Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kwenye kampeni zako ulimkumbusha Rais Magufuli juu ya ahadi yake aliyoitoa Singida kuitekeleza kabla ya 2020, amekusikia ametekeleza

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kwenye kampeni zako ulimkumbusha Rais Magufuli juu ya ahadi yake aliyoitoa Singida kuitekeleza kabla ya 2020, amekusikia ametekeleza

Jelavic

Senior Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
183
Reaction score
380
Kama tunavojua Rais wetu mpendwa ni Rais msikivu na mchapakazi, kila alichoahidi anajitahidi kukitekeleza, aliahidi kufikia 2020 Upinzani utakuwa umekwisha Tanzania, watu wengi hawakuelewa atatumia njia gani, wengine walivyoona watu wanahudhuria mikutano ya kampeni ya upinzani walibeza kuwa mheshimiwa Rais ameshindwa kutekeleza ahadi yake muhimu kwa chama kilichompa dhamana, lakini kumbe dhana yao haikuwa sahihi, ni kweli aliahidi upinzani utakufa lakini hakusema ATATUMIA NJIA GANI.

Kwahiyo kipimo alichotumia Mh:Tundu Lissu ambacho ni kuhudhuria kwa watu kwenye mikutano, SIO HICHO alichokikusudia mpendwa wetu raisi. Nadhani sasa umeelewa ahadi ya Mtukufu raisi wetu mpendwa imetimia ndani ya wakati Tanzania yote ya kijani na 2020 bado haijaisha.

Tunashukru ulimkumbusha katika muda muafaka, hatimae AMEKUTIMIZIA, Nadhani sasa umefurahi kuona raisi wetu ni mkweli.

Sisi wananchi tunakuona ni shujaa mkubwa sana ambae uliendelea kukumbusha ahadi ya raisi itekelezwe hata kama ulijua utaumiza wanachama wako wachache wasiozidi milioni saba, nadhani uliona kutekelezewa ahadi hiyo kwa wanachama zaidi ya milioni tisa wa chama chetu ni bora ukilinganisha na wanachama wako wachache.

Wewe ni shujaa wa kihistoria, historia itakukumbuka.

Hongera sana.
 
IMG-20201025-WA0041.jpg
 
Kumbuka, pamoja na uchakachuaji wote huo, JPM amechaguliwa na watu chini ya 50% ya waliojiandikisha
 
Hongereni kwa ushindi wa kishindo, msisahau sasa kubadilisha katiba ili nchi iwe kwenye mfumo wa chama kimoja na mtawale milele
Ndivyo siasa zilivyo sometimes. Ni mchezo mchafu usio na huruma wala aibu. Kwa mustakabali wa taifa, ningependa maajabu yatokee katiba ile ya Warioba ipitishwe. Muda wa thamani sana na mabilioni ya pesa yalipotezwa kipindi kile cha JK. Ilibakia kidogo tu tupate katiba nzuri sana ambayo ingepunguza mauzauza haya lakini mtoto wa mjini mwanasiasa mjanja mjanja yule akabadili gia angani dakika za mwisho...

Hata nyie wapinzani mna mengi ya kujifunza katika sakata hili; na kukaa tu mnalalama na kuporomosha matusi humu mitandaoni hakusaidii sana. Kuna kitu naandika nitakutag...

...na usiyachukulie mambo haya personal mamangu. Yasije yakakupa msongo wa mawazo wapendwa wako wakateseka [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Back
Top Bottom