Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

chogomzingwi Haya hiyo hati imeongeza au kupunguza nini? By the way sikuwa nna shida nayo. Naamini muungano Upo sikuhitaji hati. Kama nnavyoamini kuwa baba na mama yangu ni Mke na mume. Sihitaji cheti Chao cha ndoa.

angalau imetujuza tabia za viongozi wa ccm na serikali yetu,unakumbuka majibu yaliyokuwa yakitolewa kabla ya hiyo hati kutolewa?.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Kwa hakika huwa nashangazwa na wanaofikiri kwa akili kama yako!

Watu ambao hawawezi kusimamia ukweli kwa sababu ya uchaguzi na umaarufu!

Hii kwa hakika ilikuwa ni tabia ya CCM,kudanganya watu kuahidi ahadi ambazo hazitekelezeki just for election winning!

Inasikitisha sana kuona kuna baadhi ya wasomi ambao wanaendelea na utapeli huu na kuzifanya professional zao ziwe very irrelevant!

Hakuna mtu anayeweza kusimamia uadilifu,hakuna mtu anayeweza kusimamia ukweli,wote mmebaki kufanya utapeli wa kisiasa ili mzidi kufanikiwa.

Umenisikitisha sana!


MTANGANYIKA DAIMA!

Kuna uadilifu gani kwa Lissu kumuita Nyerere ni Tapeli, na Muungao ni batili halafu hajawahi muchallenge Nyerere akiwa hai, wala huo muungao kortini?

Ukweli kusema hati ya muungano haipo wakati hata mtoto wa darasa la pili mwenye kuweza kupambanua mambo anaweza jua huo ni upuuzi?Hivi wewe miaka yako uliyoishi duniani unaamini kabisa kuwa hati ya muungano haipo?kuna tofauti kubwa ya ukweli na shutuma. Shutuma kila mtu anaweza kuzitoa. Naichukia sana CCM kwa matatizo yaliyokuwepo hapo nyumbani lakini sio kwa kutukana watu hovyo.

Huyo Nyerere mnayemtukana yuko wapi kujitetea?where is dignity?where is sense rationality? Wanachokifanya CDM sasa kina faida ipi kwa taifa?kuwaambia watu Nyerere alikuwa Tapeli kunasaidia vipi kupatikana kwa katiba bora?

Go back read my 600+ posts utaelewa nasimamia wapi, shutuma unazozitoa hapa na anachofanya Lissu, hakina tofauti, Unfounded nonsense based on heat of the moment. Kwa lugha nyepesi, tunaita hot headness.
 
Jamaa kaanzisha thread halafu faster kasepa, nadhani alikuwa anapima kina cha maji
 
Upeo mdogo wa uelewa ndiyo sababu ya kumuona Tundu Lisu katuma,ni Viongozi wangapi wa CCM wenye uwezo wa kusimama na kuwaambia wananchi ukweli wa mikataba na pesa wanazopiga daily?
Sipo upande wowote wa chama lia kwa la Tundu Lisu nampa big up kuelezea ukweli halisi na ndiyo maana hadi kesho CCm wanalilia kinga ya raisi ili hata akifanya madudu na genge lake alindwe na kupewa heshima tuu.
Hapo maisha ya ndiyo mzee yamepitwa,tunaitaji hoja zilizotukuka kwa manufaa ya nchi yetu.
 
huu hauwezi kuwa uchangiaji wa mtu makini.,

Nisema tayari, ninasema tena Lazima tujifunze staha na kuvumiliana,. Matusi haya jengi nchi!

Siasa za upinzani nchi hii za ajabu sana, hazina malengo ya uungwaki mkono ili wakubalike na wengi, siasa zao ni za kuongeza maadui. Inashangaza kuona wawadhihaki na kuwakashifu watu ambao kesho watawaomba na kuwahitaji ili wafanikishe malengo yao kisiasa. Angalia ndani ya bunge leo, uungwaji hoja ni wa 2/3 miongoni mwao lakini wanawatukana, wanawakashifu wajumbe wanaowahitaji kesho! kan kwamba hoja zao zitapita kwa mabavu!!!
 
