Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

We unaweza kumwambia mzazi wako, kwamba amezowea vya "Haramu vya halali haviwezi" na pia "amezowea vya kunyonga na vya kuchinja haviwezi", na "Amezowea kuishi kwa uongouongo na hawezi kuishi katika kweli"! We binafsi unaweza kumwambia hivyo Mzazi wako?

Kwani uongo?
 
sijajua maana ya tusi na kukosolewa haya ni maajabu nyerere kakosolewa,maatahira mengine yakuja na mawazo mgando kwamba ametukanwa mjinga ni mjinga tu
Hakuna anayekataa Mwalimu kukosolewa kistaarabu kwa hadhi na heshima yake. Sio kwa kuanza na maneno yanayoandikwa kwenye kanga wanazovaa akina mama.

Tundu Lisu yuko kwenye Bunge la JMT. Bunge ambalo kwa maelezo yake ya sasa halipaswi hata kuwepo. TL na chama chake ni waasisi halisi wa mchakato wa KATIBA MPYA. Walikuwa wanataka katiba ya NCHI gani?
 
Tundu lissu jasiri pekee Tanzania aliyethubutu kumkosoa mwl.nyerere
Mwl.nyerere hakua Mungu kwamba kila alilofanya ni sahihi hivyo hapaswi kukosolewa
 
Huna hoja wewe kaa kimya,usituletee mambo ya kanisa humu,nenda ahubiri kanisani na sio humu kwenye jukwaa letu,au umeumwa na maccm????tumia akili
 
safi sana mjumbe kwa kumpa fact huyo mburula anaemsifu nyerere kama mtakatifu fulani hivi,mbona watu hamtumii akili??Nyerere hakuwa mtakatifu bali alikuwa binadamukama wewe
 
Utata Wa Kifo cha Mwalimu Nyerere - Mwanzo



Madaraka Nyerere azungumza
Madaraka Nyerere, mmoja wa watoto wanane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, amezungumza na kusema ingawa haafiki kuanza uchunguzi wa kifo cha babake, lakini kuna viashiria fulani fulani vinavyotia shaka.
Viashiria hivyo, kwa mujibu wa Madaraka, ni namna alivyoanza kuikosoa Serikali kwa mambo mengi, jambo analosema inawezekana halikuwafurahisha wengi.

KIFO CHA NYERERE NI UTATA

Tangu mwaka jana juhudi za chini chini zilianza kufanywa na baadhi ya Watanzania ambao hawajaridhika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifariki kifo cha kawaida.Wito sasa umeanza kutolewa wa kuhakikisha kuwa kifo hicho kinachunguzwa kama inavyofanywa sasa kwa aliyekuwa Kiongozi wa Palestina, Yasser Arafat, ambaye taarifa za karibuni zinasemekana kuwa aliuawa kwa kulishwa sumu.

