalisha dhahabu kwa wingi duniani,

Mansa Musa alimiliki mali zenye thamani ya Dola za kimarekani Trilion moja,(1,000,000,000,000), ukitaka kujua alikuwa anamiliki shilingi ngapi ya Kitanzania badi zidisha hiyo trilion 1,000,000,000,000 × 2300=?, utajua ni sawa na shilingi ngapi,kwa mfumo wa Benki kuu zote duniani,Mansa Musa angekuwepo mpaka leo,angekuwa na utajiri sawa na Familia ya rothchild,ambayo inamiliki mifumo ya benki zote za dunia na kutajwa kama ndio familia inayotawala dunia na kuamua nini dunia ifanye,hii familia ina utajiri wa dola trilioni 500 nusu tu ya utajiri aliopata kuwa nao Mansa Musa,

-Wasaliti waisaliti Afrika yetu.

Kwa mtu anayefuatilia vizuri historia ya harakati za ukombozi au mabadiliko ya kimsingi katika mfumo wa kiutawala katika nchi hatashangazwa sana hili suala. Classic example ni harakati za ukombozi nchi jirani ya Mozambique katika miaka ya 60 na 70 (hii iko within living memory ya vijana wa zamani). Kulikuwa na makamu mwenyekiti wa Frelimo katika miaka ya 60 aliyekuwa anaitwa Uria Simango,

Katikati ya harakati za Ukombozi iithibitika bila shaka yoyote kuwa Uria Simango alikuwa msaliti kwa kuwa alikuwa pandikizi la wakoloni wa Kireno na Makaburu wa Afrika Kusini katika Frelimo. Vikao ndani ya chama cha Frelimo vilifanyika ambapo Simango alikiri kuwa alikuwa pandikizi na pia alihusika na mauaji ya mwenyekiti wa kwanza wa Frelimo (Eduardo Mondlane) yaliyofanyika Dar mwaka 1969. Mwaka 1975 kabla ya uhuru, Simango 'alitubu' hadharani na kujutia usaliti wake katika kambi ya Frelimo Nachingwea na confession yake kutangazwa na Radio Tanzania (External Service).

-Wasaliti waisaliti Tanzania katika Ujenzi wa bwawa la Umeme la Julius Nyerere katika Mto Rufiji.

Wasaliti wakiwa Bundestag,katika kikao cha bunge lao CDU wakapinga kwa nguvu zote kuwa tutaharibu mazingira ya Mbuga ya Selous,wao wako Ujerumani eti wanateseka na Tanzania ilihali Serikali ya Tanzania ilishapewa kibali cha kuendelea (taa ya kijani) na UNESCO Kuendelea na Mradi wa Ujenzi wa bwawa kubwa la Umeme la Julius Nyerere,Rufiji.

Baada ya UNESCO kuridhishwa na ule mpango wa kutumia 3% tu ya eneo la mbuga kubwa kupita zote duniani,ona Chadema walivyo wakawaambukiza wenzao ule ugonjwa wao kupinga kila kitu,CDU nao wakajisahau na kuendelea kupinga huku kwao kukiongoza kwa kuwa na viwanda vingi vinavyotoa ajira kwa Wananchi wao,Viwanda vilivyojengwa baada ya kuteketezwa maelfu kwa malaki ya heka,

Je wao CDU na Ujerumani yao hawathamini baiyonuwai ya kimazingira wanayoipigania kweli eti tutunze mazingira na wao waendelee kutuuzia Umeme,tuingie gharama ya kununua Umeme wakati tunaweza kuuzalisha mto Rufiji,

Tukitaka kuzalisha wanatuambia tuache tutaharibu mazingira,huu ni ubwege wazungu kudhani akili zetu ndogo waendelee kutula hela ya kununua Umeme kwao,Sasa tunajenga bwawa katika mto Rufiji na tutajenga Viwanda vitazozalisha ajira kwa Watanzania Millioni sitini na tutauza Umeme vilevile,

Lissu,Zitto na vyama vyao waliwaunga mkono CDU kuendelea kuuzodoa mpango wetu wa kujenga bwawa la Rufiji,lakini Rais John Pombe Magufuli akasema iwe mvua iwe jua,tupewe hela za msaada au tusipewe hela tutalijenga bwawa kubwa la Umeme katika mto Rufiji ambao upo katika nchi yetu ya Tanzania pasipo kuingiliwa na mtu yeyote kwa hoja ya kuharibu mazingira,