Nimeshangazwa na mwanasiasa kijana mwenye taaluma ya uchumi Mwigulu Nchemba kutamka kuwa kuendesha serikali ya Shirikisho ni gharama kwa kuwa itatugharimu Shilingi Trilioni Tatu.Sasa kwa mujibu wa utafiti uliifanywa na wasomi katika mchango wao kwenye mjadala wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere walisema Tanzania hupoteza Takribani Trilioni 2.5 kila mwaka kutokana na uzembe wa kutokukusanya Kodi.Mwigulu Nchemba ni Naibu waziri wa Fedha.Anakwepa wajibu hapa.

Ndugu Zitto Kabwe,Mwanasiasa kijana mwenye Taaluma ya Uchumi alipokua kwenye Mkutano wa Hadhara kule Shelui alisema Serikali hupoteza takribani Shilingi Trilioni 1.5 kwenye sekta ya Madini pekee kwa Mwaka.

Tunaacha kutumia raslimali zetu lakini tunatafuta balaa la kisiasa kwa kutosikiliza matakwa ya wananchi.Tunatafuta political crisis kwa nguvu

Kama serikali Tatu ni gharama ,kwanini iwe serikali mbili na sio serikali Moja ?

Nanyi wabunge wa bunge la katiba jitahidini kuwajibu watu kama hawa instantly kwa Takwimu na Facts.Ndio dawa yao tu

Kuna hoja iliyonishangaza leo,Eti Kanisa Catholic linataka kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu kwa hiyo hastahili kukosolewa?

Yaani haistahili kusema ukweli kuwa Mwalimu Nyerere ali-issue Presidential Decree(Amri ya Rais) ili kuiua Tanganyika?Kwa kawaida Presidential Decree huwa issued na Madikteta na Wafalme.Mwalimu Nyerere alishawahi kukiri kufanya makosa.Wapo baadhi ambao hawataki kujadili kwa uwazi kwa kuhofia kumdhalilisha mwasisi.Hizi ni fikra finyu zinazoendeleza uimla.

Mimi ni Mkatoliki lakini sikubaliani hata kidogo na watu wanaotumia mchakato wa kanisa kumtangaza Mwl.Nyerere kuwa Mtakatifu kama chambo katika suala la kisiasa au suala hili la katiba.

Leo wacha niseme.Tusikubali viongozi wa Dini kutuburuza kimawazo kuhusu suala hili la katiba maana baadhi yao waliwahi kutuambia baadhi ya wagombea Urais ni machaguo ya Mungu kutokana na mitizamo yao binafsi na maslahi yao yasiyokua ya kiroho(Spiritual)

Adolf Hitler alisaidiwa na Askofu Pacelli Kuingia Madarakani kabla hajawa papa.

Mauaji ya Chama cha NAZI dhidi ya Wayahudi Papa Pius Aliyakalia kimya.Adolf Hitla na Pacelli kabla hajawa Papa walikua na Mkataba(Concordat) ambao baadae waliliunganisha kanisa na kujenga uhusiano kati ya Vatican na Serikali ya Kijerumani.

Ukisoma Kitabu cha John Cornwell chenye Title 'Hitlers Pope" Utaona kwanini nasema haya

Kuna kitabu kingine 'Hitler,War and the Pope'

Sasa tujitahidi kujisomea ,tusikubali kuyumbishwa na Baadhi ya Viongozi wa Dini na mambo yao binafsi kwa maslahi binafsi

Nimethubutu kusema .

Ninashangazwa sana na jitihada za kuburuzana na wengine kushawishi kutukuza na kutakasa udikteta kuwa utakatifu.Leo watu wanathubutu kusimama na kusema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu wakati huo huo Mtu/watu waliozuia sauti za wengi kwa zaidi ya Miaka 20 wanatakaswa.Watu waliokuta vyama vya upinzani na majukwaa ya kupaza sauti na maoni mbadala kisha akayavunja na kufuta vyama vya upinzani kama wafanyavyo madikteta wengi anaitwa Mtakatifu.