Baadhi ya wafuasi wa Mwalimu Nyerere, wamekuwa wagumu kuamini kama kweli Mwalimu alikufa kifo cha kawaida, kutokana na ukweli kwamba maradhi yaliyomuua - saratani ya damu (leukemia) - hayana desturi ya kuua kwa kasi kama ilivyotokea kwake. Samuel Kasori, aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu, amezungumza na JAMHURI na kusema; "Mwalimu anakuwa kwenye rekodi ya kufa haraka sana kwa ugonjwa wa saratani ya damu. Ugonjwa huo huua taratibu, lakini kwa Mwalimu ilikuwa tofauti kabisa. Kuna nini kilichotokea? Sitaki kuhoji sana, lakini naamini kuna siku Watanzania na walimwengu wataujua ukweli." Maneno ya Kasori yanaendana na ya Mwalimu James Irenge (Mwalimu wa Baba wa Taifa), aliyoyatoa mwanzoni mwa mwaka jana baada ya mvutano wa kisiasa kati ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema). Baada ya kauli ya Mbunge Nyerere kumtaka Mzee Mkapa aeleze chanzo cha kifo cha Mwalimu, Mwalimu Irenge alijitokeza na kusema amefurahishwa mno kusikia kuwa amepatikana kiongozi jasiri wa kuhoji namna Mwalimu alivyougua hadi kufariki dunia. "Mfikishieni pongezi nyingi Mbunge Nyerere... huyo mtoto amefanya jambo la maana sana kuuliza jambo hili, miaka yote nalia kwa sababu naamini Mwalimu aliuawa. "Kwa kuwa suala hili limeulizwa hadharani, sasa nipo radhi kufa. Nikifa nitakwenda moyo wangu ukiwa na furaha kwa sababu nimekuwa nikijiuliza ni nani anayeweza kuhoji namna Mwalimu… mwanafunzi wangu alivyokufa," alisema Mwalimu Irenge. Kauli hiyo ya Mwalimu Irenge ya Machi, mwaka jana haikupita bure, kwani Julai, mwaka huo, aliaga dunia mjini Musoma na kuzikwa kijijini kwake Busegwe Nyanza wilayani Butiama.Mwalimu Irenge alianza kumfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge kuanzia mwaka 1934 hadi 1936. Mwalimu Irenge aliwahi kuhojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na kusema, binafsi hakuafiki Mwalimu kupelekwa kutibiwa nchini Uingereza. Alisema alipinga kwa sababu alijua Waingereza si marafiki wa kweli wa Mwalimu, kwa kuwa aliongoza harakati za kuwang'oa katika Tanganyika na katika mataifa mengine, hasa Afrika Kusini na Zimbabwe, ambako Serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikiunga mkono utawala wa kidhalimu wa Wazungu wachache.Mwakyusa na kifo cha MwalimuProfesa David Mwakyusa alikuwa daktari wa Baba wa Taifa tangu mwaka 1987 hadi Oktoba 14, 1999, siku Mwalimu alipofikwa na mauti jijini London, Uingereza, kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu (leukemia). Katika mahojiano aliyopata kufanya muda mfupi baada ya kifo cha Mwalimu, Profesa Mwakyusa alisema walimjulisha Mwalimu kila kitu kuhusu ugomjwa wa leukemia. Hata hivyo, kwenye maelezo yake anathibitisha namna ugonjwa huo ulivyobadilika ghafla na kumsababishia mauti, ilhali kila alipopimwa ilionekana hakuwa na sababu za kuanza matibabu mapema. Swali: Mwalimu alikuwa anajulikana kwa Watanzania kama mtu mwenye afya nzuri. Wewe kama daktari wake unasemaje kuhusu afya ya Mwalimu kwa ujumla. ibu: Mwalimu alikuwa mtu mwenye afya nzuri kwa ujumla, ukiacha matatizo madogo madogo ninayoweza kuyaita ya kawaida. Alikuwa na desturi ya kufanya mazoezi na alikuwa mtu anayefuata masharti na ushauri aliokuwa akipewa na madaktari. Daktari wa kwanza aliyekuwa anamhudumia Mwalimu baada ya Uhuru alikuwa Profesa Mhonoli. Kuanzia mwaka 1979 alihudumiwa na Profesa Makene akisaidiwa na Profesa Mtulia na mimi. Mwalimu alipostaafu mwaka 1985 alibakia daktari mmoja tu, Profesa Makene. Makene alistaafu mwishoni mwa mwaka 1987 na tangu wakatu huo mimi ndiye niliyekuwa daktari wake hadi alipoaga dunia tarehe 14 Oktoba 1999. Swali: Baada ya kulazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, ndipo Watanzania tulipotangaziwa kwamba Mwalimu aligundulika kuwa na ugonjwa wa kansa ya damu mwishoni mwa mwaka 1998. Je, ugonjwa huu unafikiri aliupataje? Jibu: Ugonjwa wa kansa ya chembe chembe nyeupe za damu, huwapata watu wenye umri mkubwa na utafiti wa kisayansi haujafanikiwa