Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Embu Watanzania wenzangu tuchukue wasaa kujikumbusha mafundisho muhimu sana yaliyopo katika hadithi ya Daudi, Mwana wa Yese. Naweza kuandika volume ya vitabu kuhusu hadithi ya Daudi na mafundisho yake.
Daudi alikuwa mpakwa mafuta ambaye angali bado mdogo alipewa kibali cha kuwaongoza Wana wa Israeli. Ni lini na kwa njia gani unabii huo ungeenda kutimia, si yeye wala Samweli, Nabii aliyetumwa kumpaka mafuta waliokuwa wanajua.
Ukiweza kujitenga na ushabiki wa kisiasa na kuuweka pembeni, utaona wazi kabisa kuwa Tundu LIssu amepewa kibali cha kuwaongoza Watanzania. Njia anayopitia ni kama njia ya Daudi, Mwana wa Yese. Ni njia ya kupambana bila kukata tamaa, ya kuwakimbia watesi wake, ya kusamehe, ya kuvumilia, ya kuepuka kulipa kisasi hata pale unapokuwa na nafasi, ya kuwa na uwezo wa kunyumbulika kulingana na mazingira na changamoto iliyopo mbele.
Daudi alikuwa mchunga kondoo, commando, superspy na mwanasiasa. Kama ambavyo sina uhakika wa mafunzo aliyopitia Daudi katika maeneo haya, ni vivyo hivyo kwa Lissu ila kuna viashiria ana "uwezo wa asili" aliopewa na Muumba katika maeneo haya yote. Experience ya maisha na changamoto alizopitia inampa "on the job training" aliyohitaji ili ahadi ipate kutimia.
Sijui itakuwaje mbele ya safari ila kama hadithi hii ya Daudi nimeielewa na inatupa fundisho, inawezekana kabisa kwa Tundu, mwana wa Lissu akaja kupata kile alichoahidiwa, nalo ni kuwaongoza Wana wa Tanzania.
Ni suala la muda tu. Wanasema "It's not a matter of if but when".