Sitawahi kushawishika kufuata misingi ya kutukuza wanaominya sauti za watu

Itoshe tu kusema kiongozi fulani alikua kiongozi mzuri kulinganisha na Madikteta wengine kama Akina Idd Amin .Basi ,Inatosha.

Mwalimu Nyerere Kuwa Baba wa Taifa ndio heshima inayostahili .Mahali alikofanya Makosa tutasema na kupendrkeza marekebisho na sio kutishana kwa kutangaziana Utakatifu ili tushindwe kukosoa na kurekebisha makosa.

Pitia kitabu Kilichoandikwa na S Mwijage 'The Dark Side of Julius Nyerere' Kilipigwa Marufuku.

Soma kitabu kingine ''Julius Nyerere :The Servant of God or Untarnished Tyrant''.Tusitishane ,tusizoeshane unafiki.Call spade a spade not a big spoon.Sasa nilivisoma na wanikamate kama watavifuta kichwanj mwangu na nahamasisha wengine wavisome soft copy.walisahau kuwa hii ni digital.Unapiga marufuku hard Copy huna uwezo wa kuzuia Soft Copy.

Jambo jingine Muhimu kuweka Kumbukumbu sawa mimi sio miongoni mwa watu wa Kilimanjaro ambao Mzee Agustine Lyatonga Mrema anadai walimtuma kuwa wanataka serikali 2.Yeye sio Msemaji wa Wachaga wala watu wa Kilimanjaro.He should speak for himself.

Wazee wanafiki kama hawa tukiwajibu ipasavyo wanaishia kutishia kutoa laana ovyo ovyo kwa mambo waliojitakia wenyewe.Wajiheshimu

Sitatoa majibu kama ya wale wahuni wa UVCCM waliodai Mzee Warioba atakufa kesho.Huko ni Kuingilia kazi ya Mungu. Tuheshimiane katika mijadala hii na tuache unafiki.Tunaitaka Tanganyika na tuna hoja nzito.Amri ya Kidikteta ya mwaka 1964 haiwezi kutuburuza watanganyika Wote na kuandika historia kwa misingi ya mawazo ya kiimla ya Mtu mmoja.Mimi sitakua mmojawapo.Tanganyika iuawe kwa maoni ya Watu wa Tanganyika na sio Uimla wa mtu mmoja.

well said mkuu Tanganyika haikuwa property binafsi ya nyerere hvo alikuwa hana mamlaka yyte kuiamulia fate yke au kuiterminate ni aibu kwa watu zaidi ya milioni 40 kuendelea kuongozwa na maamuz hayo yaliyoamuliwa na mtu mmoja ikiwa ni miaka 50 iliyopita
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti. Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea. KAzi njema.

Wee Pita zako hivi..
 
Kuna uadilifu gani kwa Lissu kumuita Nyerere ni Tapeli, na Muungao ni batili halafu hajawahi muchallenge Nyerere akiwa hai, wala huo muungao kortini?

Ukweli kusema hati ya muungano haipo wakati hata mtoto wa darasa la pili mwenye kuweza kupambanua mambo anaweza jua huo ni upuuzi?Hivi wewe miaka yako uliyoishi duniani unaamini kabisa kuwa hati ya muungano haipo?kuna tofauti kubwa ya ukweli na shutuma. Shutuma kila mtu anaweza kuzitoa. Naichukia sana CCM kwa matatizo yaliyokuwepo hapo nyumbani lakini sio kwa kutukana watu hovyo.

Huyo Nyerere mnayemtukana yuko wapi kujitetea?where is dignity?where is sense rationality? Wanachokifanya CDM sasa kina faida ipi kwa taifa?kuwaambia watu Nyerere alikuwa Tapeli kunasaidia vipi kupatikana kwa katiba bora?