kutambua ni kitu gani hasa kinacholeta kansa hii. Kwa kawaida, kansa hii haioneshi dalili wakati inapoanza na wengi wanagundulika kuwa nayo bila kuihisi.Wagonjwa wengi wanaishi zaidi ya miaka miwili bila kuhitaji matibabu, ni pale tu ambako kansa hii inapoathiri kazi ya chembe chembe nyingine nyeupe au nyekundu ndipo matibabu yanapoweza kufikiriwa. Kinachohitajika ni mgonjwa kuonwa na daktari mara kwa mara, ili athari hizi zikionekana matibabu yaanze mara moja. Swali: Baada ya kugundulika kwa ugonjwa wa Mwalimu, ulimshughulikia namna gani? Jibu: Baada ya Mwalimu kugundulika kuwa na kansa mwezi Agosti 1998, alielezwa kuhusu ugunduzi huo na kuambiwa kuwa wakati ule ugonjwa ulikuwa haujafikia hatua ya kuhitaji matibabu. Alielezwa haja ya kwenda kupimwa mara nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa kawaida yake na kwamba hapakuwa na sababu ya kubadilisha mwenendo wa shughuli zake.Ratiba tuliyopewa ilimfanya Mwalimu arejee London, Novemba 1998, na majibu yaliyoonesha kuwa hakukuwa na sababu ya kuanza matibabu. Aidha, mwezi Januari 1999 alipimwa tena kwa mara nyingine ikaonekana hakuna haja ya kuanza matibabu. Mwezi Mei 1999 alikwenda tena London akapimwa. Aliambiwa hakukuwa na sababu ya kuanza matibabu na akapewa tarehe nyingine mwezi Agosti, 1999.Safari hii hitilafu zikaonekana katika damu. Hitilafu hizo zilionesha ulazima wa matibabu ya kansa kuanzishwa. Mwalimu alishauriwa kurudi London, Desemba 1999. Lakini hali yake ikabadilika kabla ya kurejea nyumbani hadi ikabidi alazwe katika hospitali ya Mtakatifu Thomas ambako alipoteza maisha yake. Swali: Mmoja wa watoto wa Mwalimu amedai kuwa familia haikujulishwa kuhusu ugonjwa wa Mwalimu. Kuna ukweli wowote katika madai hayo? Jibu: Mwalimu mwenyewe aliwaeleza baadhi ya wanafamilia yake waliokuwa karibu naye, kuhusu maradhi yake na mimi nilijua hivyo kwa vile hao aliowaeleza waliniambia na wakawa wakiniuliza maswali kuhusu ugonjwa wake. Swali: Ukiwa daktari wa Mwalimu kwa muda mrefu, uliyekuwa ukisafiri naye mara nyingi na kuwa naye karibu, je, unaweza kuzungumzia lolote kuhusu maisha yake?Jibu: Mara nyingi tukiwa pamoja aliuliza maswali mengi kuhusu ugonjwa wake na alisoma vijitabu kuhusiana na ugonjwa huo. Nadiriki kusema kwamba aliufahamu ugonjwa huo kwa kina.Madaraka Nyerere azungumzaMadaraka Nyerere, mmoja wa watoto wanane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, amezungumza na kusema ingawa haafiki kuanza uchunguzi wa kifo cha babake, lakini kuna viashiria fulani fulani vinavyotia shaka. Viashiria hivyo, kwa mujibu wa Madaraka, ni namna alivyoanza kuikosoa Serikali kwa mambo mengi, jambo analosema inawezekana halikuwafurahisha wengi.Katika mahojiano yake na JAMHURI wakati huu wa maadhimisho ya miaka 14 ya kifo cha Baba wa Taifa, Madaraka ambaye kwa kawaida ni mpole, ameeleza yafuatayo: "Binadamu wengi wanapenda sana kuamini kuwa kila jambo likitokea, basi kuna mkono wa mtu. Na hivi karibuni kifo cha Mwalimu Nyerere kimehusishwa na njama mahususi za kumuua. "Kwa desturi za Kizanaki, hakuna mtu anayekufa kwa sababu ya ugonjwa au uzee, lazima yuko mtu miongoni mwa wale waliobaki hai ambao wamesababisha kifo chake kwa njia za uchawi. Kwa mfano, Bibi Christina Mugaya wa Nyang'ombe, mama mzazi wa Mwalimu Nyerere, mara baada ya kifo cha mume wake, Mtemi Nyerere Burito, tarehe 30 Machi 1942, alitimuliwa Butiama na kuhamia kwa ndugu zake katika kijiji jirani cha Muryaza, baada ya kutuhumiwa kuwa alisababisha kifo cha mume wake. "Kwa hiyo hakurithiwa kama ilivyo desturi za wakati ule za mila za Kizanaki na akaishi kwa jamaa zake hadi Mwalimu Nyerere alipotoka masomoni Uingereza na kudai arudi nyumbani na akarudi, ingawa baadhi ya ndugu zake hawakufurahia kurudi kwake Butiama. "Kwa hiyo basi, ni kawaida kabisa kwa hisia kama hizi kuwapo ndani ya jamii. Lakini, kusema hivi haina maana kuwa haiwezekani kuwa tuhuma hizo ni za kweli. Lakini mtu yeyote muungwana hawezi kuanza kutoa shutuma nzito kama hizi