Tundu Lissu: Msimamo wangu kuhusu vita vya Ukraine unafanana na msimamo wa Mwalimu Nyerere wakati wa vita vya Soviet Union na Czechoslovakia 1968

Tundu Lissu: Msimamo wangu kuhusu vita vya Ukraine unafanana na msimamo wa Mwalimu Nyerere wakati wa vita vya Soviet Union na Czechoslovakia 1968

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Lambert alimuuliza Lissu swali la kushtukiza kuhusu msimamo wake kuhusiana na vita ya Drc na Ukraine kama angebahatika kuwa Raisi.

Lissu alijibu kwa kifupi kuhusu Drc kwamba suluhisho ni kuunganisha nguvu za nchi majirani ili kupata amani nchini humo.

Kuhusu vita vya Ukraine Lissu aliibua hoja ambazo nadhani Watanzania wengi hawana habari nazo. Lissu alirejea msimamo wa Tanzania au Mwalimu Nyerere kuhusu vita vya Soviet Union na Czechoslovakia mwaka 1968. Vilevile alielezea historia ya matishio ya usalama wa Russia tangu enzi za Napoleon, na kusisitiza kwamba suala la usalama wa Russia ni lazima lichukuliwe kwa umakini ktk kutatua mgogoro kati yake na Ukraine.

Kwa kifupi Lissu ana elimu[vijana wanaita madini] kubwa sana ambayo ili kuipata waandishi wa habari wanatakiwa waulize maswali sahihi, na sio maswali ambayo Lissu ameshayajibu mara kadhaa.

 
Kwa hiyo Lissu kasisitiza zaidi usalama wa Russia tu ndio wa kutazamwa, vipi kuhusu Uhuru wa Ukraine kama taifa huru ?
 
Kwa hiyo Lissu kasisitiza zaidi usalama wa Russia tu ndio wa kutazamwa, vipi kuhusu Uhuru wa Ukraine kama taifa huru ?

Inabidi uujue msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu vita vya Soviet Union na Ukraine.

Lissu amesisitiza suala la uhuru wa Ukraine na kulindwa kwa mipaka yake.

Lakini pia amechambua historia ya matishio ya usalama wa Russia tangu zama za Napoleon.

Sidhani kama Wanadiplomasia wetu wanaweza kudadavua suala hilo kwa namna Lissu alivyofanya.
 
..inabidi uujue msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu vita vya Soviet Union na Ukraine...
Usalama wa Russia unahusishwa na hofu yao dhidi ya NATO kujitanua mpaka nchi zilizowahi kuwa himaya yao ya kiushawishi.

Ila nchi hizo mfano Poland, Baltic ziliamua kujiunga NATO kwa hiyari yao sababu ya hofu yao ya kuvamiwa na Urusi na sasa hofu yao imedhihirika ilikuwa sahihi kabisa baada ya Ukraine kuvamiwa.

Lissu awe makini kuhusu hili suala ikiwezekana tuwe na msimamo wa pamoja na mataifa mengine ya kikanda mfano AU, SADC, EAC mfano mzuri ni kama sasa tulipokataa kuunga mkono upande wowote, kuwa na msimamo binafsi kama taifa wakati huu bila kuungana na wengine kikanda ni hatari kidiplomasia.
 
..Lambert alimuuliza Lissu swali la kushtukiza kuhusu msimamo wake kuhusiana na vita ya Drc na Ukraine kama angebahatika kuwa Raisi...
Kama Deep state haitomtumia huyu jamaa KATIKA nchi hii Bas mi Sina cha kusema!!

Nchi ni yetu sote hii kwann Haya?

KWANINI mtu asitumike kutokana na uwezo wake bila kujali ITIKADI yake ya kichama!!?

Mungu ibariki TANZANIA nchi yetu niipendayo Sana
 
Huyu jamaa aliyekua anamsimanga nyerere leo anajiweka kwenye misimamo yake aiseee

..Lissu hakubaliani na mawazo ya Mwalimu kuhusu muungano.

..Lakini Lissu amenukuliwa akimsifu Mwalimu Nyerere kwamba ndiye Raisi pekee ambaye hakutuibia Watanzania.

..Zaidi alikwenda mbali mpaka kueleza kwamba Mwalimu Nyerere alistaafu bila pensheni.
 
Huyu jamaa aliyekua anamsimanga nyerere leo anajiweka kwenye misimamo yake aiseee
Kwani Nyerere alikuwa perfect kwa Kila jambo kama Mungu? Yapo aliyofanya vizuri kama kuliunganisha taifa lakini kuhusu Muungano na katiba hii ya 1977 alifanya makosa makubwa yanayotugharimu hadi Sasa.
 
