Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, Kura yangu umepata

..hizo fedha hufika kwa mkurugenzi wa halmashauri.

..mbunge na madiwani hupanga matumizi ya fedha hizo.

..fedha hizo hazipiti hata siku moja ktk mikono ya mbunge.

..zaidi hizo fedha siyo nyingi, zinatosha kutatua shida ndogo-ndogo tu.

Asante kwa ufafanuzi.
 
Daah kuna mikoa itabakia kwenye lindi la ufukara.

Mfano hapo Singida anakotoka Lisu zaidi ya vitunguu na karanga sijui kuna nini pale jamani.

Lisu anaongea kama hajui alikotoka bwana.
 
Asante kwa ufafanuzi.

Angalia hapa uone jinsi fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo zilivyo kichekesho.

Halafu Jpm ana tabia mbaya sana ya kuwachongea wabunge kwa wananchi kuwa wanapewa fedha za mfuko wa jimbo lakini hawafanyi kitu.

Kuna kamati ya watu 7 ambayo inaongozwa na mbunge ndiyo huamua matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo.

Hii hapa chini ni sample ya fedha za mfuko wa jimbo kwa wilaya ya KONDOA inaongozwa na CCM tangu UHURU.

Tangazo la mgao wa fedha za Mfuko wa Jimbo
 
Daah kuna mikoa itabakia kwenye lindi la ufukara.

Mfano hapo Singida anakotoka Lisu zaidi ya vitunguu na karanga sijui kuna nini pale jamani.

Lisu anaongea kama hajui alikotoka bwana.

..Singida wanalima alizeti.

..utafiti uliofanyika hivi karibuni umebainisha kwamba Korosho inaweza kustawi Singida.

..Singida pia ni wafugaji wazuri wa kuku, mbuzi, na ng'ombe.

..hakuna eneo masikini ktk Tanzania yetu.
 
Kura nyingi tu atapata
 
Daah kuna mikoa itabakia kwenye lindi la ufukara. Mfano hapo Singida anakotoka Lisu zaidi ya vitunguu na karanga sijui kuna nini pale jamani. Lisu anaongea kama hajui alikotoka bwana.
Bahati mbaya Lissu hakusanyi kodi inayotolewa na wananchi wa Singida, na anayekusanya anajua anakozipeleka
 
..Singida wanalima alizeti.

..utafiti uliofanyika hivi karibuni umebainisha kwamba Korosho inaweza kustawi Singida.

..Singida pia ni wafugaji wazuri wa kuku, mbuzi, na ng'ombe.

..hakuna eneo masikini ktk Tanzania yetu.
Daah tatizo lenu hoja zenu ni za kufikirika na za kwenye makaratasi hazina uhalisia.

Ona unavyotaka kudanganya watu hapa kuwa kuku wanaweza endesha maendeleo ya mkoa.

Tusaidie tu contribution kwa sasa kwa mkoa wa singida kwa pato la Taifa.

Mjiandae kulipa fidia mikoa ambayo kwa muda mrefu toka uhuru mchango wake katika pato la Taifa umetumika kuendeleza kwingine.
 

Haiwezekani kukawa na ufisadi sababu wananchi watakuwa na mamlaka ya kumuondoa madarakani kiongozi yeyote wa jimbo tofauti na sasa hata kukiwa na ufisadi mahali hadi kiongozi mkubwa ambaye hakushirikishwa kwenye huo ugisadi aje atembelee hapo nfipo utasikia kuna ufisadi, lakini wananchi wanakuwa wanafahamu ila hawana uwezo sababu viongozi wao ni wateule. Huu utawala wa majimbo ni mwisho wa mafisadi wanaiba pesa sababu wanakuwa na uamuzi wa kuzitumia kwa chochote kile sasa zikiwa jimboni zitakuwa na matumizi ya jimbo.

Hebu fikitia hivi geita lingekuwa jimbo linajitegenea kweli wangetumia pesa za kodi zao kujenga uwanja wa Ndege wa kimataifa chato na je wangekuwa kweli wanafikiria kujenga uwanja wa michezo kwa ajiri ya kuja kutembelea watalii. Haya matumizi mabaya ya pesa ndiyo yanasababisha umasikini kwa watanzania na utajiri kwa watu wachache kutokana na ufisadi.

Kama unataka kuendekea kuwa masikini na kutoa nafasi kwa viongozi kuwa mafisadi utapigia kura CCM lakini kama umechoshwa na umasikini na ufisadi utapigia kura CHADEMA. Mimi kura yangu nitampa Tundu Lissu sababu najuwa anayo agenda ya kweli ya kutuonfoa katika huu umasikini ambao CCM wameshindwa kuondoa miaka 59 sasa.
 

Hapo Dubai palikuwa jangwa lakini nenda sasa ukaone palivyoendelea. Lakini pia usisahau kuwa serikali kuu itakuwepo pia na itakuwa na mapato yake mbona nchi nyingi zinazotumia mfumo wa majimbo zina maendeleo angalia Nigeria angalia South Africa angalia hata Kenya Jirani hapa mapato yao ya mwaka ni mara 3 ya mapato ya Tanzania
 

 
Kuna kila haja ya kila mtanzania anaeipenda kweli nchi yake kuwa balozi wa Lissu, kumuombea kura Lissu kwa watu mbalimbali na kuhamasisha wamchague ili hatimaye watanzania tupate maendeleo ya kweli ya watu na vitu!
 
Asante sana kwa hoja makini!
 
Acheni kupotosha watu kwa akili zenu mgando? Kwani Singida hakuna migodi ya dhahabu? Hakuna mapori ya akiba???Hujui kuwa Singida ndo wanaongoza kwa uzalishaji wa alizeti???

Alafu unafikiri jimbo la kati litakuwa na Mkoa wa Singida peke yake?? Kwa taarifa yako Jimbo la kati linaweza kuwa na sehemu ya Mkoa wa Morogoro, Sehemu ya Mkoa wa Manyara, na mikoa ya Dodoma na Singida. Hujui mikoa yote hiyo ina kilimo kikubwa kinachowezwa kuboreshwa na kufanywa cha biashara ya kuingiza mapato makubwa??? Hujui kuwa kuna mapori ya akiba yenye wanyamapori wa kutosha yanayoweza kitumika vizuri kiutalii na kuingiza mapato mengi sana??? Hujui kuna viwanda pia ambavyo vitazalisha vidhaa na kuingiza mapato mengi sana???

Tatizo CCM mmenyimwa sana akili. Ndo mana kila siku watanzania wanazidi kuwa mafukara
 
Itoshe kusema tu kuwa hiyo sera ni mbovu itabomoa umoja wa kitaifa tuliokuwa nao tangia tunapata uhuru, itazua taharuri na migongano baina ya jamii zetu bila ulazima wowote.

Tafuteni jambo jingine la kudanganya watu ila sio hili.
 
Itoshe kusema tu kuwa hiyo sera ni mbovu itabomoa umoja wa kitaifa tuliokuwa nao tangia tunapata uhuru, itazua taharuri na migongano baina ya jamii zetu bila ulazima wowote.

Tafuteni jambo jingine la kudanganya watu ila sio hili.
Unaitaji kuelimika. Inaonekana elimu ya CCM imekupumbaza sana akili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…