Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lisu kasema yafuatayo:
-Hati ya Makubaliano haipo hadi UN. Tanganyika iliondolewaje UN? Mjinga Tundu Lisu.
-Kwamba wapo waliozoea vya kunyonga na haramu. Mpasho huu wa kijinga aliuelekeza kwa nani, kwa lipi?
-Kwamba Mwalimu hakuwa Mungu wala Malaika. Sawa kabisa. Hakusema pia kwamba Mwalimu hakuwa Shetani au Luciferi!
-Mtu na akili yako timamu unaambiwa TANZANIA haipo kihalali bado unamshangilia mjinga kama huyu Tundu Lisu?

Tanzania haipo kihalali kwa kuwa zanziba hawakuridhia
 
"Kwa mfano: Nyerere kama kiongozi na mdau mkubwa wa muungano wa dunia tangu katika wazo walilokuwa pamoja na Nkrumah kuunganisha Afrika nzima, dunia ilimshangaa alipokubaliana na waasi wa Biafra waliotaka kujitenga kutoka Nigeria. Hiyo ni kasoro ambayo kama akili yako haijaruhusu kanuni ya imani utaiona na kusema kweli binadamu mwenzangu alikosea"

Mwalimu amekuwa kwenye UONGOZI wa TAA, TANU na NCHI za Tanganyika na Tanzania kwa muda mrefu sana. Yapo maamuzi mengi tu aliyakosea na baadhi ya makosa yake aliyakiri hadharani yeye mwenyewe.

Tunachomkatalia TL ni namna alivyomkosoa Mwalimu na kuufanya MUUNGANO wetu kuwa kama kituko flani hivi!

kwa hiyo kumkosoa mzee wetu ni kumtukana ?
 
Tanzania haipo kihalali kwa kuwa zanziba hawakuridhia
Ile sahihi ya Mzee Abeid Amani Karume kwenye hati rasmi ya Makubaliano ni ya nini? Au kilikuwa cheti cha ubatizo kile!

Tanzania ilipataje kiti kule UN, OAU, NAM, CHOGM,....,?
 
kwani ukiambiwa we si mungu inamaanisha we ni shetani?yaliyopita si mbele ccm wajinga sana
Hili mbona liko wazi tu. Au kama wewe sio Simba basi ni Yanga kwa lugha rahisi. Hakuna cha Azam hapa ebo.
 
Maamuzi yeyote ya katiba yatategemea kura za BARA na za ZANZIBAR kivyake. Wanaoegemea hoja ya "umungu" wa Nyerere, wakafanye analysis na Zanzibar. Aliyotendewa Abdu Jumbe, Deurado na wengine na Nyerere yatawapa ugumu sana CCM Zanzibar. ..

Na UKAWA wameanzia Zanzibar! A deliberate move?? or a coincidence?!
 
Na UKAWA wameanzia Zanzibar! A deliberate move?? or a coincidence?!
Maeneo kama KibandaMaiti, MchambaWima ndio mahala pa kuanzia watu wa aina hii ambao shujaa wao ni Tundu Lisu.
 
Mkuu nimekusoma vyema sana.

Kifupi Nyerere alifeli karibia asilimia 70 ya kila jambo lake aliloliasisi. Alifeli mengne hata kabla hajaanza kuyatekeleza. MUSOMA RESOLUTION lilifeli hata kabla halijaanza kutekelezwa, AZIMIO LA ARUSHA lilipelekea Taifa kuwa maskini hata kufikia nchi kuwa katika kumi za mwisho kwa hali mbaya ya uchumi. Alifeli kwakuwa hakuwa na strategia za kufikia yale malengo yake ispokuwa alikuwa ni mbinafsi na aliyetaka kujijengea umaarufu binafsi wakati kulikuwa na watu waliomzidi kimaarifa na ufahamu wa sera ya ujamaa kama ABDURHAMAN BABU. Hakutaka kujifunza bali alivamia sera ya ujamaa kwakuwa tu ilikuwa yafavour malengo yake ya kidikteta.

Mjamaa gani hata umeumwa unaenda kutibiwa nchi ya makapitolisti? Hakuwa mjamaa bali aliuchagua ujamaa kwakuwa unaendana na uongozi aliyoutaka. Haya ndio Watanzania wasiopenda kuyasema wala kuyasikia ndio maana aligeuzwa Mungu mtu kumbe hana lolote.
KWELI LISSU AJIANDAE KUKUMBUNA NA CHANGAMOTO.
Sidhani kweli kwa uchambuzi wa viongozi hapa duniani utamwita Nyerere mbinafsi na msaka umaarufu.
 