bila kuwa na ushahidi usiotiliwa shaka na ambao hauna dosari. "Lakini naweza kuelewa kwanini baadhi ya watu ambao wanashikilia hizi tuhuma kuwa zinaweza kuwa ni kweli. Tunamfahamu Mwalimu Nyerere kuwa, hata baada ya kustaafu, hakukalia kimya uamuzi au matukio ambayo aliamini yanaathiri baadhi ya misingi ambayo yeye aliiona kuwa ni nguzo inayoshikilia nchi yetu. Baadhi ya haya ni uadilifu ndani ya uongozi, umoja, uzalendo, na sera zenye kujali masilahi ya wengi badala ya sera zinazokuza na kulinda nafasi kwa wachache kujinufaisha. "Na kwa kweli ukichunguza baadhi ya matukio kwenye nyanja ya siasa katika kipindi hiki ambacho amefariki, yametokea mengi ambayo tunaamini kuwa kama angekuwa hai asingenyamaza na angeyazungumzia kuyapinga na kuyakemea au kuyatungia kitabu pale ambako ujumbe wake aliona unapuuzwa. Kwa hiyo, mtu yeyote anayefuatilia hali ya uongozi nchini, na watu wengi wanasema hivi, ni kuwa Mwalimu Nyerere angekuwapo labda baadhi ya uamuzi na mienendo ya baadhi ya viongozi wetu ungekuwa tofauti kwa kuogopa kauli yake au kuandikiwa kitabu , kitakachojenga hoja inayopingana na uamuzi wa viongozi. Na pengine baadhi ya uamuzi ambao umefanyika, usingefanyika. "Kwa hiyo kwa mantiki hii unaweza kuanza kujenga hoja kuwa baadhi ya wale waliofanya uamuzi unaoonekana unaenda kinyume au na maadili ya uongozi, au unapingana na masilahi ya umma, walitafakari kuwa njia rahisi ya kurahisisha mipango yao ni kumuondoa huyu mzee mapema. Hiyo unaweza kusema, lakini haitakuwa sahihi kufanya hivyo bila kuwa na ushahidi. "Nimewahi kusikia tuhuma kuwa Rais Kikwete anatuhumiwa kuwa ndiye mtu aliyetumwa na nchi za Magharibi kukimaliza Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nilivyosikia tuhuma hizi niliona kichekesho, lakini ukiangalia baadhi ya matukio katika uongozi wake ambayo yanaweza kuashiria hoja hiyo, unaweza kuyapata. "Enzi za Mwalimu Nyerere waliotuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya uongozi waliitwa pembeni na kuambiwa wajiuzulu. Miaka ya hivi karibuni wale ambao walikabiliwa na tuhuma za aina hiyo waliombwa kutafakari wao wenyewe uamuzi sahihi wa kuchukua. Uamuzi mgumu haufanyiki, upinzani wanapata mada ya kuzungumzia kwenye mkutano wao ujao, na CCM inazidi kudhoofu. Kama nilivyosema hakuna ushahidi wa wazi, lakini kuna viashiria tu. "Nafikiri njia nzuri ya kufunga mjadala huu ni kuzungumza kama wanasheria wanavyosema: hakuna ushahidi mpaka sasa unaothibitisha hizo tuhuma juu ya njama za kumuua Mwalimu Nyerere. "Hoja kuwa uchunguzi ufanyike kubaini kama aliuawa, sioni kama zitaleta faida yoyote kwa sababu ameshafariki tayari na hakuna uchunguzi utakaorudisha uhai wake. Tunamkumbuka Mwalimu Nyerere kwa maandishi na matamshi yake. Na naamini kuwa katika uhai wake aliandika na kutamka masuala yote aliyoamini ni ya msingi kwake na kwa jamii. "Kuna kiongozi mmoja aliyewahi kusema iwapo kuna wazo la msingi ambalo binadamu amelisema katika uhai wake, basi hilo wazo litadumu hata kama aliyelisema hayuko tena duniani. Badala ya kutafuta wachawi sasa hivi, mimi nafikiri wale wote ambao wanaamini kuwa Mwalimu Nyerere alitoa mchango mkubwa kwa nchi hii, watumie muda wao kutafakari kazi aliyofanya na kujumuisha fikra zake na matendo yake kupima yale ambayo bado yanaweza kuwa suluhisho dhidi ya baadhi ya changamoto zinazoikabili Tanzania sasa hivi. "Iwapo hoja zake zina nguvu katika mazingira ya sasa, basi hazihitaji yeye mwenyewe kuzisemea. Wanaoziamini wazichambue na wazitumie kama silaha ya kupambana na upungufu ambao tunauona leo katika nyanja mbalimbali. "Lakini pia ni muhimu kwa vijana kujitafutia elimu kuhusu hayo yaliyopita, ili kupata mifano mizuri ya uongozi ambayo iliweka masilahi ya Taifa mbele na kuzuia kabisa hizi hoja za siku hizi za kumpa kila mtu fursa ya kufanya anavyotaka. Zinazungumzwa fursa za mwananchi, lakini ukweli ni kuwa baadhi ya viongozi wanapigana vikumbo na wananchi hao hao kutafuta fursa zao binafsi," amesema Madaraka.
 