Go back read my 600+ posts utaelewa nasimamia wapi, shutuma unazozitoa hapa na anachofanya Lissu, hakina tofauti, Unfounded nonsense based on heat of the moment. Kwa lugha nyepesi, tunaita hot headness.

Mkuu,
Bado sijajua ni kitu gani unataka kuzungumza!

Kwanza kabisa hakuna mahali popote ambapo Lissu amemuita Mwl Nyerere tapeli HAKUNA!

Pili,hoja ya kwamba Tundu Lissu hakupaswa kumkosoa Mwl Nyerere akiwa ameshakufa ni hoja ya KITOTO sana,kwani kila mtu alizaliwa Mwl Nyerere akiwa hai?Lakini madhara ya maamuzi yake si yapo mpaka leo?

Na pia suala la hati ya muungano kuwapo au kutokuwa Lissu alilizungumzia vizuri tu,lkn watu wengi naona mnajaribu kupotosha!Alisema hati ya muungano haipo na kama IPO muungano ni batili kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa kwenye KUUNDA muungano huo!Kuna tatizo gani kusema hayo?

Halafu pia watu mmeng'ang'ania AMETUKANA!! AMETUKANA!! mbona hayo matusi sie hatujayaona?

Kuna matusi gani kwenye hoja hizi hapa chini;

................................




d) Katika kitabu chake kiitwacho 50 Years of Independence: A ConcisePolitical History of Tanzania, kilichochapishwa Januari ya mwaka huu 2014, MzeePius Msekwa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Katibu Mtendaji wake wa kwanzaamesema yafuatayo kuhusu mambo yaliyofanyika baada ya Makubaliano ya Muunganokusainiwa:
(i) Tarehe 26 Aprili, 1964, yaani Siku ya Muungano, Rais Nyerere alitungaPresidential Decree (Amri ya Rais) iliyoitwa The Transitional ProvisionsDecree, 1964, yaani, Amri ya Masharti ya Mpito ya mwaka 1964, iliyochapishwakatika Gazeti la Serikali la siku hiyo. “Amri hiyo iliwabadilisha watuwaliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na kuwafanya watumishiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwaMahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano; na nembo ya taifa ya Jamhuri ya Tanganyikailigeuzwa kuwa nembo ya taifa ya Jamhuri ya Muungano.”
(ii) Tarehe hiyo hiyo, Rais Nyerere alitunga Amri nyingine ya Rais iliyoitwaThe Interim Constitution Decree, 1964, yaani, Amri ya Katiba ya Muda ya mwaka1964. “Amri hii iliitangaza Katiba ya Tanganyika kuwa ndiyo Katiba ya Muda yaJamhuri ya Muungano. Kifungu cha 4 cha Amri hii ndicho kilichoipatia Serikaliya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muunganoyote na vile vile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika.”
(iii) Tarehe 15 Juni 1964 Mwalimu Nyerere alitunga Amri nyingine tena iliyoitwaThe Transitional Provisions (No. 2) Decree, 1964, yaani, Amri ya Masharti yaMpito (Na. 2) ya mwaka 1964. Amri hii ilielekeza kwamba mahali popote ambaposheria zilizopo zimetaja jina la ‘Tanganyika’ basi jina hilo lifutwe na badalayake jina la ‘Jamhuri ya Muungano’ liwekwe. Vile vile, Amri hiyo ilielekeza,mahali popote ambapo ‘Serikali ya Tanganyika’ imetajwa, au kwenye jambo au kituchochote ambacho kwa namna yoyote kinamilikiwa au kinahusishwa na Serikalihiyo, basi itachukuliwa kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyoiliyotajwa.
(iv) Kwa maneno ya Mzee Msekwa mwenyewe: “Tanganyika was thus decreed out ofexistence. The cumulative effect of these legislative measures was that thepolitical entity which was Tanganyika, was decreed totally out of existence.That is the reason why even the name of the geographical unit formerly known asTanganyika, had to be changed to Tanzania Mainland.” Tafsiri ya maneno haya nikwamba “uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla zaAmri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndio ilikuwa Tanganyika lilitolewauhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo lakijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwaTanzania Bara.”
2. Vitendo vya kuivika Jamhuri ya Tanganyika joho la Muungano na kuigeuza kuwandio Jamhuri ya Muungano hakikuwa na uhalali wowote kwa mujibu wa Makubalianoya Muungano:
(a) Aya ya (v) ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ilitamka wazi kwamba “sheriazilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutiliwa nguvu katika maeneoyao....” Kwa maana hiyo:
(i) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganowala chini ya Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza sheria zote za Jamhuriya Tanganyika kuwa sheria za Jamhuri ya Muungano hata kwa mambo yasiyokuwa yaMuungano;
(ii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano wala kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kuwageuzawatumishi wote wa Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Jamhuri ya Muunganohata kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano;
(iii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza MahakamaKuu ya Tanganyika kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano;
(iv) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa Nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.Nembo za Taifa, yaani ‘Bibi na Bwana’ inayotumika hadi leo hii ni Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika!
(v) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganoau kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kufuta matumizi ya jina laTanganyika katika sheria zote za Jamhuri ya Tanganyika au katika mambo au vituvyote vilivyokuwa vinamilikiwa ama kuhusishwa na Jamhuri ya Tanganyika hata kwamambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika;
(vi) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya ‘kutoa uhai wa nchiya Tanganyika kwa njia ya Amri ya Rais’ au kwa njia nyingine yoyote ya kisheriana kuigeuza kuwa Jamhuri ya Muungano.