Huyu jamaa aliyekua anamsimanga nyerere leo anajiweka kwenye misimamo yake aiseee
Fikra zako ni dhaifu zana, na ni tatizo la wengi wa kizazi hiki. Yaani mtu utamsikia namwunga mkono Rais Samia au Magufuli au Mwalimu Nyerere, na kwa upeo duni anaamini kuwa maana yake ni kuunga mkono kila kitu, kiwe kibaya au kizuri. Huo ndiyo uzezeta.

Unaunga mkono fikra au matendo ya mtu fulani. Huungi mkono mtu. Lisu, hapo ameeleza vizuri sana, na ndivyo sisi sote tunavyotakiwa kuwa. Amesema, "katika suala la vita vya Russia na Ukraine, msimamo wangu ni kama wa Mwalimu Nyerere wakati wa Vita kati ya Russia na Czekislovakia", hajasema anamwunga mkono Mwalimu kwa kila kitu. Na hata aliposema anatofautiana na Baba wa Taifa, ilikuwa ni kutofautiana na Mwalimu Nyerere katika fikra na sera za uchumi na masuala ya Mwungano. Hakusema yeye anamchukia Mwalimu Nyerere au alikuwa na uadui na Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere, aliwahi kuwakemea wajinga wa utawala wake ambao wakati huo kwenye mikutano walikuwa wanasema zidumu fikra za Mwenyekiti. Mwalimu aliwakanya kuwa siyo sahihi. Fikra za Mwenyekiti zidumu hata kama ni za hovyo? Aliuliza Mwalimu Nyerere. Ndipo walipobadili na kusema, zidumu fikra SAHIHI za Mwenyekiti. Maana yake Mwenyekiti anaweza kuwa na fikra zisizo sahihi. Na hizo hazistahili kudumu wala kuenziwa.

Siku hizi tuna wajinga wanaoelekea kwenye uwendawazimu, ambao wengine kazi yao ni kusifu yote anayotenda au anayoyapenda Rais. Kama vile kwao Rais ni malaika, au Serikali ni ya malaika, haiwezi kukosea katika lolote. Hawaelewi hata kwa nini mataifa yaliamua kuwa na Serikali, Bunge na Mahakama kama mamlaka zinazojitegemea. Hawajui kuwa hizo taasisi ziliundwa ili kuwepo na vyombo zaidi ya kimoja kwaajili ya kusahihisha makosa yanayofanywa na taasisi nyingine, kama yapo.

Kijana unaaswa, usiwe chawa, usiwe shabiki wa mtu, uwe shabiki wa fikra, falsafa au matendo yake.
 
Huyu jamaa aliyekua anamsimanga nyerere leo anajiweka kwenye misimamo yake aiseee
Nyerere unayemsema yeye mwenyewe aliwahi kukiri kuna Mambo alikosea. Sasa wewe unayedhani Nyerere alikuwa Malaika asikosolewe umetoka wapi? Lissu kumkosoa Nyerere hakufanyi asikubali mazuri yake. Hata Magufuli anayemkosoa anajua ana mazuri aliyofanya. Wepesi wa akili yako ndo unadhani katika uzuri Hakuna kasoro.
 
Samia kama anataka kufanikiwa amteue Lissu kuwa mshauri wake wa maswala ya kisheria, MO, GSM, Bakherasa, Rostam wawe washauri wake upande wa uchumi, Mbowe awe mshauri wake kwa mambo ya kisera nje na hao chawa wake atafanikiwa sn.
 
Nyerere unayemsema yeye mwenyewe aliwahi kukiri kuna Mambo alikosea. Sasa wewe unayedhani Nyerere alikuwa Malaika asikosolewe umetoka wapi? Lissu kumkosoa Nyerere hakufanyi asikubali mazuri yake. Hata Magufuli anayemkosoa anajua ana mazuri aliyofanya. Wepesi wa akili yako ndo unadhani katika uzuri Hakuna kasoro.
Point sn
 
Fikra zako ni dhaifu zana, na ni tatizo la wengi wa kizazi hiki. Yaani mtu utamsikia namwunga mkono Rais Samia au Magufuli au Mwalimu Nyerere...
Mwenye sikio na asikie.
 
Fikra zako ni dhaifu zana, na ni tatizo la wengi wa kizazi hiki. Yaani mtu utamsikia namwunga mkono Rais Samia au Magufuli au Mwalimu Nyerere, na kwa upeo duni ...
Una madini sn safi, kuna tofauti kubwa kati ya chuki na kuunga mkono
 
Back
Top Bottom