Leo mtasema mnamuenzi baba wa taifa...kesho mnasema uyo baba. wa taifa ni mwongo na kila alichofanya ni haramu na ndio tabia yake vya haramu...Nyie angalieni sana,sie tunawachora tu.
 
Tundu lissu jasiri pekee Tanzania aliyethubutu kumkosoa mwl.nyerere
Mwl.nyerere hakua Mungu kwamba kila alilofanya ni sahihi hivyo hapaswi kukosolewa
Ni kweli Mwalimu hakuwa Mungu. Hakuupenda kabisa utukufu. Watu wote kwake walikuwa NDUGU. hakukuwa hata na waheshimiwa! Ni kweli pia kwamba Mwalimu hakuwa shetani. Hakutuibia kabisa.

Hili la kuambiwa na Tundu Lisu kwamba alizoea vya kunyonga, alizoea vitu haramu, alighiribu watu kwa ujanjaujanja ili iweje? Kuna anayeweza kutuambia Muungano huu ulimnufaisha vipi Mwalimu hadi aulinde kiharamu?
 
Anayemuenzi Nyerere nani? ccm hii ninayoijua? Mara ngapi jk amem-quote Nyerere ktk hotuba zake? yapi ameyafanya kuonesha anamuenzi Nyerere...

by the way kitu gani hakibadiriki...mbona tu nchi nyingi zomebadiri majina na bado maisha yakaendelea vizuri....mnachoogopa nini! Lisu ni shujaa kama alivyo Warioba.

Tumwombe Mungu tu Warioba awe mpole zaidi ya kondooo. Sidhani kama hana support ya kutosha akimua ku-revange in any way possible...anatukanwa kama mtoto mdogo! Jk hii nchi akiaxha salama tutamshukuru Mungu.
 
Mkuu nimekusoma vyema sana.