Cutting long story short,Makinikia,Madini,na hii miradi imewaamsha mabwana wakubwa na sasa wameanza kujipenyeza kupitia kibaraka wao Lissu na kuwatumia vibaraka wao wengine kama Zitto,Yuko wapi Mangosuthu Buthelezi aliyekuwa kibaraka wa mababuru Afrika Kusini? Yuko wapi Abel Muzorewa aliyekuwa pandikizi la akina Iam Smith huko Rhodesia?

Tuwakatae Zitto,Lissu na mabwana zao wazungu waliowatuma,kataa vurugu,kataa vibaraka wachumia matumbo,Ndugu zangu Watanzania tuisalimishe Nchi yetu pendwa kwa kuwakataa Zitto na Lissu na vyama vyao na hila zao za kishetani na kihayawani za kutumwa na wazungu kuja kuiharibu nchi yetu ya Tanzania.

-Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam,
0755078854.

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
While the pythons of sickness Swallow the children And the buffaloes of poverty Knock the people down And Ignorance stands there Like an elephant The war leaders are tightly locked in bloody feuds Eating each other’s liver. (Okot p'Bitek)
 
Maneno mengi, machache yenye ukweli . Na majumuisho ya uwongo mtupu.

Ulivyoandika ni kama mwanafunzi wa bachelor, yaliyomo ni vigumu kufikia hata kiwango cha mtu wa diploma. Majumuisho, ni ya mtu aliyeshindwa kuwa mkweli hata kwa nafsi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante Lissu kwa ujio wako maana kwa sasa UVCCM na CCM wanaimba nyimbo zako!

Tutaimba kisha tutatupa kule mkoroni pandikizi,
Vijana wetu bado tunawapenda wawe wenye nguvu na akili kuliko kusababishiwa kuwa legelege na sera za ushoga.
 
Kwa akili hii, na ujengaji huu wa hoja, hufai hata kuwa enumerator kwenye research firm yangu.
Huyu bwana mdogo ni mtoto wa Oscar Mbena aliyekuwa mbunge wa Morogoro mjini mwaka 2000.Baba yake alikuwa na akili na hekima na anayejitambua. Sijui why amekuwa na mtoto wa aina hii surely anakera.Leslie jitambue unamshushia heshima baba yako unaboa na rubbish arguments zako.
 
Huyu bwana mdogo ni mtoto wa Oscar Mbena aliyekuwa mbunge wa Morogoro mjini mwaka 2000.Baba yake alikuwa na akili na hekima na anayejitambua. Sijui why amekuwa na mtoto wa aina hii surely anakera.Leslie jitambue unamshushia heshima baba yako unaboa na rubbish arguments zako.
Please mtendee haki baba yako Oscar Mloka alijitambua tulimuheshimu stop nonsense
 
Propaganda za kikomunist nyakati hizi hazina nafasi, dunia Sasa iko digtal, wenye technologia ndo wanaongoza uchumi wa dunia,
 
Mtayasema yoooote, lakini wapiga kura wataamua, kukaa upande huu wa "ni YEYE" Daudi, ama la, ule wa "ni yule" Sauli. Hisabati na ithibati haviongopi ktk hili.

Kupitia kwa mfano tunaweza kujifunza kitu, "Kutokanaa ya yule muovu, ambaye kwa hila ameotesha magugu ndani ya shamba la ngano. Ni lazima ngano iachwe iote pamoja na magugu, ili wakati wa mavuno ukifika zikapate kutenganishwa na magugu yakapate kuchomwa moto, na mavuno ya ngano yakapate kuhifadhiwa vyema ghalani"
 
Duuuuu kweli ajira limekuwa tatizo mpaka vijana wanaamua kuandika kuponda upande wa pili na kisha kuacha namba zao na cv zao ili wakumbukwe kwenye teuzi. [emoji706][emoji706][emoji706]

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Mnaweza kuandika hadithi na myths ndefu sana lakini kama mmejaa viburi kushughulika na matatizo ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara mtabaki kuimba nyimbo nyingi sana ila hamtaeleweka
 
Back
Top Bottom