Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Ng'wamapalala kwa kiasi fulani anaweza akawa sawa, lakini title aliyoamua kuitumia ana madhumuni fulani, yaani amelenga kitu fulani, yaani ametoka title kwa kufasiri na kuchambua...
Mkuu, hili siyo suala la kuwa "sawa kwa kiasi fulani". Maudhui ya Mh. Lissu ndiyo yanayotengeneza title ya kile alichokisema pale bungeni.

Ninadhani unasumbuliwa na kaugonjwa ketu watanzania wengu ambako ni kutokubali ukweli kwa jinsi ulivyojibainisha/unavyojibainisha.
 

Shukran Mkuu nimekusoma!

Pamoja kwa saana tu Kaka!

Mpaka sasa hatujashuhudia yeyote aliekuja na hoja nzito zenye mantik hapa jamvini...wengi wao wanajitahidi tu kukubeza na kukulaumu weye mbeba ujumbe!? Daah!

Endelea kumwaga dose Kaka...Wazalendo wenzio tunakusoma!

Wee mtu unatisha! Duuh!

Pamoja kwa saana tu!

Ahsanta.
 
Lisu anawapatia sana magamba. Anawatia taratiiiibu!

Mkuu,

Mbona watuletea lugha za kibanati na makhanatha!?

Au umeamua kumchafulia hii thread yake Mkuu Ng'wamapalala!?

Sidhani hao uwaitao ati "magamba" wana appreciate lugha utumiayo dhidi yao!? Daah!

Ahsanta sana.
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

Haaaahaaaa....hajagundua hilo miaka yote hii? Kuna game nyingine ndogo ndogo zinawatoa povu mpaka super strikers kwa ugumu wake wa kuzicheza. This is one of those games kwa mhe. Lissu,lol!
 
NI ukweli kuwa nyerere alifanya mambo mengi makubwa lakini ni ukweli kuwa alifanya pia makosa makubwa mojawapo ni hili la Zanzibar na muungano, Zidumu fikra sahhi za Nyerere
 
NI ukweli kuwa nyerere alifanya mambo mengi makubwa lakini ni ukweli kuwa alifanya pia makosa makubwa mojawapo ni hili la Zanzibar na muungano, Zidumu fikra sahhi za Nyerere


Mkuu wakupaswa kumlaumu Nyerere ni Watu Wa Nchi ya Zanzibari na sio sisi Watanganyika!

Kuna Kitu Nyerere alikona Zanzibari ambacho ni faida kwetu sisi watanganyika! Na ndiyo maana ikabidi tuwakalie tu wazanzibari kimabavu !

Nyerere hakufanya vile kwakuwa alijiskia tu bali ni faida kubwa aliyoiona kwa sisi watanganyika !
 
Mkuu,

Mbona watuletea lugha za kibanati na makhanatha!?

Au umeamua kumchafulia hii thread yake Mkuu Ng'wamapalala!?

Sidhani hao uwaitao ati "magamba" wana appreciate lugha utumiayo dhidi yao!? Daah!

Ahsanta sana.
Hii ngoma nzito sana hakuna Bavicha yeyote atakaeweza kuingia humu.

Nyerere, ni role model wa Dr.Slaa, Lema, Mnyika, Mbowe, na Bavicha, sasa Tundu Lissu, anawambia Nyerere alizoea kuishi kwa uongo.

Na Bavicha wanamuogopa Tundu Lissu unaona kazi hiyo.
 
Andiko lako linachagiza kuwa Mwl. Nyerere na Watanganyika waliihujumu Zanzibar kwa maslahi yao!. Are you serious?.

Hebu nisaidie kwa kudadavua zaidi.
 
Muunganooooo .hivi pemba na unguja viliungani vipi....Maana naona tanganyika na zanzibar tu.
 
Tumekuwa tukisema kwa miaka mingi sana kwamba nyerere alikuwa bumunda tuu, tunaitwa waislamu. Miaka kadhaa iliyopita miongoni mwa waja wa nyerere wa hapa JF, mmoja wao alisema nyerere ni zaidi ya mandela. Nikamjibu kwa kumwambia kwamba tofauti ya nyerere na mandela ni kwamba, Mandela angezaliwa nchi yoyote duniani, basi angekuwa rais wa nchi hyo. Lakini nyerere asingeweza kuongoza nigeria hata kwa siku tano tuu.

Haya sasa, baba wenu wa taifa huyo.
 

Kumtazama nyerere kwa jicho la tatu ndiyo kwanza unaanza leo? "welcome to the reality son". Watu wakisema kwamba nyerere ni muongo, dictator, mwoga wa mapambano ya kimawazo;.... wathao mnawaita siasa kali.
Haya haya yaliyosemwa na tundu lisu kama yangesemwa na sheikh ponda au ustaadh bin jumaa; wote msingeyaamini.
 
Waswahili bwana wamezoea ukoloni wa kifikra...mtu akisema ukweli anaitwa mkorofi na mwenye kiburi..tena maneno yake yaukweli yanageuzwa kuwa matusi...acheni ukoloni wa kifikra..ni wapi palipoandikwa mtu akishafariki mabaya yake yasijadiliwe?kama ni dhambi basi pia acheni unafiki wa kuenzi mazuri ya marehemu..
 
Kina shekh Ponda,Ilunga,na wapambanuzi wengi includence of me...tulifaham kwa kina mbichi za mwl Nyerere kitamboooooo....Hongera Hon Lissu kwa kuungana nasi katika kuweka bayana ukweli pacna woga....
 

Kila kitabu na zama yake! Mimi sioni dhambi ya watanzania kuhoji leo kama Muungano una uhalali , au kama una usawa, au kama kasoro zake zinatatulika! Kama Watanzania wa 1964 hawakuwa na uelewa huo, wa leo wanao. Kama wanao sioni kama ni dhambi kwao kuhoji.

Binafsi najua ni kweli kuna usanii mwingi umekuwa unafanywa. Historia ya nchi yetu imepotoshwa sana tu. kwa kiwango ambacho watoto wetu wanazaliwa wakiujua owongo huo. Wanakua wakiukulia uwongo huo! hii ni aibu.

Ni katika misingi hiyo ya uwongo na ubabaishaji ndipo ilipozaliwa serikali ya ovyo kama hii ya sasa. Ambapo wananchi wamekuwa wanadanganywa kila kukicha, mpaka wanakuwa wageni kwenye nchi yao.

Wanatakiwa wahoji. Naaam wahoji kila kinacholeta mashaka. Ni haki yao na wanawajibika kufanya hivyo.
 

Nyerere alishakiri si mara moja kuwa kuna mambo mazuri alifanya na mengine mabaya, kwanini sisi tunataka kumfanya yeye ni malaika hakukosea?
 
Tusubiri, ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Kumbuka juzi, Sitta ingawa yupo busy bungeni lakini kaitwa na Pengo na kaenda mbio-mbio, jiuliize kunani?

Na kwa Shehe Mkuu mbona husemi? ??
Acha udini wako Mtoto wa Kike...!
 
Tundu lisu anaona uwongo wa mwl.nyerere2...mbona hasemei uongo wa historia aliyosoma ya watu kutokea kwa nyani? Au wakisema wazungu siyo uongo? Wakat huyu mzee akiwapo hakuna hata paka mmoja aliyethubutu kusema kwa kuogopa kuumbuka, ni uongo huu huu ulitupatia ziwa nyasa, mt.kilimanjaro na kagera. Ule ulikuwa wakat wao yeye leo amefanya nn kama siyo porojo2 na kula pesa za walala hoi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…