Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

neno uongo si tusi..
hayo mengine ni misemo ambayo hata kwenye kanga ipo..so hakuna cha ajabu..
mnatafuta huruma ya umma tu hakuna chochote

We unaweza kumwambia mzazi wako, kwamba amezowea vya "Haramu vya halali haviwezi" na pia "amezowea vya kunyonga na vya kuchinja haviwezi", na "Amezowea kuishi kwa uongouongo na hawezi kuishi katika kweli"! We binafsi unaweza kumwambia hivyo Mzazi wako?
 
Tundu Lisu kasema yafuatayo:
-Hati ya Makubaliano haipo hadi UN. Tanganyika iliondolewaje UN? Mjinga Tundu Lisu.
-Kwamba wapo waliozoea vya kunyonga na haramu. Mpasho huu wa kijinga aliuelekeza kwa nani, kwa lipi?
-Kwamba Mwalimu hakuwa Mungu wala Malaika. Sawa kabisa. Hakusema pia kwamba Mwalimu hakuwa Shetani au Luciferi!
-Mtu na akili yako timamu unaambiwa TANZANIA haipo kihalali bado unamshangilia mjinga kama huyu Tundu Lisu?

CCM ndo imemtukana Nyerere kwakutofuata amri zake.
1. Nyerere alikataa Kikwete kuwa rais wa Tanzania. CCM kwa kujiona wanaakili kuliko Nyerere wakakaidi na kumpa JK urahisi.
2. Nyerere alikataa Lowasa kuwa rais wa Tanzania. Lakini kwa dharau na kiburi cha ccm wanamuandaa Lowasa kuwa rais.
3. Nyerere alikataza wanachama wake wa ccm kukimbilia ikulu. kwasasa kila mtu shahidi, zaidi ya wanaccm 12 kila mmoja kwa wakati wake anajitangaza kwamba ndo next president.
Sasa tujiulize. Kati ya lisu na CCM nani kamtukana Nyerere. BTW lisu kamsifu Nyerere lakini ccm wamempuuza Nyerere. Sasa je aliemsifia Nyerere na aliempuuza yupi kamtukana Nyerere?
 
Kwa nini Ahdul Jumbe u Mjimwema ?
 
- tunawasamehe wenye akili lakini sio wendawazimu kama Tundu Lissu ametukana Mwalimu halafu amemtukana na Mzee Mtei, inaa maana kwao huyu mbunge wenu hakuna wazee wala watuwazima hivi amesoma nini hasa kinachomfanya ajione ana akili sana kuliko Mwalimu na Mtei?

- Chadema mnacheza siasa za self-destructions badala ya kuja kuo,mba radhi mnakuja na hizi? Subiri hii habari kwenye uchaguzi ujao mbona itakuwa super sana!!

Le Mutuz System

CCM ndo imemtukana Nyerere kwakutofuata amri zake.
1. Nyerere alikataa Kikwete kuwa rais wa Tanzania. CCM kwa kujiona wanaakili kuliko Nyerere wakakaidi na kumpa JK urahisi.
2. Nyerere alikataa Lowasa kuwa rais wa Tanzania. Lakini kwa dharau na kiburi cha ccm wanamuandaa Lowasa kuwa rais.
3. Nyerere alikataza wanachama wake wa ccm kukimbilia ikulu. kwasasa kila mtu shahidi, zaidi ya wanaccm 12 kila mmoja kwa wakati wake anajitangaza kwamba ndo next president.
Sasa tujiulize. Kati ya lisu na CCM nani kamtukana Nyerere. BTW lisu kamsifu Nyerere lakini ccm wamempuuza Nyerere. Sasa je aliemsifia Nyerere na aliempuuza yupi kamtukana Nyerere?
 
Kutoka kamusi ya Kiswahili hapo hakuna tusi hata moja..sijajua nkuulize hivi Baba akiahidi kukuletea zawadi na asipoleta..ukimwambia baba umenidanganya..utakuw umemtukana..

Maccm huwa hayatumii kamusi kutafisili matusi, kwa mfano haturuhusiwi siku hizi kuita jina la M.A.S.A.B.R.I, Jamaa huyu kapoteza jina la ukoo kabakiwa na jina la Didas tu.
 
