Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

chogomzingwi Haya hiyo hati imeongeza au kupunguza nini? By the way sikuwa nna shida nayo. Naamini muungano Upo sikuhitaji hati. Kama nnavyoamini kuwa baba na mama yangu ni Mke na mume. Sihitaji cheti Chao cha ndoa.

angalau imetujuza tabia za viongozi wa ccm na serikali yetu,unakumbuka majibu yaliyokuwa yakitolewa kabla ya hiyo hati kutolewa?.
 
Last edited by a moderator:

Kuna uadilifu gani kwa Lissu kumuita Nyerere ni Tapeli, na Muungao ni batili halafu hajawahi muchallenge Nyerere akiwa hai, wala huo muungao kortini?

Ukweli kusema hati ya muungano haipo wakati hata mtoto wa darasa la pili mwenye kuweza kupambanua mambo anaweza jua huo ni upuuzi?Hivi wewe miaka yako uliyoishi duniani unaamini kabisa kuwa hati ya muungano haipo?kuna tofauti kubwa ya ukweli na shutuma. Shutuma kila mtu anaweza kuzitoa. Naichukia sana CCM kwa matatizo yaliyokuwepo hapo nyumbani lakini sio kwa kutukana watu hovyo.

Huyo Nyerere mnayemtukana yuko wapi kujitetea?where is dignity?where is sense rationality? Wanachokifanya CDM sasa kina faida ipi kwa taifa?kuwaambia watu Nyerere alikuwa Tapeli kunasaidia vipi kupatikana kwa katiba bora?

Go back read my 600+ posts utaelewa nasimamia wapi, shutuma unazozitoa hapa na anachofanya Lissu, hakina tofauti, Unfounded nonsense based on heat of the moment. Kwa lugha nyepesi, tunaita hot headness.
 
Jamaa kaanzisha thread halafu faster kasepa, nadhani alikuwa anapima kina cha maji
 
Upeo mdogo wa uelewa ndiyo sababu ya kumuona Tundu Lisu katuma,ni Viongozi wangapi wa CCM wenye uwezo wa kusimama na kuwaambia wananchi ukweli wa mikataba na pesa wanazopiga daily?
Sipo upande wowote wa chama lia kwa la Tundu Lisu nampa big up kuelezea ukweli halisi na ndiyo maana hadi kesho CCm wanalilia kinga ya raisi ili hata akifanya madudu na genge lake alindwe na kupewa heshima tuu.
Hapo maisha ya ndiyo mzee yamepitwa,tunaitaji hoja zilizotukuka kwa manufaa ya nchi yetu.
 
huu hauwezi kuwa uchangiaji wa mtu makini.,

Nisema tayari, ninasema tena Lazima tujifunze staha na kuvumiliana,. Matusi haya jengi nchi!

Siasa za upinzani nchi hii za ajabu sana, hazina malengo ya uungwaki mkono ili wakubalike na wengi, siasa zao ni za kuongeza maadui. Inashangaza kuona wawadhihaki na kuwakashifu watu ambao kesho watawaomba na kuwahitaji ili wafanikishe malengo yao kisiasa. Angalia ndani ya bunge leo, uungwaji hoja ni wa 2/3 miongoni mwao lakini wanawatukana, wanawakashifu wajumbe wanaowahitaji kesho! kan kwamba hoja zao zitapita kwa mabavu!!!
 

well said mkuu Tanganyika haikuwa property binafsi ya nyerere hvo alikuwa hana mamlaka yyte kuiamulia fate yke au kuiterminate ni aibu kwa watu zaidi ya milioni 40 kuendelea kuongozwa na maamuz hayo yaliyoamuliwa na mtu mmoja ikiwa ni miaka 50 iliyopita
 

Wee Pita zako hivi..
 

Mkuu,
Bado sijajua ni kitu gani unataka kuzungumza!

Kwanza kabisa hakuna mahali popote ambapo Lissu amemuita Mwl Nyerere tapeli HAKUNA!

Pili,hoja ya kwamba Tundu Lissu hakupaswa kumkosoa Mwl Nyerere akiwa ameshakufa ni hoja ya KITOTO sana,kwani kila mtu alizaliwa Mwl Nyerere akiwa hai?Lakini madhara ya maamuzi yake si yapo mpaka leo?

Na pia suala la hati ya muungano kuwapo au kutokuwa Lissu alilizungumzia vizuri tu,lkn watu wengi naona mnajaribu kupotosha!Alisema hati ya muungano haipo na kama IPO muungano ni batili kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa kwenye KUUNDA muungano huo!Kuna tatizo gani kusema hayo?