...............................


Kuna matusi yoyote hapa?

Mie nafikiri kuna watu mnamuona Nyerere kama Mungu mtu!

hakosolewi,

haguswi,

hasemwi,

hachunguzwi,

....wakati si ajabu wengi wenu UJAMAA mumeuua,AZIMIO LA ARUSHA mmelisahau, na hata yawezekana ndio mawakala wakubwa wa MAFISADI!!!

Kama umeumia sana na maneno ya TUNDU LISSU ungewasaidia wenzio kujibu hoja hizo NZITO za TUNDU LISSU badala ya kuleta PROPAGANDA!!

JIBUNI HOJA ,ACHENI UNAFIQ!!


NA TANGANYIKA YETU LAZIMA MUILETE!!!

MTANGANYIKA DAIMA
 
Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.

Sidhani kama kuna ukweli wowote wa kusema nyerere hakua mtu wa kawaida, ambacho alijahariwa ni kuweza kudadisi mambo na kuyafikiri kwa kina ingawa hata yale aliyokua anayakosea ubabe ndo ulikua unamuokoa, kinachokosewa na nyinyi m ni hiki hawasomi, hawajui, hawadadisi mambo na wanataka kuwa kama nyerere ni lazima watu smart kama lisu watawahumbua na wenye akili finyu watamini kama lisu mropokaji.
 
Kimsingi mtu mwenye akiri na muona mbali hujibu kwa hoja na si maneno ya shombo kama wengine mjibuvyo. uko sawa ben.
 
Hapo sawa kabisa, kwa kulopoka kwao na kutofikiri kimsingi na kiupana wanaisi lisu kawatusi, alafu kingine nashangaa wa2 wote mnaoisi lisu katukana mbona hamna Facts za kutosha na Ushawishi wenye visibitisho ili watanganyika tuwaelewe? Nchi yetu Kama mlizoea dezo jua mwisho wenu unakaribia kama sio kuisha.
 
Mwl. Nyerere alikuwa binadamu na alifanya makosa mengi ya kutokujua na ya makusudi kwahyo tusipoteze muda kumtetea na kamanda Lisu amemaliza kazi! Nadhan sasa wanaong'ang'ania serikal 2 waone aibu na wapige hatua 5 tu za kufikiria kama kweli ni wasomi.
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti. Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea. KAzi njema.

Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.


Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA.
 
Kwa kauli izo za Tundu Lissu ni sawa na kumwambia baba yake hajui kutomba........sasa ajiulize alimzaa vp
 
Mkuu,
Bado sijajua ni kitu gani unataka kuzungumza!