Tundu Lisu kasema yafuatayo:
-Hati ya Makubaliano haipo hadi UN. Tanganyika iliondolewaje UN? Mjinga Tundu Lisu.
-Kwamba wapo waliozoea vya kunyonga na haramu. Mpasho huu wa kijinga aliuelekeza kwa nani, kwa lipi?
-Kwamba Mwalimu hakuwa Mungu wala Malaika. Sawa kabisa. Hakusema pia kwamba Mwalimu hakuwa Shetani au Luciferi!
-Mtu na akili yako timamu unaambiwa TANZANIA haipo kihalali bado unamshangilia mjinga kama huyu Tundu Lisu?

Wewe na Tundu Lissu nani mjinga??
 
CCM ndo imemtukana Nyerere kwakutofuata amri zake.
1. Nyerere alikataa Kikwete kuwa rais wa Tanzania. CCM kwa kujiona wanaakili kuliko Nyerere wakakaidi na kumpa JK urahisi.
2. Nyerere alikataa Lowasa kuwa rais wa Tanzania. Lakini kwa dharau na kiburi cha ccm wanamuandaa Lowasa kuwa rais.
3. Nyerere alikataza wanachama wake wa ccm kukimbilia ikulu. kwasasa kila mtu shahidi, zaidi ya wanaccm 12 kila mmoja kwa wakati wake anajitangaza kwamba ndo next president.
Sasa tujiulize. Kati ya lisu na CCM nani kamtukana Nyerere. BTW lisu kamsifu Nyerere lakini ccm wamempuuza Nyerere. Sasa je aliemsifia Nyerere na aliempuuza yupi kamtukana Nyerere?
Hii mada nyingine kabisa.
 
Haya ndiyo mawazo ya BAWACHA.

"Umezoe vya kunyonga vya kuchinja huviwezi, Umezoea vya haramu vya halali huviwezi" umeambiwa utaje matusi aliyotukana Tundu Lisu anaharakishia kwa vya kuyonga.
 
Uongo linakuwa sio tusi kama kilichofanywa, kilichosemwa au kilichotendwa ni uongo kweli. Kipi katika MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar ni uongo? Hati ya Makubaliano ya Muungano haipo kama alivyosema mjinga Tundu Lisu?

Unaikumbuka approach ya JJ Mnyika kwenye suala hili? Ulimsikiliza Evod Mmanda kwenye suala hili?
Ni hiyo hati ya makubaliano kutoridhiwa na Baraza la mapinduzi kulingana na matakwa ya makubaliano yenyewe, kilikuwa kinakwepwa kitu gani? Na hilo limethibitishwa na wengi akiwemo Jumbe aliyekuwa mjumbe wa baraza hilo 1964-1984. Kama ulivyoandika mwenyewe, kwa kuwa alichosema Lisu ni ukweli, dhana ya matusi haipo.
 
Binadamu yeyote mwenye akili timamu huwezi kutukana marehemu ntarahamwe pekee na warabu kwa sheria za uislamu na mwizi ndo watu huwa wanajilizisha kupiga maiti na mwingine ameongezeka kwenye hili kundi la kutukana marehemu R.I.P tundu
 
Sijui kwa nini wanasema Tundu Lissu katukana. Je; kueleza uyajuayo kuhusu kitu fulani ni unatukana? Hapa namsikiliza Prof. Palamaghamba Abudi Live TBC anachokieleza hakina tofauti na anachokifanya Tundu Lissu. Tangu enzi ya Mwl Nyerere ilikuwa ukisema ukweli wewe ni msaliti na huna adabu. KUTHUBUTU kwa Tundu Lissu kueleza suala la Muungano ulivyokuwa wa giza giza imekuwa ISSUE ON TABLE. Hao ndio watu wanaostahili kuwepo kwenye serikali ya sasa. Lazima ukweli usemwe vinginevyo matatizo yatakuwa mengi sana huko mbeleni.

Nasikitishwa sana na wanaomtukana Tundu Lissu. Tujiulize leo hii nani angejua kama hati ya muungano ipo hata kama haieleweki. Wanasheria wa wakati huo na hata Makatibu walikuwa hawajawahi kuiona kwa miaka 50 ya uhai wa muungano. Hivi siyo suala la kumpongeza Tundu Lissu? Au watanzania wanataka tuwe kama Lukuvi anatutisha watu wazima nyau? Lukuvi na Tundu Lissu nani apigwe mawe? Kututisha kwamba tukiwa na serikali tatu jeshi litakosa mapato na hivyo kupindua nchi hii ni akili au matope?