Kifupi Nyerere alifeli karibia asilimia 70 ya kila jambo lake aliloliasisi. Alifeli mengne hata kabla hajaanza kuyatekeleza. MUSOMA RESOLUTION lilifeli hata kabla halijaanza kutekelezwa, AZIMIO LA ARUSHA lilipelekea Taifa kuwa maskini hata kufikia nchi kuwa katika kumi za mwisho kwa hali mbaya ya uchumi. Alifeli kwakuwa hakuwa na strategia za kufikia yale malengo yake ispokuwa alikuwa ni mbinafsi na aliyetaka kujijengea umaarufu binafsi wakati kulikuwa na watu waliomzidi kimaarifa na ufahamu wa sera ya ujamaa kama ABDURHAMAN BABU. Hakutaka kujifunza bali alivamia sera ya ujamaa kwakuwa tu ilikuwa yafavour malengo yake ya kidikteta.

Mjamaa gani hata umeumwa unaenda kutibiwa nchi ya makapitolisti? Hakuwa mjamaa bali aliuchagua ujamaa kwakuwa unaendana na uongozi aliyoutaka. Haya ndio Watanzania wasiopenda kuyasema wala kuyasikia ndio maana aligeuzwa Mungu mtu kumbe hana lolote.
KWELI LISSU AJIANDAE KUKUMBUNA NA CHANGAMOTO.

Cc zumbemkuu Elli.
 
Last edited by a moderator:
Azimio la Arusha lilivunjwa Nyerere akiwa hai, na kwa ridhaa yake maana hakulikomalia kama lile la G55 na TANGANYIKA yao!
Azimio la Arusha lilivunjwa wakati DUNIA nzima ikifanya kinachoitwa 'STRUCTURAL ADJUSTMENT' baada ya mfumo wa ujamaa DUNIANI ukionyesha kushindwa kuhimili mapigo ya VITA VYA BARIDI mnamo miaka ya 1980 ya mwishomwisho!
KWAHILI LA KUVUNJA AZIMIO LA ARUSHA NAOMBA WATANI ZANGU BORA MNYAMAZE!
NA KUHUSU 'ATI KUNA' WATU NYERERE ALIKUWA HAWATAKI VILEVILE MNAONGEA BILA USHAHIDI, HEBU TULETEENI USHAHIDI NA SAHIHI MTUONYESHE! (TUMEISHAWAONYESHA MKATABA WA MUUNGANO!)

mbona hueleweki?nahisi hujasoma vitabu vya historian vinavyoihusu Tanzania labda umepewa majalada ya ccm tu,kama azimio la arusha lilivunjwa ili kuondokana na mfumo wa ujamaa je Tanzania kwa sasa ni nchi inayofuata mfumo upi ulio lasmi kiuchumi?nini matokeo baada ya kuvunja azimio la arusha watanzania wamefanikiwa?ama ccm ndio wamefanikiwa? kama mfumo wa ujamaa ulikuwa kikwazo kwa kukuwa kwa uchumi wa Tanzania je vipi kuhusu mataifa kama China,urusi na Qiuba ilikuwa vipi wao wakafanikiwa chini ya siasa za ujamaa?unataka kujua watu waliokataliwa na mwalimu kisa walikua na mitazamo tofauti,Oscar kambona,Prof.Abrahaman Babu,Abdul jumbe na wengine wengi sasa kama we ni -------- utapingana na ukweli daima.
 
Leo mtasema mnamuenzi baba wa taifa...kesho mnasema uyo baba. wa taifa ni mwongo na kila alichofanya ni haramu na ndio tabia yake vya haramu...Nyie angalieni sana,sie tunawachora tu.

Chadema wote wana siasa za ulaghai, wanazunguka nchi nzima wakinukuu kauli mbali mbali za Hayati Nyerere zile zinazowapa ahueni ili kupata kura! Sasa wamemdhalilisha marehemu sijui watakwenda na gia gani tena! Watu yawapasa kuwa makini na mijitu hii inayojiita eti chadema mkombozi wa watanzania, hawana lolote zaidi ya kutafuta cheap popularity!
 
Tatizo la watanzania ni pale tunapomfanya Nyerere kama kanuni ya imani. Wakatoliki wananielewa vizuri ninaposema hili. Wakati nikianza mafundisho ya ubatizo tulikuwa na mtihani ambao pamoja na sara zingine ulitakiwa kuijua vizuri kanuni ya imani ambayo inasema nasadiki kwa kanisa katoliki la Rumi. Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi. Nasadiki, Nasadiki, Nasadiki.