Halafu pia watu mmeng'ang'ania AMETUKANA!! AMETUKANA!! mbona hayo matusi sie hatujayaona?

Kuna matusi gani kwenye hoja hizi hapa chini;

................................




d) Katika kitabu chake kiitwacho 50 Years of Independence: A ConcisePolitical History of Tanzania, kilichochapishwa Januari ya mwaka huu 2014, MzeePius Msekwa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM na Katibu Mtendaji wake wa kwanzaamesema yafuatayo kuhusu mambo yaliyofanyika baada ya Makubaliano ya Muunganokusainiwa:
(i) Tarehe 26 Aprili, 1964, yaani Siku ya Muungano, Rais Nyerere alitungaPresidential Decree (Amri ya Rais) iliyoitwa The Transitional ProvisionsDecree, 1964, yaani, Amri ya Masharti ya Mpito ya mwaka 1964, iliyochapishwakatika Gazeti la Serikali la siku hiyo. “Amri hiyo iliwabadilisha watuwaliokuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na kuwafanya watumishiwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwaMahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano; na nembo ya taifa ya Jamhuri ya Tanganyikailigeuzwa kuwa nembo ya taifa ya Jamhuri ya Muungano.”
(ii) Tarehe hiyo hiyo, Rais Nyerere alitunga Amri nyingine ya Rais iliyoitwaThe Interim Constitution Decree, 1964, yaani, Amri ya Katiba ya Muda ya mwaka1964. “Amri hii iliitangaza Katiba ya Tanganyika kuwa ndiyo Katiba ya Muda yaJamhuri ya Muungano. Kifungu cha 4 cha Amri hii ndicho kilichoipatia Serikaliya Muungano majukumu kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muunganoyote na vile vile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika.”
(iii) Tarehe 15 Juni 1964 Mwalimu Nyerere alitunga Amri nyingine tena iliyoitwaThe Transitional Provisions (No. 2) Decree, 1964, yaani, Amri ya Masharti yaMpito (Na. 2) ya mwaka 1964. Amri hii ilielekeza kwamba mahali popote ambaposheria zilizopo zimetaja jina la ‘Tanganyika’ basi jina hilo lifutwe na badalayake jina la ‘Jamhuri ya Muungano’ liwekwe. Vile vile, Amri hiyo ilielekeza,mahali popote ambapo ‘Serikali ya Tanganyika’ imetajwa, au kwenye jambo au kituchochote ambacho kwa namna yoyote kinamilikiwa au kinahusishwa na Serikalihiyo, basi itachukuliwa kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyoiliyotajwa.
(iv) Kwa maneno ya Mzee Msekwa mwenyewe: “Tanganyika was thus decreed out ofexistence. The cumulative effect of these legislative measures was that thepolitical entity which was Tanganyika, was decreed totally out of existence.That is the reason why even the name of the geographical unit formerly known asTanganyika, had to be changed to Tanzania Mainland.” Tafsiri ya maneno haya nikwamba “uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za jumla zaAmri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndio ilikuwa Tanganyika lilitolewauhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu hata jina la eneo lakijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika ilibidi libadilishwe na kuwaTanzania Bara.”
2. Vitendo vya kuivika Jamhuri ya Tanganyika joho la Muungano na kuigeuza kuwandio Jamhuri ya Muungano hakikuwa na uhalali wowote kwa mujibu wa Makubalianoya Muungano:
(a) Aya ya (v) ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ilitamka wazi kwamba “sheriazilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutiliwa nguvu katika maeneoyao....” Kwa maana hiyo:
(i) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganowala chini ya Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza sheria zote za Jamhuriya Tanganyika kuwa sheria za Jamhuri ya Muungano hata kwa mambo yasiyokuwa yaMuungano;
(ii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano wala kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kuwageuzawatumishi wote wa Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Jamhuri ya Muunganohata kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano;
(iii) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza MahakamaKuu ya Tanganyika kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano;
(iv) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kugeuza Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa Nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.Nembo za Taifa, yaani ‘Bibi na Bwana’ inayotumika hadi leo hii ni Nembo yaTaifa ya Jamhuri ya Tanganyika!
(v) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano ya Muunganoau kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya kufuta matumizi ya jina laTanganyika katika sheria zote za Jamhuri ya Tanganyika au katika mambo au vituvyote vilivyokuwa vinamilikiwa ama kuhusishwa na Jamhuri ya Tanganyika hata kwamambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika;
(vi) Rais Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote kwa mujibu wa Makubaliano yaMuungano au kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanganyika ya ‘kutoa uhai wa nchiya Tanganyika kwa njia ya Amri ya Rais’ au kwa njia nyingine yoyote ya kisheriana kuigeuza kuwa Jamhuri ya Muungano.