Azimio la Arusha lilivunjwa Nyerere akiwa hai, na kwa ridhaa yake maana hakulikomalia kama lile la G55 na TANGANYIKA yao!
Azimio la Arusha lilivunjwa wakati DUNIA nzima ikifanya kinachoitwa 'STRUCTURAL ADJUSTMENT' baada ya mfumo wa ujamaa DUNIANI ukionyesha kushindwa kuhimili mapigo ya VITA VYA BARIDI mnamo miaka ya 1980 ya mwishomwisho!
KWAHILI LA KUVUNJA AZIMIO LA ARUSHA NAOMBA WATANI ZANGU BORA MNYAMAZE!
NA KUHUSU 'ATI KUNA' WATU NYERERE ALIKUWA HAWATAKI VILEVILE MNAONGEA BILA USHAHIDI, HEBU TULETEENI USHAHIDI NA SAHIHI MTUONYESHE! (TUMEISHAWAONYESHA MKATABA WA MUUNGANO!)
Kishimbe, ebu sikiliza hotuba ya Mwalimu alivyoongelea Azimio la Zanzibar. Hapakuwa na ridhaa pale maana hasingesema ilifanyika kwa siri, lakini kwa wenye akili tulijua tu Azimio la Arusha limezikwa.
 
Lissu ni mkristo wa kundi gani?
Wakatoliki ndio wanao muenzi zaidi Mwalimu.
Waislam wengi hawamuoni Nyerere kama mwema kwao..
Ccm wao wanatumia kina lake kujipandisha kwa wakatoliki.
Baba wa taifa ni title tu haifanyi kutomkosoa ni dhambi kama wanavo itikadi wakatoliki.
 
Mkuu nimekusoma vyema sana.

Kifupi Nyerere alifeli karibia asilimia 70 ya kila jambo lake aliloliasisi. Alifeli mengne hata kabla hajaanza kuyatekeleza. MUSOMA RESOLUTION lilifeli hata kabla halijaanza kutekelezwa, AZIMIO LA ARUSHA lilipelekea Taifa kuwa maskini hata kufikia nchi kuwa katika kumi za mwisho kwa hali mbaya ya uchumi. Alifeli kwakuwa hakuwa na strategia za kufikia yale malengo yake ispokuwa alikuwa ni mbinafsi na aliyetaka kujijengea umaarufu binafsi wakati kulikuwa na watu waliomzidi kimaarifa na ufahamu wa sera ya ujamaa kama ABDURHAMAN BABU. Hakutaka kujifunza bali alivamia sera ya ujamaa kwakuwa tu ilikuwa yafavour malengo yake ya kidikteta.

Mjamaa gani hata umeumwa unaenda kutibiwa nchi ya makapitolisti? Hakuwa mjamaa bali aliuchagua ujamaa kwakuwa unaendana na uongozi aliyoutaka. Haya ndio Watanzania wasiopenda kuyasema wala kuyasikia ndio maana aligeuzwa Mungu mtu kumbe hana lolote.
KWELI LISSU AJIANDAE KUKUMBUNA NA CHANGAMOTO.
Ni kweli usiofichika kuwa Julius alishindwa kwa kila alilotabiri kwa asilimia 80 na sio sio 70 ni ukweli watu wasiotaka kuuona na jambo la kwanza unalotakiwa kulijua ni siri ya mwenge, serekali mbili mambo ya ajabu ajabu ila alikuwa dicteta hakuna ubishi juu ya hilo umemtaja Marehemu Babu ambaye alimwambia waziwazi " Yakhe wewe wapenda siasa za ewala Bwana"
 
wapo wasomi mbumbumbu wanaoshabikikia ujinga,kila nikiangalia bunge huwa naona kichefuchefu msomi mzima anaunga hoja upumbavu,eti serikali mbili,kisa yupo ccm,jamani niaibu kwa kwel,
 
Lissu ni mkristo wa kundi gani?
Wakatoliki ndio wanao muenzi zaidi Mwalimu.
Waislam wengi hawamuoni Nyerere kama mwema kwao..
Ccm wao wanatumia kina lake kujipandisha kwa wakatoliki.
Baba wa taifa ni title tu haifanyi kutomkosoa ni dhambi kama wanavo itikadi wakatoliki.