Labda tumuulize Lukuvi, Rais amekuwa akianzisha mikoa na wilaya na matokeo ya hayo yote ni kwamba zinazaliwa kata, vijiji na vitongoji, je; pesa za kuendesha mikoa mipya, wilaya, Hivi kuna mtoto anazaliwa akiwa amevaa nguo au huwa zinatofutwa zinazomtosha? Hawa ndio mawaziri wenye dhamana na rasilimali za nchi tena Mnadhimu upande wa Serikali. Inaonekana hata mawazo aliyotoa Rais bungeni kwamba nchi itachukuliwa na jeshi alishauri yeye.

Wabunge acheni ushabiki kwa sababu mtarudi tu huku mtaani tutawauliza mlienda kufanya nini. Msichangie ili mpendwe na wanachama wenu au rais wenu, changieni mpendwe na WATANZANIA. There will be a day when the so-called chama won't exist.

Naomba kutoa hoja
 
- Mwalimu alikuwa na tabia ya kuishi kwa uongo uongo na ujanja ujanja, ndio maana hata huu muungano wake hauna hati, unasema haya sio matusi? kwa baba wa Taifa?

- Kaka soma Jambo Leo kesho uone hii habari nimeiweka vizuri sana kule!!

Le Mutuz System

Kwani ni uongo, mwalimu alikuwa anaishi kwa ujanjaujanja, uwongo ktk hili suala la muungano, muungano gani wa kuongea leo kesho nchi zimeungana, hati hakuna, muungano wa watu wawili, aliyeuliza kuhusu muungano aliuawa au kuwekwa kizuizini.
Ukiambiwa wewe ni muongo hilo ni tusi??
Hilo gazeti la jambo leo si ndiyo lile la wauza unga au na wewe ni mmoja wao??
Msalimie Juma Pinto mwambie border la Uzberkistan ndiyo poa kwa sasa
 
tatizo watanzania maneno mingiiiiiiiii!bungeni ukimuita mtu MUONGO wanakuambia futa kauli sema HAJASEMA UKWELI!Hapo huwa nashangaa sana mtu ambaye hajasema ukweli maana yake kasema uongo na ni muongo tu!
 
Tundu Lissu mwenyewe amekiri sasa sijui wewe unakataa nini. Lissu amemwambia Nyerere ameisha kwa uwongo maisha yake yote. Alizoea vya haramu. Wewe bado huoni kwamba hayo ni matusi. Kubalini tu kwamba hapa jamaa alichemsha big time yaishe.

Sasa huo ni ukweli siyo tusi au huko ugambani mtu akisema ukweli anaambiwa ametukana
 
sijajua maana ya tusi na kukosolewa haya ni maajabu nyerere kakosolewa,maatahira mengine yakuja na mawazo mgando kwamba ametukanwa mjinga ni mjinga tu
 
Ni hiyo hati ya makubaliano kutoridhiwa na Baraza la mapinduzi kulingana na matakwa ya makubaliano yenyewe, kilikuwa kinakwepwa kitu gani? Na hilo limethibitishwa na wengi akiwemo Jumbe aliyekuwa mjumbe wa baraza hilo 1964-1984. Kama ulivyoandika mwenyewe, kwa kuwa alichosema Lisu ni ukweli, dhana ya matusi haipo.
Rasimu ya sasa sura ya kwanza, sehemu ya kwanza kabisa inaondoa kabisa huo utata wa Zanzibar kutoridhia hati ya makubaliano. Kwa hali ilivyokuwa Zanzibar wakati ule sio rahisi kufahamu kama Baraza la Mapinduzi halikuridhia hati ile. Alichokuwa anatafuta Sheikh Karume wakati ule ni namna ya kuyalinda Mapinduzi yale.

Ujinga wa mwenzetu Tundu Lisu ni ile kutangaza kwa nguvu kabisa kuwa hati ya makubaliano haipo kabisa kwa kuwa tu aliiomba hakupewa. Hati ilipoonyeshwa akaanza kujadili sahihi ya Marehemu Karume!
 
Back
Top Bottom