...............................


Kuna matusi yoyote hapa?

Mie nafikiri kuna watu mnamuona Nyerere kama Mungu mtu!

hakosolewi,

haguswi,

hasemwi,

hachunguzwi,

....wakati si ajabu wengi wenu UJAMAA mumeuua,AZIMIO LA ARUSHA mmelisahau, na hata yawezekana ndio mawakala wakubwa wa MAFISADI!!!

Kama umeumia sana na maneno ya TUNDU LISSU ungewasaidia wenzio kujibu hoja hizo NZITO za TUNDU LISSU badala ya kuleta PROPAGANDA!!

JIBUNI HOJA ,ACHENI UNAFIQ!!


NA TANGANYIKA YETU LAZIMA MUILETE!!!

MTANGANYIKA DAIMA
 
Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.

Sidhani kama kuna ukweli wowote wa kusema nyerere hakua mtu wa kawaida, ambacho alijahariwa ni kuweza kudadisi mambo na kuyafikiri kwa kina ingawa hata yale aliyokua anayakosea ubabe ndo ulikua unamuokoa, kinachokosewa na nyinyi m ni hiki hawasomi, hawajui, hawadadisi mambo na wanataka kuwa kama nyerere ni lazima watu smart kama lisu watawahumbua na wenye akili finyu watamini kama lisu mropokaji.
 
Kimsingi mtu mwenye akiri na muona mbali hujibu kwa hoja na si maneno ya shombo kama wengine mjibuvyo. uko sawa ben.
 
Hapo sawa kabisa, kwa kulopoka kwao na kutofikiri kimsingi na kiupana wanaisi lisu kawatusi, alafu kingine nashangaa wa2 wote mnaoisi lisu katukana mbona hamna Facts za kutosha na Ushawishi wenye visibitisho ili watanganyika tuwaelewe? Nchi yetu Kama mlizoea dezo jua mwisho wenu unakaribia kama sio kuisha.
 
Mwl. Nyerere alikuwa binadamu na alifanya makosa mengi ya kutokujua na ya makusudi kwahyo tusipoteze muda kumtetea na kamanda Lisu amemaliza kazi! Nadhan sasa wanaong'ang'ania serikal 2 waone aibu na wapige hatua 5 tu za kufikiria kama kweli ni wasomi.
 

Nilisikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.


Edwin Mtei
Founder Chairman of CHADEMA.
 
Kwa kauli izo za Tundu Lissu ni sawa na kumwambia baba yake hajui kutomba........sasa ajiulize alimzaa vp
 

kama unaamini kauli za Lisu kuhusu Nyerere ni kauli za kistaarabu, basi ama wewe ni Lissu mwenyewe au unashabihiana nae kwa ukaribu sana. Kama mimi ningekuwa Lissu, ningesema hata nimekuwa"quoted" out of context. Morinho alimuta eto babu lakini aakaomba 'radhi' ki-mourinho kwa kusema yale aliyoyasema hayakupaswa kuwekwa wazi.

Hivyo vifungu unavinukuu hapo juu kwa sababu ya elimu ambayo huyo mchonga alipigania kwa njia halali na Haramu uipate wewe na kizazi chako.SMH
 
Nakubaliana kabisa na ndugu Ng'wamapalala kwamba kuna mapungufu ya fikara kwa baadhi ya wabunge, kama Mheshimiwa Tundu Lisu. Nyerere alikuwa kiongozi aliyejua kazi na nafasi yake Katika jamii. Siku zote alijua kuongoza na kutawala watu ni kusimamia kwa uadilifu taratibu na kanuni Ilizowekwa; kama katiba na sharia za nchi. Kusimamia taratibu na kanuni ni kuwafikia ha kila mhusika, bila una guide, anazingatia utekelezaji na anayekiuka anachukuliwa hatua site hiking. Hilo ndilo Nyerere alikuwa akiyanya alipowachukulia hatua wote waliojaribu kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inaelekea Tundu ni mwanasheria asiyejua, au aaiyethamini utawala wa sharia. Umuhunyari.
 

- Saafi sana hatimaye wazee wa zamani wa JF mmeanza kujitokeza naona mmeona hawa watoto wanakwenda mbali sana na matusi kwa Taifa, kaka wape darasa hawa watoto wadogo wasiojua kitu huu mjadala mimi nakuachia mkuu nakuaminia sana!!

ES
 
Huyu jamaa kweli nimeamini ni mgonjwa wa akili.
Source: Kigwangala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…