Mawazo yako ukiyaweka katika kuamini kwamba hii ndiyo imani uliyoingia kamwe hutaruhusu kusikia upinzani dhidi ya kile ulichokiamini. Wakatoliki watupu wakiingia katika mjadala juu ya imani ya matumizi ya rozari kamwe hatutegemei upande wa pili katika rozari hiyo. Wasabato wawili watupu katika mjadala juu ya ibada ya siku ya jumamosi kamwe hatutegemei kuiona kasoro ya uhakika wa siku hiyo, hali kadharika mashehe wawili wenye imani juu ya mtume hawataweza kuja na jipya juu ya kasoro ya mtume kwa sababu tu kwamba wako ndani ya kanuni moja ya imani.

Inahitaji msuli na ubabe wa hali ya juu kusimama katikati ya watu walioiva katika kanuni ya imani ya matumizi ya rozari ukaanza kuikosoa, Tegemea ukweli alioubainisha "Henrick Ibsen" katika kitabu chake "An Enemy of the Peole". Utaitwa adui mkubwa wa watu kwa sababu umetamuka jambo ambalo watu hawataki kulisikia. Wenye msuli wa hivi mara nyingi humaliza vibaya. Huishia kupotea kabisa kwa sababu hata walio karibu nao hawako tayari kuonyesha kuungana nao kwa sababu wanajua kanuni ya imani iliyo katika jamii wanayopambana nayo. Kama ni ukweli bado utabaki kuwa ukweli lakini dhahili itaonekana wakati wewe tayari umeshapotea katika jamii. Umeshabwagwa kama msaliti.

Nyerere alikuwa binadamu hivyo kuna kasoro alizozifanya, lakini kwa vile ni kanuni ya imani kwa wengi hakuna mwenye ujasiri wa kutamuka kasoro zake. Ukiruhusu akili zako zimuone kama binadamu utaona kasoro zake nyingi tu za ubinadamu.

Kwa mfano: Nyerere kama kiongozi na mdau mkubwa wa muungano wa dunia tangu katika wazo walilokuwa pamoja na Nkrumah kuunganisha Afrika nzima, dunia ilimshangaa alipokubaliana na waasi wa Biafra waliotaka kujitenga kutoka Nigeria. Hiyo ni kasoro ambayo kama akili yako haijaruhusu kanuni ya imani utaiona na kusema kweli binadamu mwenzangu alikosea.

Nyerere aliwahi kusema katika moja ya Bith day part yake kwamba watanzania wananiombea niishi miaka mingi wakati sayansi inasema miaka kuanzia 80 ni ya shida. Nami nashukuru na kwa afya niliyonayo naamini nitafikisha na kuiona 2000. Kama akiri yako haiko katika kanuni ya imani utaiona kasoro kubwa ya ubinadamu wa kutokujua kwamba Mungu ndiye anaamua. Matokeo yake Nyerere hakuiona 2000. Kama akiri yako iko katika kanuni ya imani utapata tafsiri nzuri. Waweza kusema alikuwa akiwafariji watanzania, au lolote la kupamba kauli hiyo.

Tatizo langu kwa Lissu ni uchaguzi wa maneno ambayo unaweza ukatoa ukweli lakini bado ukaacha faraja kwa wadau wa kanuni ya imani. Anayoyasema yote ni kweli. Kuna sababu gani ya kutokuonekana Abdul Jumbe katika matukio mengi ya kitaifa wakati yuko hapa Mji mwema?

Nani aisiyejua kwamba wasira aliwahi kumwendea Nyerere akimfahamisha kwamba safari hii warioba hataupata ubunge kwa sababu watu wamechoka na mikono mitupu. Nyerere kwa kauri hiyo alizunguka majimbo yote ya mkoa wa Mara akiwaambia wasira ni mtoa rushwa mkubwa. Anachinja ng'ombe, anagawa kanga, chumvi ili kupata ubunge jimbo la Bunda. Akawaambia wasira hafai. WARIOBA anafaa. Haya niliyasikia mimi mwenyewe uwanja wa sabasaba Bunda. (kumbuka Lissu alisema kuna watu waliingia upinzani mpaka Nyerere amekufa ndio wakarejea CCM).

