Kuna uadilifu gani kwa Lissu kumuita Nyerere ni Tapeli, na Muungao ni batili halafu hajawahi muchallenge Nyerere akiwa hai, wala huo muungao kortini?
Ukweli kusema hati ya muungano haipo wakati hata mtoto wa darasa la pili mwenye kuweza kupambanua mambo anaweza jua huo ni upuuzi?Hivi wewe miaka yako uliyoishi duniani unaamini kabisa kuwa hati ya muungano haipo?kuna tofauti kubwa ya ukweli na shutuma. Shutuma kila mtu anaweza kuzitoa. Naichukia sana CCM kwa matatizo yaliyokuwepo hapo nyumbani lakini sio kwa kutukana watu hovyo.
Huyo Nyerere mnayemtukana yuko wapi kujitetea?where is dignity?where is sense rationality? Wanachokifanya CDM sasa kina faida ipi kwa taifa?kuwaambia watu Nyerere alikuwa Tapeli kunasaidia vipi kupatikana kwa katiba bora?
Go back read my 600+ posts utaelewa nasimamia wapi, shutuma unazozitoa hapa na anachofanya Lissu, hakina tofauti, Unfounded nonsense based on heat of the moment. Kwa lugha nyepesi, tunaita hot headness.
Mkuu,
Bado sijajua ni kitu gani unataka kuzungumza!
Kwanza kabisa hakuna mahali popote ambapo Lissu amemuita Mwl Nyerere tapeli HAKUNA!
Pili,hoja ya kwamba Tundu Lissu hakupaswa kumkosoa Mwl Nyerere akiwa ameshakufa ni hoja ya KITOTO sana,kwani kila mtu alizaliwa Mwl Nyerere akiwa hai?Lakini madhara ya maamuzi yake si yapo mpaka leo?
Na pia suala la hati ya muungano kuwapo au kutokuwa Lissu alilizungumzia vizuri tu,lkn watu wengi naona mnajaribu kupotosha!Alisema hati ya muungano haipo na kama IPO muungano ni batili kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa kwenye KUUNDA muungano huo!Kuna tatizo gani kusema hayo?
Halafu pia watu mmeng'ang'ania AMETUKANA!! AMETUKANA!! mbona hayo matusi sie hatujayaona?
Kuna matusi gani kwenye hoja hizi hapa chini;
................................
d) Katika kitabu chake kiitwacho 50 Years of Independence: A ConcisePolitical History of Tanzania, kilichochapishwa Januari ya mwaka huu 2014, MzeePius Msekwa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Katibu Mtendaji wake wa kwanzaamesema yafuatayo kuhusu mambo yaliyofanyika baada ya Makubaliano ya Muunganokusainiwa:
(i) Tarehe 26 Aprili, 1964, yaani Siku ya Muungano, Rais Nyerere alitungaPresidential Decree (Amri ya Rais) iliyoitwa The Transitional ProvisionsDecree, 1964, yaani, Amri ya Masharti ya Mpito ya mwaka 1964, iliyochapishwakatika Gazeti la Serikali la siku hiyo. Amri hiyo iliwabadilisha watuwaliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na kuwafanya watumishiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwaMahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano; na nembo ya taifa ya Jamhuri ya Tanganyikailigeuzwa kuwa nembo ya taifa ya Jamhuri ya Muungano.
(ii) Tarehe hiyo hiyo, Rais Nyerere alitunga Amri nyingine ya Rais iliyoitwaThe Interim Constitution Decree, 1964, yaani, Amri ya Katiba ya Muda ya mwaka1964. Amri hii iliitangaza Katiba ya Tanganyika kuwa ndiyo Katiba ya Muda yaJamhuri ya Muungano. Kifungu cha 4 cha Amri hii ndicho kilichoipatia Serikaliya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muunganoyote na vile vile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika.
(iii) Tarehe 15 Juni 1964 Mwalimu Nyerere alitunga Amri nyingine tena iliyoitwaThe Transitional Provisions (No. 2) Decree, 1964, yaani, Amri ya Masharti yaMpito (Na. 2) ya mwaka 1964. Amri hii ilielekeza kwamba mahali popote ambaposheria zilizopo zimetaja jina la Tanganyika basi jina hilo lifutwe na badalayake jina la Jamhuri ya Muungano liwekwe. Vile vile, Amri hiyo ilielekeza,mahali popote ambapo Serikali ya Tanganyika imetajwa, au kwenye jambo au kituchochote ambacho kwa namna yoyote kinamilikiwa au kinahusishwa na Serikalihiyo, basi itachukuliwa kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyoiliyotajwa.
(iv) Kwa maneno ya Mzee Msekwa mwenyewe: Tanganyika was thus decreed out ofexistence. The cumulative effect of these legislative measures was that thepolitical entity which was Tanganyika, was decreed totally out of existence.That is the reason why even the name of the geographical unit formerly known asTanganyika, had to be changed to Tanzania Mainland. Tafsiri ya maneno haya nikwamba uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla zaAmri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndio ilikuwa Tanganyika lilitolewauhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo lakijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwaTanzania Bara.
2. Vitendo vya kuivika Jamhuri ya Tanganyika joho la Muungano na kuigeuza kuwandio Jamhuri ya Muungano hakikuwa na uhalali wowote kwa mujibu wa Makubalianoya Muungano:
(a) Aya ya (v) ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ilitamka wazi kwamba sheriazilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutiliwa nguvu katika maeneoyao.... Kwa maana hiyo:
(i) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganowala chini ya Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza sheria zote za Jamhuriya Tanganyika kuwa sheria za Jamhuri ya Muungano hata kwa mambo yasiyokuwa yaMuungano;
(ii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano wala kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kuwageuzawatumishi wote wa Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Jamhuri ya Muunganohata kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano;
(iii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza MahakamaKuu ya Tanganyika kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano;
(iv) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa Nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.Nembo za Taifa, yaani Bibi na Bwana inayotumika hadi leo hii ni Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika!
(v) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganoau kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kufuta matumizi ya jina laTanganyika katika sheria zote za Jamhuri ya Tanganyika au katika mambo au vituvyote vilivyokuwa vinamilikiwa ama kuhusishwa na Jamhuri ya Tanganyika hata kwamambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika;
(vi) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kutoa uhai wa nchiya Tanganyika kwa njia ya Amri ya Rais au kwa njia nyingine yoyote ya kisheriana kuigeuza kuwa Jamhuri ya Muungano.
...............................
Kuna matusi yoyote hapa?
Mie nafikiri kuna watu mnamuona Nyerere kama Mungu mtu!
hakosolewi,
haguswi,
hasemwi,
hachunguzwi,
....wakati si ajabu wengi wenu UJAMAA mumeuua,AZIMIO LA ARUSHA mmelisahau, na hata yawezekana ndio mawakala wakubwa wa MAFISADI!!!
Kama umeumia sana na maneno ya TUNDU LISSU ungewasaidia wenzio kujibu hoja hizo NZITO za TUNDU LISSU badala ya kuleta PROPAGANDA!!
JIBUNI HOJA ,ACHENI UNAFIQ!!
NA TANGANYIKA YETU LAZIMA MUILETE!!!
MTANGANYIKA DAIMA