Kwanza kabisa hakuna mahali popote ambapo Lissu amemuita Mwl Nyerere tapeli HAKUNA!

Pili,hoja ya kwamba Tundu Lissu hakupaswa kumkosoa Mwl Nyerere akiwa ameshakufa ni hoja ya KITOTO sana,kwani kila mtu alizaliwa Mwl Nyerere akiwa hai?Lakini madhara ya maamuzi yake si yapo mpaka leo?

Na pia suala la hati ya muungano kuwapo au kutokuwa Lissu alilizungumzia vizuri tu,lkn watu wengi naona mnajaribu kupotosha!Alisema hati ya muungano haipo na kama IPO muungano ni batili kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa kwenye KUUNDA muungano huo!Kuna tatizo gani kusema hayo?

Halafu pia watu mmeng'ang'ania AMETUKANA!! AMETUKANA!! mbona hayo matusi sie hatujayaona?

Kuna matusi gani kwenye hoja hizi hapa chini;

................................




d) Katika kitabu chake kiitwacho 50 Years of Independence: A ConcisePolitical History of Tanzania, kilichochapishwa Januari ya mwaka huu 2014, MzeePius Msekwa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Katibu Mtendaji wake wa kwanzaamesema yafuatayo kuhusu mambo yaliyofanyika baada ya Makubaliano ya Muunganokusainiwa:
(i) Tarehe 26 Aprili, 1964, yaani Siku ya Muungano, Rais Nyerere alitungaPresidential Decree (Amri ya Rais) iliyoitwa The Transitional ProvisionsDecree, 1964, yaani, Amri ya Masharti ya Mpito ya mwaka 1964, iliyochapishwakatika Gazeti la Serikali la siku hiyo. "Amri hiyo iliwabadilisha watuwaliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na kuwafanya watumishiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwaMahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano; na nembo ya taifa ya Jamhuri ya Tanganyikailigeuzwa kuwa nembo ya taifa ya Jamhuri ya Muungano."
(ii) Tarehe hiyo hiyo, Rais Nyerere alitunga Amri nyingine ya Rais iliyoitwaThe Interim Constitution Decree, 1964, yaani, Amri ya Katiba ya Muda ya mwaka1964. "Amri hii iliitangaza Katiba ya Tanganyika kuwa ndiyo Katiba ya Muda yaJamhuri ya Muungano. Kifungu cha 4 cha Amri hii ndicho kilichoipatia Serikaliya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muunganoyote na vile vile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika."
(iii) Tarehe 15 Juni 1964 Mwalimu Nyerere alitunga Amri nyingine tena iliyoitwaThe Transitional Provisions (No. 2) Decree, 1964, yaani, Amri ya Masharti yaMpito (Na. 2) ya mwaka 1964. Amri hii ilielekeza kwamba mahali popote ambaposheria zilizopo zimetaja jina la ‘Tanganyika' basi jina hilo lifutwe na badalayake jina la ‘Jamhuri ya Muungano' liwekwe. Vile vile, Amri hiyo ilielekeza,mahali popote ambapo ‘Serikali ya Tanganyika' imetajwa, au kwenye jambo au kituchochote ambacho kwa namna yoyote kinamilikiwa au kinahusishwa na Serikalihiyo, basi itachukuliwa kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyoiliyotajwa.
(iv) Kwa maneno ya Mzee Msekwa mwenyewe: "Tanganyika was thus decreed out ofexistence. The cumulative effect of these legislative measures was that thepolitical entity which was Tanganyika, was decreed totally out of existence.That is the reason why even the name of the geographical unit formerly known asTanganyika, had to be changed to Tanzania Mainland." Tafsiri ya maneno haya nikwamba "uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla zaAmri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndio ilikuwa Tanganyika lilitolewauhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo lakijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwaTanzania Bara."
2. Vitendo vya kuivika Jamhuri ya Tanganyika joho la Muungano na kuigeuza kuwandio Jamhuri ya Muungano hakikuwa na uhalali wowote kwa mujibu wa Makubalianoya Muungano:
(a) Aya ya (v) ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ilitamka wazi kwamba "sheriazilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutiliwa nguvu katika maeneoyao...." Kwa maana hiyo:
(i) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganowala chini ya Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza sheria zote za Jamhuriya Tanganyika kuwa sheria za Jamhuri ya Muungano hata kwa mambo yasiyokuwa yaMuungano;
(ii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano wala kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kuwageuzawatumishi wote wa Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Jamhuri ya Muunganohata kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano;
(iii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza MahakamaKuu ya Tanganyika kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano;
(iv) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa Nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.Nembo za Taifa, yaani ‘Bibi na Bwana' inayotumika hadi leo hii ni Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika!
(v) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganoau kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kufuta matumizi ya jina laTanganyika katika sheria zote za Jamhuri ya Tanganyika au katika mambo au vituvyote vilivyokuwa vinamilikiwa ama kuhusishwa na Jamhuri ya Tanganyika hata kwamambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika;
(vi) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya ‘kutoa uhai wa nchiya Tanganyika kwa njia ya Amri ya Rais' au kwa njia nyingine yoyote ya kisheriana kuigeuza kuwa Jamhuri ya Muungano.