Kwa vile siasa inakutaka uwe mnafiki, sasa hivi wasira ndiye mpinga rushwa mkubwa. Ndiye wa kumuenzi baba wa taifa. Sijui kama rushwa alishaacha au lah.

Ndio maana mara nyingi nimekuwa nikisema katika ngazi ya uongozi wa kitaifa lazima uwe mnafiki na wakati mwingine hata mbinu chafu za kuhakikisha msimamo unaouamini kwamba ni muafaka unakubalika katika jamii. Haya yote wanayafanya wanasiasa akiwemo Nyerere na hawa tulionao leo. Hata Lissu akiingia madarakani lazima awe mnafiki na mzoefu wa mbinu chafu.

Namaliza kwa kumwambia Lissu umegusa kwenye kanuni ya Imani, tegemea mashambulizi mengi. Usiposimama imara utapotea. Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika hawatakutetea kwa sababu wanaogopa kugusa kanuni ya imani.

Pengine ni uzalendo na ujasiri wa hali ya juu !
Haya yangejulikana tu
 
"Kwa mfano: Nyerere kama kiongozi na mdau mkubwa wa muungano wa dunia tangu katika wazo walilokuwa pamoja na Nkrumah kuunganisha Afrika nzima, dunia ilimshangaa alipokubaliana na waasi wa Biafra waliotaka kujitenga kutoka Nigeria. Hiyo ni kasoro ambayo kama akili yako haijaruhusu kanuni ya imani utaiona na kusema kweli binadamu mwenzangu alikosea"


Mwalimu amekuwa kwenye UONGOZI wa TAA, TANU na NCHI za Tanganyika na Tanzania kwa muda mrefu sana. Yapo maamuzi mengi tu aliyakosea na baadhi ya makosa yake aliyakiri hadharani yeye mwenyewe.

Tunachomkatalia TL ni namna alivyomkosoa Mwalimu na kuufanya MUUNGANO wetu kuwa kama kituko flani hivi!
 
Sijawahi kuona mtu anaitwa lyimo yuko sawa.

Hili la UBAGUZI ndiyo dhambi kubwa mliyofundishwa na mnaendelea kuieneza katika dini baada ya kufanikiwa kuwatenga watu wa kanda ya kaskazini. Kwanini usinihukumu mimi, bali unanihukumu kwa majina yetu? Hata hivyo kuna mwanajamii aliuliza ni tusi gani kubwa mh. Lissu alilomtukana Baba wa Taifa katika maelezo yake, nami nimeona ndilo hilo. Maana tunasema katukana bila kusema amemtukana vipi.
 
Hivi mtu ukiambiwa uliunda MUUNGANO kiharamu, kwa uongo, kwa kuzoea vya kunyonga haya sio matusi?

Je, ukiambiwa wewe sio Mungu wala Malaika bila ya kuambiwa wewe pia sio Shetani wala Luciferi haujatukanwa?

Ukiambiwa kile kilichosababisha uwepo na uhalali wa MUUNGANO hakipo kabisa hadi UN umesifiwa?

Hata pale unapoonyeshwa kwamba hati ipo bado unadai sahihi za marehemu hawa sizo utajisikiaje?

kwani ukiambiwa we si mungu inamaanisha we ni shetani?yaliyopita si mbele ccm wajinga sana
 
Chadema wote wana siasa za ulaghai, wanazunguka nchi nzima wakinukuu kauli mbali mbali za Hayati Nyerere zile zinazowapa ahueni ili kupata kura! Sasa wamemdhalilisha marehemu sijui watakwenda na gia gani tena! Watu yawapasa kuwa makini na mijitu hii inayojiita eti chadema mkombozi wa watanzania, hawana lolote zaidi ya kutafuta cheap popularity!

nyerere is gone na siyo mungu watanzania si waoga tena lazima tukumwage damu soma ID
 
Back
Top Bottom