Wasiotaka kukosoa ukweli ni wale wanaofaidika na uwongo.Kuna watu waliumizwa sana na utawala wake leo wakijitokeza sijui kama CCM watawafanya nini?Ni wengi mno.Unakumbuka wakati wauhujumu uchumi,je ni wangapi waliowekwa ndani walikuwa na hatia na wangapi walikuwa hawana?Je,waliruhusiwa kutetea au kufunguliwa kesi wajibu mahakamani?Ni kwa nini hawakupelekwa mahakamani,sababu hawakuwa binadamu?AU kwa sababu ya sheri alizokuwa anatunga yeye mwenyewe hazikuwa na impact kwa viongozi aliokuwa nao karibu bali watu wakawaida ndiyo alioumia,kuwekwa magerezani nk.

Kungekuwa na haki hata leo wanasheria wangeanza kuwatetea hawa waliodhulumiwa enzi za uongozi wa Mwalimu ili wapate haki zao hasa familia zao ambapo watoto walioswekwa ndani ndiyo walioumia kwa kukosa ada za shule,malazi,na hata chakula wazazi wao wakiwa jela.

Simlaumu Lissu hata kidogo ni bora ukweli utoke sasa kuliko baadaye.
 
Anayemuenzi Nyerere nani? ccm hii ninayoijua? Mara ngapi jk amem-quote Nyerere ktk hotuba zake? yapi ameyafanya kuonesha anamuenzi Nyerere...

by the way kitu gani hakibadiriki...mbona tu nchi nyingi zomebadiri majina na bado maisha yakaendelea vizuri....mnachoogopa nini! Lisu ni shujaa kama alivyo Warioba.

Tumwombe Mungu tu Warioba awe mpole zaidi ya kondooo. Sidhani kama hana support ya kutosha akimua ku-revange in any way possible...anatukanwa kama mtoto mdogo! Jk hii nchi akiaxha salama tutamshukuru Mungu.
mkuu jk ni dhaifu kuliko maelezo, na atatuacha vibaya sana, hebu chukulia hili la lukuvi lingetamkwa na mpinzani jumuia zote za kiislam mpaka mwisilam mmoja mmoja wangehamasishwa kulaani na kutoa matamko dhidi ya mtamkaji! Sasa hivi naona kimyaaaa au kuna jumuiya yoyote ya kiislamu iliyo laani tamko la Lukuvi?
 
Kimsingi suala la katiba mpya limekufa!Hii katiba inakosa Legitimacy km itaendelea bila ya kuwa na wawakilishi waliotoka kwani nao wanawakilisha watanzania wengi tu!Rais km ana hekima na wanaomshauri wanaona mbali angelivunja hili bunge tuendelee na katiba yetu ya 1977 ambayo ni manifesto ya CCM!!!!
 
Sijaona wala kusikia mtu ambaye ameweza (hata kujaribu) kuja na hotuba mbadala ya kupinga hoja za Tundu Lisu. Tena akitumia taarifa za kitafiti....Hadi hapo tutakapompata mtu wa namna hiyo, ila kwa sasa Lisua ataendelea kuwatesa wanafiki!
 
TISS ifanye mpango wamshugulikie lisu mapema!sijui kwa nini Kikwete anamchekea au ndio kawatuwa wazidi kumchafua mwalim?
 
Hakuna kitu kama kanuni ya imani kwa nyerere kuaminiwa, ubinadamu wake upo palepale, kinachowaudhi wengi juu ya hoja za kutapatapa za lissu ni jinsi anayotoa hoja zake as if what nyerere did 4 this country is useless wakati yeye ni product ya siasa makini na safi za huyo mzee wa watu...ukweli utabaki palepale..Nyerere sio na wala hatawahi kuwa malaika......lakini atabaki kuwa miongoni mwa viongozi na wanafalsafa bora kuwahi kutokea katika bara la Africa kwa kipindi chote alichoishi mpaka sasa
 
Sidhani kweli kwa uchambuzi wa viongozi hapa duniani utamwita Nyerere mbinafsi na msaka umaarufu.

Ubinafsi upo wa aina nyingi sio lazima kuwa wa mali tu bali hata kulazimisha mawazo yako kuwa ndio sheria.
 
Back
Top Bottom