...............................


Kuna matusi yoyote hapa?

Mie nafikiri kuna watu mnamuona Nyerere kama Mungu mtu!

hakosolewi,

haguswi,

hasemwi,

hachunguzwi,

....wakati si ajabu wengi wenu UJAMAA mumeuua,AZIMIO LA ARUSHA mmelisahau, na hata yawezekana ndio mawakala wakubwa wa MAFISADI!!!

Kama umeumia sana na maneno ya TUNDU LISSU ungewasaidia wenzio kujibu hoja hizo NZITO za TUNDU LISSU badala ya kuleta PROPAGANDA!!

JIBUNI HOJA ,ACHENI UNAFIQ!!


NA TANGANYIKA YETU LAZIMA MUILETE!!!

MTANGANYIKA DAIMA

kama unaamini kauli za Lisu kuhusu Nyerere ni kauli za kistaarabu, basi ama wewe ni Lissu mwenyewe au unashabihiana nae kwa ukaribu sana. Kama mimi ningekuwa Lissu, ningesema hata nimekuwa"quoted" out of context. Morinho alimuta eto babu lakini aakaomba 'radhi' ki-mourinho kwa kusema yale aliyoyasema hayakupaswa kuwekwa wazi.

Hivyo vifungu unavinukuu hapo juu kwa sababu ya elimu ambayo huyo mchonga alipigania kwa njia halali na Haramu uipate wewe na kizazi chako.SMH
 
Nakubaliana kabisa na ndugu Ng'wamapalala kwamba kuna mapungufu ya fikara kwa baadhi ya wabunge, kama Mheshimiwa Tundu Lisu. Nyerere alikuwa kiongozi aliyejua kazi na nafasi yake Katika jamii. Siku zote alijua kuongoza na kutawala watu ni kusimamia kwa uadilifu taratibu na kanuni Ilizowekwa; kama katiba na sharia za nchi. Kusimamia taratibu na kanuni ni kuwafikia ha kila mhusika, bila una guide, anazingatia utekelezaji na anayekiuka anachukuliwa hatua site hiking. Hilo ndilo Nyerere alikuwa akiyanya alipowachukulia hatua wote waliojaribu kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inaelekea Tundu ni mwanasheria asiyejua, au aaiyethamini utawala wa sharia. Umuhunyari.
 
Kwa kuongezea, watu wengi humu hawamfahamu Mao Zedong, huyu bwana alikuwa mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha china, na raisi wao kwa kipindi kirefu mara baada ya mapinduzi ya miaka ya 40.
Huyu bwana amefanya mambo mengi sana sana china, hakuna mchina ambaye hajawa affected na maamuzi yake, na asilimia kubwa mno, si watu kumi au ishirini, mamilioni ya watu wasiopungua milioni 300 na kuendelea walipata shida sana wakati wa utawala wa huyu bwana. Alikuwa dikteta kamili, alikuw ani sheria, alikuwa ni alfa na omega. Watu wengi sana walimchukia ndani ya China.

