Where are they Sir?kitendo cha tundu lisu kumtukana nyerere kimewasikitisha sana dr.slaa na mbowe
Waarabu tuna usemi NI RAHISI SANA KUWADANG'ANYA WATU, LAKIN NI VIGUMU SANA KUWAAMBIA WATU KUWA MUMEDANG'ANYWA NA WAKAKUAMINI.
Ahsantum Tundu Lissu kwa kubainisha usemi wa Bob Marley katika album yake ya Uprising wimbo Redemption. alinena hivi
YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CAN'T FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME.
Hongera sana Tundu Lissu
Amemtukanaje Nyerere?, hoja ipingwe kwa hoja, acheni ushabiki wa kipuuzi, kama vipi weka hayo matusi aliyotukana, jamaa ana vithibitisho kabisa, wewe unakuja na maneno matupu tena ya kijinga...Tindu lisu uliyesoma bure leo unaweza kumtukana Nyerere? Siasa imekupa kiburi? Nimekutemea mate usoni puuuuuu.
Jumbe alikuwa si Mzanzibari?
Wolfgang Dourado alikuwa si Mzanzibari?
Tundu Lissu anasema wote hao walipohoji kuhusu muungano Nyerere aliwaweka kizuizini.
Njoo na lingine.
na wewe sometimes hauna tofauti na MamndenyiSometimes naona Lissu hana tofauti na Lema
debe tupu ni wewe pamoja na Ng'wamapalalaWote ni debe tupu
Yes, yes, kwanini ukasingle out nyerere na umerudia tena kusingle out nakuwaacha Shivj, mwakyembe nk
Ungekuwa na lengo zuri ungebalance hoja yako kwa uwakilishi kama Lisu alivowasilisha.
Kuchukuwa Lisu Vs Nyerere peke yake nakuacha hao alioweka nukuu kutoka vitabu vyao maana yake nimoja tu
1. Kujenga hoja ya kumchonganisha Lisu kwa baadhi ya watu, yes yako inaukweligani ikiwa hawa wengine kwenye heading yako hawaonekani? propaganda za kiccm kuishi kwa uwongo, majungu na fitina.
2. sio rahisi kwa mwanaccm kukubali kwamba nje ya ccm kuna watu wengine wenye uwezo, kwa ujanja wa hali ya juu unajaribu kumpaka Lisu mafuta kwa kipande cha chupa ilihali ukimhujum kwa kumjengea bifu nakwahili umefanikiwa nimeona michango mingi tu ambayo umekamatisha nakufikia malengo.[
Hili ndilo Lisu alosema wewe na ccm yako manishi kwa uwongo na ujanjaujanja.
Wewe unadai aina ya Muungano wa Abeid Amani Karume na Mwl. Nyerere wakati wenzako wanakuambia, kisheria hakukuwa na Muungano!.Aina ya Muungano wa Karume na Nyerere ni Tofauti na Muungano wa Sasa,kwani Muungano wa Sasa umejaa Magumashi,Ukiritimba,na Maujanja Mengi,Hata Zanzibar wametumia Fursa hiyo Kujigeuza Nchi Kinyemela na sasa Rais wao ni Amri jeshi anakagua Gwaride la vikosi vya Ulinzi nk,Waziri Mkuu Hana Sauti au mamulaka Zanzibar ,ni Kama hawamtambui,Nyerere alipenda mabadiliko Ndio Maana alianzisha mfumo wa Vyama vingi, Nina imani angekuwa Hai lazima angekubali kwenda na wakati , yaani kuirejesha Tanganyika na kumaliza Unyonyaji wa Zanzibar juu ya Pesa za Tanganyika kwa visingizio vya kumaliza Kero za Muungano.
Mbona mimi nilisikiliza hotuba ya Tundu Lissu hayo maneno kwenye bold sikuyasikia au we runinga yako inasikikaje au ina fasiri kabisa, halafu mbona unanukuu kana kwamba runinga unayo mwenyewe humu jf, acha upotoshaji basi, au TBC walipokata akaendelea akatamka hivyo?Kwa hiyo unaulibali uwongo na udanganyifu wa Mwl. Nyerere kuhusu Muungano?. Mh. Lissu amesema, Mwl. Nyerere alikuwa muongo na mdanganyifu kama alivyobainisha kwenye maandiko yake na vitendo vyake.
Nyerere ktk Hotuba zake alikubali Kuwa Wakati wa Utawala wake wa Miaka 26 Serikali yake ilitenda Mabaya na Mazuri ,lakini ikija Serikali mpya inachukua Mazuri hasa ya Msingi inayaendeleza na Yale mabaya wanaachana nayo , huenda Muungano kukosa Hati ni mojawapo ya Mabaya,lakini Tambua Nyerere alikiri Mapungufu Enzi ya Utawala wake , hapaswi kulaumiwa sana,Watawala wa sasa Ndio wa kulaumiwa kwa Kuiruhusu Zanzibar kujitangaza Kuwa ni Nchi huku Pesa za kuwahudumia zikitoka Tanganyika ambayo sasa imekuwa Koloni la Zanzibar inasaka uhuru wake.
Lissu omba radhi. Kumtukana Nyerere ni kuwatukana watanzania
Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.
Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, "Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.
Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.
Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.
Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.
Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).
Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.
Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.
Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.
Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.
Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.
Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!.
[video=youtube_share;bB7BxxMepR8]http://youtu.be/bB7BxxMepR8[/video]
[video=youtube_share;jE7oTPXtpas]http://youtu.be/jE7oTPXtpas[/video]
debe tupu ni wewe pamoja na Ng'wamapalala
Udini at Work