Sasa kilichotokea baada ya Kufariki wale waliokuwa wanamchukia wakachukua hatamu, kundi la shanghai la kina Deng Xiaoping na wenzie, hawa mabwana walipata shida sana wakati wa Mao, kwani sera zao hazikupewa nafasi.

Baada ya deng Xiaoping kuchukua nchi akatangaza "Gaiga Kaifang", aka the great opening to the world. China ikaanza kufungua milango yake kwa dunia, ikaanza michakato ya kujiunga IMF n.k.

Hayo yote yakiendelea,ambayo yalikuwa kinyume na wakati wa MAO, Wachina hawakuwahi kumtukana MAO hadharani, hakuna mwanasiasa anayethubutu kumsema vibaya Mao, hata Deng Xiaoping mwenyewe hakuwa na Mafua hayo, kwani Mao alipendwa na watu wengi Mno China, aliwapa wachina kitu kinaitwa sense of security and pride as a nation baada ya kipindi kirefu cha mateso ya wajapani na washirika 7 walioivamia china. Wachina walikuwa tayari ku-sacrifice maisha yao kutimiza Vision ya Mao.

Deng Xiaoping na Timu yake kwa kuwa hawakuwa Vichaa kama kina lisu, waliendelea Kuyatukuza mema ya Mao, na mchanganyiko huu wa mema ya Mao na Mema ya Deng Xiaoping Ndio unaifanya China iwe Taifa linaloogopeka Dunia nzima.

Deng Xiaoping aliendeleza mkono wa chuma alioachiwa na Mao huku akitoa uhuru wa kiuchumi kwa wananchi wake kwa awamu. Miaka 40 toka Mao afariki, wachina wengi waliokuwa hawampendi Mao sasa wanampenda kuliko ilivyokuwa awali, wameelewa sacrifice alizozifanya kwa taifa ili kuwepo na usawa, heshima, nidhamu na mafanikio kwa kila mmoja. Wengi waliompenda Deng Xiaoping hapo mwanzoni, sasa hawawapendi "protege" wake ambao walichukua sera za Deng Xiaoping pure bila kuchanganya na za Mao.

Ukisoma kwa makini utagundua kuwa kati ya hawa viongozi wawili, kila mmoja alifanya makubwa mema, na kila mmoja alikosea kwingi, lakini nia yao kuu ilikuwa kuifanya China iwe sehemu bora kwa kila Mchina. Hakuna upande uliowaita wenzie Matapeli, kwa kuwa wote wamejaaliwa busara. Sera walizotofautiana wanazirekebisha kistaarabu na kubalance kwa manufaa ya wote.

Huyu Nyerere mnayemtukana ndio ametengeneza amani iliyokuwepo sasa, ndio aliyetumia udikteta wake kulinda mipaka ya Tanzania ilipovamiwa, ndio alitumia udikteta wake kuwafanya mabeberu watuheshimu na umasikini wetu, ingawa heshima hiyo inaanza kutoweka kwa kasi, ndio alifanya kila awezalo kwa uwezo wake kuhakikisha elimu inakuwa bure kwa wote, mpaka hao kina Lisu, Slaa, na wazazi wako wewe wakasoma bila shida.

Leo hii kuna Mpuuzi anasimama Bungeni na kumuita Tapeli?seriously?

- Saafi sana hatimaye wazee wa zamani wa JF mmeanza kujitokeza naona mmeona hawa watoto wanakwenda mbali sana na matusi kwa Taifa, kaka wape darasa hawa watoto wadogo wasiojua kitu huu mjadala mimi nakuachia mkuu nakuaminia sana!!

ES
 
Huyu jamaa kweli nimeamini ni mgonjwa wa akili.
Source: Kigwangala
 
Back
Top Bottom